Tuombe ili tuweze kujitambua sisi binafsi na kumjua Yesu Tuombe ili tuweze kujitambua sisi binafsi na kumjua Yesu 

Kujitambua sisi wadhambi ndiyo hatua ya kwanza ya kumjua Yesu!

Kujitambua kuwa sisi ni wadhambi kwa dhati ni kutambua upendo wa Yesu Kristo, ili tusije kuwa wakristo wa maneno tu kama kasuku. Ndiyo wito wa Papa Francisko asubuhi katika tafakari ya Misa takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta, tarehe 25 Oktoba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Je ninaye Yesu? Baba Mtakatifu Francisko, ameuliza swali hilo katika mahubiri yake wakati wa Misa Takatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 25 Oktoba 2018. Katika mahubiri anasema, “iwapo mtu anakuuliza Yesu Kristo ni nani, sisi tunaweza kusema kile ambacho tumejifunza ya  kuwa ni Mwokozi wa dunia, ni Mwana wa Baba, na kile ambacho tunasali katika sala ya “Nasadiki”, lakini kwa kiasi ni ngumu”. Lakini katika kujibu swali hilo, Baba Mtakatifu anabinisha, “kujibu swali juu ya Yesu kwangu mimi ni nani, ni swali ambalo linatupatia shida kidogo, pia kuwa hata na aibu ya kujibu kwa maana ni lazima kutoa jibu hilo  ndani ya moyo, yaani kuanzia katika uzoefu”.

Kama Mtakatifu Paulo ni kuanzia katika uzoefu binafsi

Mtakatifu Paulo kwa hakika hatulii kabisa kuonesha kuwa, yeye alimtambua Yesu Kristo kwa njia ya uzoefu wake. Alipoanguka kutoka juu ya farasi wake, na Bwana alipoongea katika moyo wake. Hakumtambua Yesu wakati anaanza kusoma taalimungu, hata kama baadaye alikwenda kutazama ni nini kilikuwa kimeandikwa katika maandiko matakatifu yaliyokuwa yanamhusu Yesu. Kile ambacho Mtakatifu Paulo alisikia, ndicho hata sisi tunapaswa tusikilize. Na swali ambalo tunaweza kuuliza Paulo, ni ili, “je Kristo ni nani kwako? Na yeye bila shaka atajibu kupitia uzoefu wake rahisi kwamba: “Yeye alinipenda na akajikabidhi kwa ajili yangu”. Baba Mtakatifu ameongeza kusema, pamoja na hayo Paulo pia alijihusisha kabisa na Kristo na kulipa kwa ajili yake.  Uzoefu wa Paulo, ndiyo unataka hata sisi wakristo wote katika kesi hiyo kwa wakristo wa Efeso, waweze kuingia kwa dhati katika uzoefu hadi kufiki hatua ya kila mmoja aseme, “alinipenda na kujikabidhi kwangu”, lakini pia aonesha uzoefu binafsi hasa!

Katika Somo la Kwanza la Liturujia ya siku, kwa dhati linatoka katika Barua ya Paulo kwa Waefeso (Ef 3,14-21), mahali ambapo mtume anasema “Kristo akae mioyoni mwenu kwa Imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

Kuchaguliwa kwa upendo lakini wadhambi

Ili kufikia uzoefu wa Mtakatifu Paulo alio upata na Yesu, Papa Francisko anasisitiza kuwa, ukisali mara nyingi sala ya “Nasaidiki”, inasaidia, lakini njia bora zaidi inapitia kujitambua binafsi kwamba ni wadhambi na ndiyo hatua ya kwanza. Hiyo hasa, ni kutokana na Mtakatifu Paulo anayesema,Yesu alijikabidhi kwake,ikiwa na maana ya kwamba alilipa kwa ajili yake na anaelezea hayo katika barua zake. Ufafanuzi wa kwanza ambao anautoa yeye binafsi ni ule wa kuwa mwenye dhambi na kuthibitisha kwamba, alikuwa anawatesa wakristo na hivyo hakuchaguliwa kwa sababu ya upendo tu na kustahili, bali kwakuwa alikuwa mwenye dhambi. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza yakumtambua Kristo ili kuweza kuingia katika fumbo hilo. Baba Mtakatifu amethibitisha.

Kadhalika anasisisitiza zaidi kuwa, utambuzi wa dhambi binafsi ndiyo hatua ya kwanza na hivyo katika sakramenti ya kutubio, sisi tunasema dhambi zetu lakini jambo la kuzungumza dhambi ni jambo jingine lenye kuwa na utambuzi wa dhambi kwa asili yake na kuwa na uwezo wa kufanya kila uwezalo wa kutambua uchafu. Mtakatifu Paulo, alifanya uzoefu wa kweli binafsi wa udhaifu wa dhambi na ambao ulikuwa unahitaji kukombolewa na mtu ambaye alilipa haki na kumfanya awe mwana wa Mungu. Sisi sote ni wana, lakini tuseme, tuhisi maana kulikuwa na haja ya sadaka ya Kristo.  Ni vema kutambua kwa dhati dhambi zetu na kuona aibu sisi binafsi, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Kutambua Yesu na siyo wakristo wa maneno tu

Kuna hatua nyingine ya Pili ya kutambua Yesu, Papa amesema, hiyo ni ile ya kutafakari na kusali ili kumtambua Yesu. Ipo sala nzuri ya Mtakatifu mmoja isemayo, “Ili niweze kukutambua na kukujua wewe.  Kujitambua sisi wenyewe na kumtambua Yesu ndiyo jambo msingi. Na hiyo ni kutika kujikita kwenye uhusiano wa wokovu na ambayo inakutaka usiridhike kwa kusema  maneno matatu, au manne ya haki juu ya Yesu, badala yake kutambua Yesu ni kadhia ( adventure), lakini kadhia hiyo ni makini na siyo kadhia kama ya kijana mdogo kwa maana upendo wa Yesu hauna kikomo.  Baba Mtakatifu anabinisha kuwa, “Wakristo wenye maneno wapo wengi sana; hata sisi wenyewe mara nyingi tuko hivyo. Huo siyo utakatifu; Utakatifu ni kuwa wakristo wanao tenda katika maisha yao kile ambacho alifundisha Yesu, kile alichopanda Yesu katika mioyo”.

Hata Mtakatifu Paulo anasema mwenyewe: “Katika Yule mwenye kuwa na nguvu anaweza kufanya mengi ambayo sisi hatuna uwezo wa kuomba au kufikiria, anao uwezo wa kufanya yote”. Kutokana na hilo, ni lazima kuomba, Ee Bwana nifanye nikutambua; wakati nitakapozungumza juu yako, na nisizungumze maneno kama kasuku, bali maneno yatokanayo na uzoefu wang”. Na kama Paulo ninaweza kusema “alinipenda na kujikabidhi na ninakubali ukweli huo. Hiyo ndiyo nguvu yetu, huo ndiyo ushuhuda wetu. Papa anahimiza kusali kila siku ili kumtambua Bwana na sisi wenyewe!

Hitimisho la Papa ni hatua mbili za kumtambua Yesu Kristo

Papa amehitimisha mahubiri yake kwa kukazia kuwa : “Hatua ya kwanza ni kujitambua binafsi ya kuwa mdhambi au wadhambi.” “Bila kuwa na utambuzi huo na bila kuwa na maungamo hayo ya kina, ya kuwa mimi ni mdhambi, haiwezekani kwenda mbele”. Na hatua ya pili ni “ile ya sala kwa Bwana, ambaye kwa nguvu yake anaweza kutufanya tutambue fumbo la Yesu ambaye ndiye moto aliyotupa katika duniani”. “Itakuwa ni tabia nzuri ya  kila siku na wakati mwingine tunaweza kusema : Ee Bwana niweze kukutambua na mimi kujitambua. Na hivyo kuweza kwenda mbele”.

 

 

25 October 2018, 14:17