Kipindi cha Ave Maria katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia Kipindi cha Ave Maria katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia 

Papa anatafakari mada ya hofu katika kipindi cha Ave Maria!

Ni kipindi ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kinacho husu sala ya “Ave Maria” kitanaendelea hata usiku wa tarehe 23 Oktoba kwa kuongozwa na Padre Marko Pozza, mtaalimungu na msimamizi wa Kanisa dogo la magereza ya Padova

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Usiku wa tarehe 23 Oktoba ni sehemu ya pili ya tafakari ya sala ya “Salam Maria ikiwa ni mwendelezo wa vipindi 11 vinavyotolea na Televisheni ya Baraza la Maaskofu wa Italia (TV2000). Ni kipindi ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, na anayeongoza kipindi hicho ni Padre Marko Pozza, mtaalimungu na msimamizi wa Kanisa dogo la magereza ya Padova.

Kipindi kinaanza na maelezo mafupi ya Baba Mtakatifu, na baadaye kufuatia mgeni anayekuwa amekaribishwa kwa siku, kwa maana hiyo katika kipindi cha tarehe 23 Oktoba Padre Pozza atahojiana na mwendesha kipindi katika Televisheni kwa anayeitwa Bi Michelle Hunziker na Vera Vigevani Jarach, mmoja wa wa mama wa Nyumba Mayo.

“Hofu mbele ya maamuzi msingi”, ndiyo mada ambayo Papa Francisko atasisitiza katika kipindi hiki kipya cha “Ave Maria” katika Televisheni ya maaskofu wa Italia, ambayo saa 3.05 usiku masaa ya Ulaya itaonesha. Hii ni kutaka kuonesha juu ya wito wa Mama Maria alioupokea, ambapo Papa Francisko anathibitisha kuwa yeye alikuwa peke yake na kwamba mwanzo aliogopa kidogo. Hakuwa anajua vizuri ni kitu gani anaambiwa. Na hakuwahi kufikiria jambo kama hili la kuitwa. Lakini baada ya kupewa maelezo alindelea mbele peke yake akiwa na Bwana.

Wanaume na wanawake leo hii: Hata hivyo papa anapanua mawazo zaidi ya maisha ya wanaume na wanawake leo hii kwamba maamuzi ambayo wanachukua, lazima yapate ushauri,na uthibitisho, lakini mwisho wa kufanya hatua mbele ni wewe peke yako na Bwana. Papa Francisko ametoa mifano ya kesi nyingi kama vile kijana anayehisi kuitwa kwa namna ya pekee ya kumfuasa Yesu kwa karibu katika maisha ya kitawa, kikuhani; hata kufikia ndoa.

Hofu iliyofungwa: Katika kutazama kwa karibu juu ya hofu, Papa anathibitisha kuwa kuna aina mbli za hofu ya kwanza iliyo wazi na uliyofungwa. Hofu iliyofungwa ni ile ambayo inakufanya uwe mtumwa, wewe ni mtoto wa hofu, na hiyo ahitajikiwi kwani haikufanyi ukue na kukuacha uwe huru katika makuzi. Hofu iliyofunguliwa ni ile takatifu ya Mungu. Hofu ya mungu, vyote hivyo vinakupeleka mbele kwa uhakika. Hofu na uhakika vyote kwa pamoja.

Katika mahojiano ya mwendesha vipindi ya televisheni Bi Michelle Hunziker na hasa Bi Vera Vigevani Jarach, mmoja wa mama katika nyumba ya  Mayo, Papa Francisko anasema ni mama aliyeteseka sana na janga la kutisha kwani ni mama ambaye aliondolewa mtoto wake na kutupwa; ni uzoefu mbaya sana. Mara nyingi papa anaongeza kusema, wengi wanauliza, hivi Kanisa liko wapi wakati ule ambao hawakuweza kulinda. Katika swali hilo, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa ni kukaa kimya na kuwasindikiza. Mahangaiko ya mama wa Nyumba ya Mayo siyo ya kueleza, ni kukaa kimya na kusindikiza, kuheshimu uchungu na kumshika mkono.

23 October 2018, 13:51