Cerca

Vatican News
Mkutano wa Papa Francisko na mahujaji wa Kanisa la Kigiriki Katoliki kutoka Slovikia Mkutano wa Papa Francisko na mahujaji wa Kanisa la Kigiriki Katoliki kutoka Slovakia  (Vatican Media)

Papa kwa Kanisa la Kigiriki Katoliki - Slovakia:Iga mfano wa wafiadini

Baba Mtakatifu amekutana mjini Vatican na mahujaji wa Kanisa la Kigiriki Katoliki kutoka Slovakia, na kuwahimiza kuiga mfano bora wa watakatifu wafiadini. Kanisa hilo, linaweza kufikiriwa katika kielelezo cha uzuri wa mitindo mbalimbali ya maisha ya Kanisa, ya wingi ambao si kutoa dosari katika umoja wa Kanisa, bali kuuonesha

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mtakatifu Yohane Paulo II akizungumza huko Prešov mwaka 1995 alitumia sura nzuri ya asili  ili kuelezea utambulisho na utume  wa jumuiya ya Kigiriki Katoliki: Katika maji mang’avu, yanaonesha mlima mzuri sana wa juu; uwanda huo (…)unazungumza uzuri na wema wa Muumba. Katika nchi za  Mashariki ya mlima wa Tatra hadi mtelemko wa Zempli, kwa karne nyingi wanaishi kwa kushikamana ndugu kaka na dada wa liturujia ya jumuiya ya masharikina ambao wanaalikiwa kuwakilisha kama maziwa madogo ambayo yanaonesha na kung’aa kwa ukarimu wa Mungu. Ni Bwana mwenyewe anaye tajirisha na Kanisa lake kwa mitindo mbalimbali za utamaduni”.( Hotuba kwa wakatoliki wa liturujia ya kibizantini, tarehe 2 Julai 1995,6).

Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyo anza nayo wakati wa kukutana na mjini Vatican na mahujaji wa Kanisa la Kigiriki Katoliki kutoka nchini Slovakia, tarehe 6 Oktoba 2018, wakiwa katika hija yao ya kuandhimisha miaka 200 tangu kuanza kwa upatriaki wao. Akiendelea na hotuba yake amsema: “ Kanisa la Kigiriki Katoliki nchini Slovakia, linaweza kufikiriwa katika kielelezo cha uzuri wa mitindo mbalimbali ya maisha ya Kanisa, ya wingi ambao si kutoa dosari katika umoja wa Kanisa, bali kuuonesha” (CONC. ECUM. VAT. II, Decr. Orientalium Ecclesiarum, 2).

 “Leo hii mpo hapa na Papa kuadhimisha miaka 200 tangu kuanzisha kwa Upatriaki wa Prešov, ulizaliwa kutokana na Mama wa Upatriaki wa Mukačevo, ambao kwa sasa ni sehemu ya nchi ya Ukraine.  Upatriaki wao umeendelea na kuwa kwa namna nyingine mama wa familia moja ya Kanisa na kutoa upatriaki mwingine, mojawapo ukiwa nchini Canada na ambao  kwa miaka kumi iliyopita umekuwa na Makao makuu kisheria”.

Kulinda familia

Hata hivyo Baba Mtakatifu katika fursa hiyo ameitumia kumsalimia kiongozi wao mkuu Ján Babjak  ambaye amesikia aeti anakwenda mstuni kuokota uyoga na maaskofu wenzake Chautur wa Košice, Askofu Rusnák wa  Bratislava na askofu mpya nchini Canada Pacák. Amewaomba wandelee na shughuli yao ya kuongoza na kuwa  mababa wa watu wa Mungu ambao wamekabidhiwa. Wafuate mwanga wa mfano wa wenyeheri Maaskofu  wafiadini Peter Pavol Gojdič na Vasiľ Hopko. Waeneze wema, amani, ukarimu, upole unyenyekevu wa kina na urahisi, katika kubaki daima wachungaji kwa mujibu wa Moyo wa Mungu ambaye ni Baba , kufuata nyayo za Kristo ambaye  hakuja kwa ajili ya kuhudumiwa bali kuhudumia.

Baba Mtakatifu akisisitiza zaidi, amesema kuwa, kwa mtiindo huo, anao uhakika kuwa mapadre , ambao ndiyo wahudumu wao wa kwanza, watafuata daima kwa furaha na na shauku, uwezekano wa kuhudumia Kanisa ambalo kwao wameombwa. Na kwa mapadre amewasalimia kwa moyo wa dhati na uhai kindugu, watu walei waliowekwa wakfu  na walei na familia zao pia watawa wote. Anawashukuru kwa kazi yao katikati ya watu waamini wa Mungu. Baba Mtakatifu amaesema kuwa, familia za mapadre wanahishi utumeakwa namna ya pekee kwa siku za sasa, mahali ambapo mawazo ya familia yamewekwa katika hoja , kwa maana hiyo anawaomba waendelee kutoa ushuhuda wa maisha masafi na ya kuigwa mfano

Hepukeni mambo ya kiulimwengu na ukuhani ulio tasa

Mapadre, wanaweza kuchota mifano hai iliyopo katika historia ya Kanisa lao wakati wa miaka 10 ya ku teswa katika nusu karne iliyo pita wakati wa kuchukuliwa na kukosa kila aina ya mambo muhimu ya kuishi.Hata hivyo amesema, anao utambuzi ya kwanza Askofu Babjak amekusanya na kutangaza historia nyingi. Leo hii na ndiyo  sasa katika kizazi ambacho kinaonesha uminifu na labda siyo mbele ya kufuatiliwa moja kwa moja na kwa nguvu, lakini uwepo wa matatizo na hatari nyinginezo. Leo hii mapadre kama ilivyo waseminari, Baba Mtakatifu ameongeza, anawasalimia na ambao kwa namna moja wamejaribiwa na vishawisho tofauri. Kwanza vya kubobea katika malimwengu, ambao unawapeeleka katika maisha ya ulimwengu huu, au katika tabia nyingine ambazo kwa dhati sio za kiinjili na wala nafasi ya Kanisa; mitindo ambayo baadaye uweza kugeuka kuwa ya ukuhani ukuhani usio zaa matunda.

Sura zenye kuonesha imani kidete, utambulisho wa Kanisa na kugundua mizizi

Baba Mtakatifu akiwatazama mahujaji hao amesema: katika uwepo wao wa furaha pamoja na wachungaji wao, anaona sura zenye shauku na furaha kubwa ya Kanisa katika imani iliyo kidete, wakiwa na a utambuzi wa hadi na ari ya kuwa na utambulisho wa Kanisa: kwa namna hiyo wao ni wana wa ujiilishaji uliotendeka kwa ukamilifu wa Utume wa Vatican na watakatifu wasimamizi wa Ulaya, Mtakatifu Cirily na Methodius. Bara la Ulaya katika mashariki kama ilivyo  hata na magharibi linahitaji kugunduliwa mizizi yake na wito wake; na kutoka katika mizizi ya kikristo , haiwezekani isiote miti yanye msingi mkuu ambao unatoa matunda kimalilifu kulingana na hadhi ya binadamu na kila aina ya hali, na kila aina ya hatua za maisha.

Kuendelea kulinda utamaduni wa kibizantini

Anawatia moyo waendelee kulinda utamaduni za kibizantini na ambaoo anasema Papa kuwa, akiwa kijana alijifunza kuutambua na kuupenda. Wagundue na kuiishi kikamilifu kama Mtaguso wa Vatican II unavyofundisha: kuwa na umakini mkubwa wa mchakato wa uinjilishaji na katekesi ambayo kabla ya yote wachungaji,  walio mstari wa mbele ni wazazi na baba ambao kwa walio wengi wamejifunza sala za kwanza na maana ya ukristo katika maisha. Shukrani kwa baba na mama, babu na bibi, na walimu wote ambao walikuwapi kwa kazi yao ambayo ni muhimu kushuhudia.

Na kwa kumalizia hotuba yake, Baba Mtakatifu amewaomba wawe na kumbukumbu maalum , hasa watakapoadhimisha misa Takatifu ya Liturujia katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu, hekalu lenye thamani kwa ajili ya kumbukumbu ya watakatifu Cirily na Methodius na kwa ajili ya historia yao . Na Mama Mtakatifu wa Mungu ambaye tunamtazama kwa matumaini na upendo wa wanae, kwa maombezi yake, alinde Kanisa katika kipindi hiki cha majaribu na  Sinodi kuhusu vijana ambayo imeanza hivi karibuni. Amewashukuru na kuwabariki wote jumuiya nzima ya Kikigiri Katoliki nchini Slovakia.

06 October 2018, 14:28