Tafuta

Mapadre wa Jimbo la Creteil na Askofu wao kutoka Ufaransa wamekutana na Papa Francisko Vatican Mapadre wa Jimbo la Creteil na Askofu wao kutoka Ufaransa wamekutana na Papa Francisko Vatican 

Papa kwa mapadre wa Créteil:nyenyekea kwa uaminifu katika huduma

Baba Mtakatifu anawalekeza mapadre wa Jimbo la Créteil kutoka Ufaransa namna ya kuendelea kuitikia wito wa Bwana: “Hatukuwekwa wakfu kwa njia ya zawadi ya Roho Mtakatatifu ili kuwa mashujaa wakuu tu”. “Tumetumwa kwa utambuzi wa kuwa sisi ni watu tulio samehewa, ili kuwa wachungaji kwa mfano wa Yesu Kristo, aliyejeruhiwa, akafa na kufufuka

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Msisahau unyenyekevu mwaminifu wa kila siku katika huduma ambayo Bwana anawawezesha kuishi kwa ukuu, kwa wale ambao ametwatoa katika Kanisa kama makuhani”. Ndiyo wito wa Papa Francisko alioutoa kwa mapadre wa Jimbo la Créteil, nchini Ufaransa, aliokutana nao katika ukumbi wa mikutano wa Clementina mjini Vatican, tarehe 1 Okotba 2018, ambapo katika mantiki hiyo, Papa amekumbusha kuwa mtumbwi wa Kanisa umekumbwa na upepo mkali na wenye nguvu sababu ya makosa makubwa yaliyotokana na watu wake”

Shuhuda wa nguvu ya Ufufuko: Baba Mtakatifu anawalekeza mapadre wa Jimbo la Créteil (Ufaransa) namna ya kuendelea kuitikia wito wa Bwana ya kuwa: “Hatukuwekwa wakfu kwa njia ya zawadi ya Roho Mtakatatifu ili kuwa mashujaa wakuu tu”. “Tumetumwa kwa utambuzi wa kuwa sisi ni watu tulio samehewa, ili kuwa wachungaji kwa mfano wa Yesu Kristo, aliyejeruhiwa, akafa na kufufuka. Kwa sababu ya utume wetu kwa jinsi ulivyo, huduma ya Kanisa leo hii, kama jinsi ilivyokuwa hata jana, ni kushuhudia kwa nguvu ya Ufufuko katika majeraha ya ulimwengu huu. Kwa njia hiyo walitiwa wakfu, wanaweza kuwasaidia wafuasi wa Yesu Kristo, kujibu wito wao wa utabatizo.

Kutazama majeraha ya Kanisa: Baba Mtakatifu Francisko pia amewaalika mapadre tena waliosindikizwa na Askofu Michel Santier, akiwaomba kutafakari na kufanya upyaisho wa mabadiliko ya jimbo lao:“Msiwe na hofu ya kutazama majeraha ya Kanisa letu, siyo kulilalamikia, bali kwenda mbele hadi mwisho na Yesu Kristo. Yeye anaweza kuliponya na kuliwezesha kuanza na Yeye na kupata zana za dhati ambazo zinapendekeza maisha yake Yesu kwa wote na katika mantiki ya umasikini na katika ukosefu wa miito.

Kuwa mfano kwa ajili ya wito wa kikuhani: Hata vyo pia Papa Francisko ameelezea mapadre kwamba, ni katika njia ya namna ya kuishi huduma ya kikuhani ambayo inawawezesha vijana kupokea wito wa Bwana katika ukuhani au maisha ya kitawa: “kwa maana hiyo ninawatia moyo ili mwendelee na mtazamo juu ya Yesu Kristo na kukuza mahusiano kwa namna kuungana naye kwa njia ya sala binafsi, kusikiliza Neno lake, kuadhimisha Sakrameni na huduma kwa ndugu”.

Maisha ya wakfu ni kisima cha furaha: Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amewaalika makuhani wa Jimbo hilo kuchota katika kisima cha neema ambayo ni wito wa nguvu ya Roho Mtakatifu, ili kuweza kuwa mashuhuda wa matumaini ambayo hayakatishi tamaa: “ Licha ya matatizo na ugumu wa kila siku: “onesheni, kwa njia ya maisha yenu ya kila siku , juhudi  ya kufikia uzoefu wa udhaifu wenu, kwamba zawadi ya maisha katika kuhudumia Injili na ndugu zake, ni kisima cha furaha ambayo hakuna yoyote anaweza kuiondoa!

01 October 2018, 15:55