Cerca

Vatican News
Papa anahimiza kusali Rosari mwezi Oktoba Papa anahimiza kusali Rosari mwezi Oktoba  

Nia ya maombi ya Papa Francisko kwa mwezi Oktoba 2018

Kama ilivyo kawaida ya kila mwezi, Baba Mtakatifu Francisko katika mwezi wa Oktoba ametoa nia ya sala kwa njia ya video kusali Rosari na kuhitimisha sala hiyo kwa kusali tunaukimbilia ulinzi wako na sala ya Malaika Mkuu Mikaeli

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

"Shetani  anajiwakilisha mwenye nguvu sana anakuletea zawadi, lakini wewe hujui kilichopo ndani yake". Kwa maana hiyo ninapyaisha wito kwa  wote kusali Rosari kila siku katika mwezi wa Oktoba na  kuhitimisha na salaya "Tunaukimbilia ulinzi wako na kufuatia sala ya  Malaika Mkuu Mikaeli ili aweze kufukuza mbali mashabulizi ya shetani anayetaka kugawa Kanisa".  Huo ndiyo ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya Video, katika nia ya maombi kwa mwezi wa Oktoba, ambapo imekuwa sasa kawaida ya kutoa nia ya kila mwezi kwa njia ya video. 

Ikumbukwe tarehe 29 Septemba Baba Mtakatifu Francisko  aliamua kuwaalika waamini wota duniani kote kusali Rosari kila siku, wakati wa mwezi mzima wa Oktoba ambao ni wa Mama Maria. Na aliomba kuwa sala iunganishwa na umoja na kitubio kama watu wa Mungu, kwa kumwomba Mama Maria Mtakatifu Mama wa Mungu na Mtakatifu Malaika Mkuu kulinda Kanisa dhidi ya shetani ambaye daima anataka kututengenisha na Mungu na kati yetu.

Sala ya Tunaukimbilia na Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu 

Aliwaomba waamni wote kuhitimisha na sala ya: "Tunaukimbilia ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, tuokoe siku zote tuingiapo hatarini, Ee Bikira mtukufu mwenye baraka Amina

Kadhalika na sala ya: "Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina"

 

10 October 2018, 16:56