Tafuta

Papa: ai passionisti;affrontate nuove sfide migrazioni e Papa: ai passionisti;affrontate nuove sfide migrazioni e  

Papa:Kanisa linahitaji wahudumu wa upendo na kusikiliza!

Papa Francisko amewambia Mapadre wa Shirika la Mateso kuwa, Kanisa leo hii linahisi kwa nguvu ule wito wa kutoka nje binafsi, kwenda pembezoni na kukumbatia mipaka mipya katika utume wao na ili kukabiliana na changamoto za nyakati zetu, kama vile wahamiaji na ulimwengu wa digital

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ninayo furaha ya kukutana nanyi katika fursa ya Mkutano wenu Mkuu, ninamshukuru Mkuu wa Shirika kwa maneno yake. Katika siku hizi kwa tafakari lenu mmengozwa na mada ya, “Kupyaisha utume wetu: kwa shukrani, Unabii na matumaini”. Maneno haya matatu: shukrani, unabii na matumaini yanajieleza tasaufi ambayo mnapenda itiwe chachu katika Shirika lenu kwa upyaisho wa kimisionari. Kwa hakika ili kuweza kuongoza Shirika, ninyi mnapendekeza kujikita katika safari mpya ya mafunzo ya kudumu katika jumuiya zenu, zinazo chimba mzizi katika uzoefu wa maisha ya kila siku: na zaidi mnapendelea kujikita katika mang’amuzi ya mitindo ya kichungaji hasa kwa umakini wa kizazi cha vijana.

Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi tarehe 22 Oktoba 2018 alipokutana na wanashirika wa Mapadre wa Mateso ambao wako  katika Mkutano wao Mkuu. Akiendelea na hotuba yake, amesema, “ Mwanzilishi wao Mtakatifu Paulo wa Msalaba alianzaisha suala hili akiwa na wenzake kwa kutoa moto wao wa, Mateso makuu ya Yesu Kriasto yawe daima katika mioyo yetu”.Katika maandiko yake ya kwanza, Mtakatifu Vincenzo Maria Strambi, aliandika kuw, “Utafikiri Mungu Mwenyezi alichagua Padre Paulo kwa namna ya pekee, ili kufundisha namna ya kutafuta Mungu kwa kina ndani ya moyo; Mtakatifu Paulo wa Msalaba alikuwa anataka jumuiya zao ziwe shule ya sala, mahali ambapo unaweza kufanya uzoefu wa Mungu. Utakatifu wake aliuishi kati ya kiza nene na upekwe, lakini hata na furaha na amani  ambayo iliweza kugusa moyo kwa yule aliye bahatika kukutana naye.

Kanisa linahitaji wahudumu wa upendo, kusikiliza bila kuhukumu na kupokea kwa huruma: Baba Mtakatifu Francisko anasema: “Katika kitovu cha maisha yao na utume wao kuna mateso ya Yesu ambayo Mwanzilisha alikuwa akiyaelezea“ kama yaliyo makubwa na ya kushangaza katika kazi ya upendo wa Mungu (Barua II, 499). Nadhiri zinazowafungamanisha, na ambazo zinawawajibisha, nakuendelea kuwafanya wawe  hai katika kumbukumbu ya mateso na kuwaweka katika miguu ya msalab, mahali ambapo unatoka upendo wa kuponesha na mapatano ya Mungu. Baba Mtakatifu Francisko, anawatia moyo wawe wahudumu wa uponyaji wa kiroho na mapatano, ambayo yanahitajika katika dunia ya sasa, ambayo imegubishwa na yale ya zamani na majeraha mapya.

Aidha amefafanua kuwa: Katiba yao inawaalika kujikita  na kujitoa wao binafsi katika kuinjilisha watu kwa upya, hasa kupendelea zaidi sehemu ya maskini na sehemu zilizo pembezoni mwa jamii (cost,70).  Ukaribu wao kwa watu, unajieleza kiutamaduni kwa njia ya utume mahalia, kusindikiza watu kiroho na sakramenti ya kitubio na  ndiyo ushuhuda msingi. Kanisa linahitaji wahudumu ambao wanazungumza kwa upendo, wanasikiliza bila kuhukumu na kuwapokea kwa huruma.

Kanisa leo hii linahisi kwa nguvu ule wito wa kutoka nje binafsi, kwenda katika pembezoni, iwe kijiografia katika maisha ya watu. Na kati yao wakumbatie mipaka mipya katika utume wao ambao sio tu kwenda katika maeneo kwa ajili ya kupeleka Injili bali kwenda kukabiliana na changamoto za wakati wetu, kama vile wahamiaji, wabobea ulimwangu na ulimwengu wa digital. Hiyo yote ina maana ya kuwepo katika hali halisi mahali ambapo watu wanahisi ukosefu wa Mungu ,na kutafuta kuwa karibu nao ambao kwa namna nyingine na katika hali nyingine wanateseka.

Katika nyakati hizi ya mabadiliko, na ambazo zaidi ni mabadiliko ya nyakati, wao wanaitwa kuwa makini katika uwepo na matendo ya Roho Mtakatifu, wakisoma ishara za nyakati. Hali mpya zinahitaji majibu mapya. Mtakatifu Paulo wa Msalaba alikuwa ni mbunifu sana katika kujibu mahitaji ya wakati wake na kutambua, kama inavyosema Kanuni ya shirika:“ upendo wa Mungu ni mwepesi sana na aujioneshi kwa maneno mengi sana, bali katika matendo na mifano ya yule anayependa” (XVI). Uaminifu wa kibunifu katika karama yao, itawasaidia kujibu mahitaji ya watu wa leo hii na kuweza kubaki karibu na Kristo mteswa na ili kuweza kupeleka uwepo wake katika dunia inayoteseka.

Mifano mingi watu watakatifu wa Mungu wa shirika la Mapadre wa Mateso: Shirika lao, Baba Mtakatifu ameongeza, limetoa mifano mingi ya utakatifu wa watu wa Mungu: kwa kufikiria Mtakatifu Gabriel wa Mateso, kijana ambaye alikuwa na furaha ya kumfuasa Kristo na ambaye hata leo hii anazungmzwa na vijana wa leo. Ushuhuda wa Watakatifu na wenye heri wa  Familia ya watawa wa kike, pia inaonesha matunda ya karama na kuwakilisha mtindo wa kuigwa katika uchaguzi wa kitume.  Nguvu na urahisi wa ujumbe wao ambao ndiyo upendo wa Mungu, ulio jionesha juu ya msalaba, unaweza tena kuzungumza leo hii katika jamii ambayo inajifunza kuwa siyo kuamini maneno tu, bali kuamini kwa matendo hai. Vijana wengi wanaotafuta  Mungu, upendo mkuu wa Yesu wanaweza kupata kisima cha matumani na ujasiri , kwa kuwafundisha wao kwamba kila mmoja amependwa binafsi  hadi mwisho. Ushuhuda wao na utume wao, unaweza kuendelea kutajirisha Kanisa, na waweza kubaki karibu sana na Kristo msulibiwa na watu wake wanao teseka. Amehitimisha kwa kuwabariki wote, lakii bila kusahau kuomba sala kwa ajili yake.

 

 

22 October 2018, 16:10