Katekesi ya Papa Francisko amesititzia Amri ya tano ya Mungu Katekesi ya Papa Francisko amesititzia Amri ya tano ya Mungu 

Papa katika Katekesi:ubaya wote wa dunia hii unatokana na fedha!

Katika Katekesi ya Papa Jumatano 10 Oktoba 2018, Papa ametafakari juu ya amri ya Tano ya Mungu isemayo: " Usiue". Amehimiza kuwa, tunapaswa kuwambia watu wote, wanawake, vijana duniani wasidharau maisha:“Hacheni tabia ya kukataa kazi ya Muumba! maana "Wewe ni kazi nzuri ya Mungu, usijishushe"

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Ndugu Kaka na dada habari za asubuhi! Katekesi ya leo inajikita katika Amri ya tano isemayo usiue. Ni amri ambayo inakataza usiue. Hapa tuko katika sehemu ya pili ya Amri Kumi za Mungu, sehemu ambayo inahusu uhusiano wa jirani; na amri hiyo kwa dhati katika tabia yake, inaonesha kama nguvu ya ulinzi wa thamani msingi katika mahusiano ya kibinadamu. Je ni thamani gani msingi katika mahusiano ya ubinadamu? Ni thamani ya maisha. Kwa maana hiyo usiue!

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 10 Oktoba 2018, kwa waamini na mahujaji wote waliofika kutoka pande zote za dunia, kuungana naye katika tafakari hii. Katekesi ambayo ni mwendelezo wa ufafanuzi wa “Amri kuu za Mungu”.  Baba Mtakatifu Francisko, ametoa tafakari hiyo kwa kuongozwa na somo kutoka katika Kitabu cha, (Hk 11, 24-26):“Wewe wapenda vitu vyote vilivyopo wala huchukii chochote ulichokiumba. Hungaliumba chochote kile kama ungekuwa unakichukia…. Chawezaje chochote kudumu ila kwa kupenda kwako? Chawezaje kuendelea kuwako kama hungalikiumba? Umeruhusu vitu vyote viwepo ee Bwana, kwa maana ni vyako, nawe wapenda vitu vyote hai”.

Ubaya wa dunia hii unakusanywa katika kudharau maisha

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi wa amri ya Tano ya Mungu anathibitisha: “inawezekana kusemakwamba, ubaya wote unaotendeka katika dunia, hii unakusanywa katika hili: “kudharua maisha”. Ni katika maisha yaliyoshambuliwa na vita, mashirika ya kunyonya watu, kama tunavyosoma katika magazeti au kusikiliza katika luninga na kuona mambo mengi; waviziaji na waharibifu wa kazi ya uumbaji; katika utamaduni wa ubaguzi na mifumo yote ambayo inakandamiza maisha ya binadamu, kuhesabu fursa, wakati huo huo idadi za kashfa ya watu wanaishia kuishi  katika  hali isiyo stahili ya mtu. Hiyo ndiyo hali ya kudharau maisha, na ndiyo maana ya kuua kwa namna hiyo, Baba Mtakatifu amebainisha!

Kuua maisha ambayo bado hayajazaliwa

Kuna njia nyingine ambazo pia ni kinyume, zinazo ruhusu hata kuharibu maisha ya binadamu katika umbu la mama kwa kutumia jina la kile kiitwacho “kulinda haki nyingine”. Lakini ni jinsi gani hiyo inawezakana kuwa tiba, raia, au kwa urahisi binadamu katika tendo la kuharibu maisha yasiyo na hatia na chipukizi hicho kikubwa?  Baba Mtakatifu anauliza: hiyo ni hali ya kuharibifu wa maisha ya binadamu eti kwa sababu ni suluhisho la matatizo? Je ninyi mnafikiri nini? Ni haki?... (watu wamemjibu hapana… Ni haki au hapana? (wamejibu hapana”) Ni haki kutafuta mahali pa kukodisha dimbwi ili  kutatua tatizo? (wamejibu: hapana!) Haiwezekani, na siyo haki kuharibu maisha ya binadamu, awe mdogo eti kwa ajili ya kutatua tatatizo. Ni kama kukodisha dimbwi la takataka ili kutatua tatizo.

Vurugu na kukataa maisha unatokana na hofu

Lakini hayo yote yanatokana na nini? Baba Mtakatifu ameuliza, yaani vurugu na kukataa maisha kichini chini yanatokana na nini?  Hayo yanatokana na hofu. Kumkaribisha mwengine kwa dhati, anaongeza, ni changamto binafsi. Tufikirie kwa mfano, anapogunduliwa kuwa, aliyebeba mimba ni mlemavu. Katika kesi ngumu hiyo, wazazi wanahitaji ki ukweli kuwa karibu sana, mshikamano wa kweli na ili kukabiliana na hali halisi katika kushinda hofu.  Lakini Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, “mara nyingi na kwa haraka ya ushauri, ni ule wa kutoa mimba, ikiwa na maana ya kuua mtu moja kwa moja.  Mfano mwingine Baba Mtakatifu ameutoa ni: “Mtoto mgonjwa, ni kama kila yeyote mwenye kuhitaji msaada katika ardhi hii, kama mzee mwenye kuhitaji msaada, kama maskini ambao wanajitahidi kwenda mbele”. “Na kila mmoja anayewakilisha kama matatizo, kwa dhati ni zawadi ya Mungu ambayo hawezekani kuondolewa kwa sababu ya ubinafsi, na kumzuia asikue katika upendo”. Maisha yaliyo athirika yanatuonesha njia ya kuondokana nayo, kwa njia ya kujiokoa katika maisha yaliyo jifungia katika ubinafsi na kugundua furaha ya upendo. Kutokana na kipengele hicho Baba Mtakatifu ametaka kusisitiza zaidi hasa kwa kuwashukuru watu wengi wa kujitolea kwa namna ya pekee amesema, “kwa nguvu ya watu wa kujitolea wa Italia ambao ni wenye nguvu zaidi kuliko aliyo wahi kukutana nao”. Shukrani nyingi zimewaendea!

Fedha, madaraka na sifa ni miungu inayosababisha kukataa maisha

Ni kitu gani kinamfanya binadamu akatae maisha? Ni miungu ya dunia hii, ambayo Baba Mtakatifu ameitaja kuwa ni fedha kwa sababu, wanasema kuwa: “ni vema kutoa mimba hiyo katikati, kwa maana itagharimu; pia miungu mingine ni madaraka na sifa. Hivyo ndivyo vizingiti vyenye makosa vya kuthamini maisha. Lakini kipimo kimojawapo cha kizamani katika maisha ni kipi? Ni upendo; upendo ambao Mungu anampenda mtu! Upendo ambao Mungu anapenda maisha, ndicho kipimo. Ni upendo ambao Mungu anapenda maisha ya binadamu. Kadhalika Papa anauliza je, “kwa dhati ni nini maana uchanya wa Neno la Mungu, “Usiue?  Hiyo ina maana ya kwamba: “Mungu ni mpenda maisha”, kama jinsi ilivyosomwa katika Somo la Biblia”, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Siri ya maisha inaionekana katika Mwana wa Mungu

Siri ya maisha imeoneshwa kwetu kama vile walivyo mfanya Mwana wa Mungu ambaye alijifanya mtu hadi kubeba msalaba kwa ajili yetu. Kutaliwa, udhaifu, umaskini na uchungu (Yh 13,1). Kila mtoto aliye mgonjwa, kila mzee mdhaifu, kila mhamiaji katika mahangaiko, kila maisha madhaifu na hatarishi, Kristo yupo anatutafuta (Mt 25,34-46) anatafuta mioyo yetu, ili kuweka ndani yake furaha ya upendo. Ni vema kupokea kila aina ya maisha kwa sababu kila binadamu anathamani ya damu ya Kristo mwenyewe (1 Pt 1,18-19). Haiwezekani kudharau kile ambacho Mungu alikipenda sana!

Tunapaswa kuwambia watu wote na wanawake duniani kwamba, msidharau maisha! Maisha yoyote mengine, lakini pia hata binafsi, kwani hata hayo yanastahiki amri hiyo ya “Usiue”. Vijana wengi wanapaswa kuwambiwa kwa “Msidharau maisha! Hacheni tabia ya kukataa kazi ya Muumbaji! Wewe ni kazi nzuri ya Mungu! Usijipunguze, na usidharau kutokana na kasumba ambazo zitakuharibu na kukufikisha katika kifo!

Hakuna yeyote anayepima maisha kwa mujibu wa ulaghai wa dunia hii, bali kila mmoja ajipokee mwenyewe na kuwapokea wengine kwa jina Baba aliyetuumba. Yeye ni mpenda maisha”. Ni vema hiyo kwani Mungu ni mpenda maisha. Na tusema kwa wote…,“Mungu ni mpenda maisha”  wote kwa pamoja Papa amasema…. (wamerudia) Rudieni kwa nguvu zote: (“Mungu ni mpenda maisha”). Kwa mara nyingine tena: (Wamerudia) Asanteni. Na sisi sote ni wapendwa ambao alimtumwa Mwanae kwa ajili yetu. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

10 October 2018, 16:07