Tafuta

Papa Francisko: Waamini msigope kumfungulia Kristo malango ya maisha yenu! Papa Francisko: Waamini msigope kumfungulia Kristo malango ya maisha yenu! 

Papa Francisko: Msiogope kumfungulia Kristo malango ya maisha yenu kwa uaminifu na huduma!

Papa Francisko katika kipindi hiki ambacho Kanisa linaendelea kufanya kumbu kumbu ya miaka 40 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipochaguliwa kuliongoza Kanisa, anawaalika tena waamini kumfungulia Kristo Malango ya maisha yao pasi na woga,

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 17 Oktoba 2018, Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi hiki ambacho Kanisa linaendelea kufanya kumbu kumbu ya miaka 40 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipochaguliwa kuliongoza Kanisa, anawaalika tena waamini kumfungulia Kristo Malango ya maisha yao pasi na woga, changamoto na mwaliko wa kuendelea kuwa waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake; kwa njia ya huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa la Kristo!

Baba Mtakatifu ametambua uwepo wa watawa wa Shirika la Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing, waliokuwa wanashiriki mkutano mkuu wa Shirika katka mkutano huu, Mheshimiwa Sr. Terese Zemale kutoka Ndanda aliwawakilisha Masista wa Tutzing kutoka Ndanda, Tanzania. Kulikuwepo pia washiriki wa Mkutano wa Radio Maria duniani na kwa upande wa Tanzania, ujumbe wa Radio Maria umeongoza na Padre John Maendeleo. Baba Mtakatifu ametambua pia uwepo wa mahujaji kutoka Ghana, Nigeria, Afrika ya Kusini, Uganda na Tanzania.

Baba Mtakatuifu amekumbusha kwamba, tarehe 17 Oktoba, Mama Kanisa ameadhimisha Kumbu kumbu ya Mtakatifu Inyasi wa Antokia, Shahidi na Askofu aliyemimina maisha yake hapa Roma kwa kutupwa kwenye tanuru na Simba, awe ni mfano bora wa ushuhuda na ujasiri katika imani. Kwa njia ya maombezi yake, Mwenyezi Mungu awakirimie waja wake nguvu ya kudumu katika imani na matumaini licha ya chuki, uhasama na madhulumu wanayoweza kukumbana nayo katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Papa: Mahujaji
17 October 2018, 13:55