Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amehimiza kwa mara nyingine tena kusali Rosari Takatifu Papa Francisko amehimiza kwa mara nyingine tena kusali Rosari Takatifu 

Papa:Jumamosi itakuwa ni Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Macatacomb

Tarehe 7 Oktoba ya kila mwaka Kanisa linakumbuka Mama Maria wa Rosari. Papa anakumbusha kuhitimisaha Rosari na sala ya “Tunaukimbilia ulinzi wako, na Jumamosi ni Siku ya kwanza ya maadhimisho ya Macatacomb”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo ni Sikukuu ya Mama Maria wa Rosari, ninatoa salam maalum kwa waamini waliounganika katika madhabahu ya Pompei kama Utadamuni kwa ajili ya sala inayoongozwa katika fursa hii na Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria. Kwa mara nyingine ninawaomba kusali Rosari kila siku katika mwezi wa Oktoba, kwa kuhitimisha na sala ya “Tunaukimbilia ulinzi wako" na sala ya Mtakatifu Malaika Mikaeli ili aweze kuzuia mashambulizi ya shetani anayetaka kugawanya Kanisa.

Kadhalika Baba Mtakatifu amesema kuwa: " Jumamosi ijayo mjini Roma itakuwa ni kwa mara ya kwanza kuadhimisha Siku ya  mapango ya wakristo( macatacomb). Maeneo mengi hayo ya kumbukumbu ya wakristo walioteswa yatafunguliwa kwa watu  wote na kutakuwepo na  wahudumu wa mafunzo na matukio ya utamaduni. Baba Mtakatifu ameongeza kusema, “Ninashukuru Tume ya Kipapa  ya Kamishna ya Sanaa Takatifu kwa kuanzisha shughuli hii na ninawatakia matashi mema na ufanisi.

Amewasalimia makundi yote kutoka Roma, mahujaji hasa familia na makundi mengi ya kutoka parokia mbalimbali  nchini Italia na duniani kote. Salam kwa mahujaji kutoka Kanisa ka Kigiriki katoliki kutoka nchini Slovakia, waamini wa Pozna (Poland) na Fortaleza Brazil; mabibi kutoka Kisiwa cha Malta, na wanafunzi wa Neuilly (Ufaransa): watawa wa Mtakatifu Paolo wa Cahartres kutoka Australia. Kwa wote amewatakia Dominka njema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

Ikumbukwe kwa ufupi historia na lengo la kuanzishwa kwa Macatacomb: Pamoja na changamoto iliyotolewa na Mwenyeheri Paulo VI kunako mwaka 1965 alipokazia umuhimu wa Macatacomb katika maisha na utume wa Kanisa alikaza kusema, hapa Kanisa lilivuliwa nguvu za kibinadamu, Kanisa likawa maskini na nyenyekevu; Kanisa lilikumbata na kumcha Mungu; hapa Kanisa lilidhulumiwa na kuibuka kuwa shujaa!

Wakati wa Jubilei ya miaka 50 tangu Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walipoweka sahihi Mktaba wa Macatacomb, watawa wa Mashirika mbali mbali walishiriki kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na Njia ya Msalaba. Kulikuwepo hata semina pamoja makongamano mbali mbali, ili kufafanua umuhimu wa Kanisa kuwa fukara kwa ajili ya kuwahudumia maskini wa hali na kipato.  Mkataba huu ni changamoto kubwa kwa Kanisa Barani Afrika ambalo kwa kiasi kikubwa linawahudumia maskini na watu wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Changamoto kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba, Kanisa linakuwa kati ya watu kwa ajili ya huduma makini kwa watu, ili hatimaye waweze kufika mbinguni kwenye maisha ya uzima wa milele. Ni dhamana kubwa ya Kanisa Barani Afrika kushughulikia haki, amani, upendo na maridhiano kati ya watu.

huo”. http://sw.radiovaticana.va/storico/2015/11/16/kanisa_linachangamotishwa_kuwa_fukara_ili_kuwahudumia_vyema_maskini!/sw-1187217 

08 October 2018, 09:17