Kristo anaonesha upendo wa kweli, Yeye anayeishi upendo na Baba na  ndiyo nguvu hiyo ambapo ni rafiki mwaminifu Kristo anaonesha upendo wa kweli, Yeye anayeishi upendo na Baba na ndiyo nguvu hiyo ambapo ni rafiki mwaminifu  

Katekesi ya Papa:mapendo yanataka uwe halisi na mungano usiovunjika

Papa Francisko anaendelea na tafakari Amri Kumi za Mungu na Jumatano tarehe 24 Oktoba 2018 amefikia amri ya sita ya Mungu ambayo ni “Usizini”. Katika amari hiyo amahimiza kuwa na upendo wa kweli, hasa wanandoa wajiandae vema wakati wa uchumba maana siyo mchezo ni maisha ya dhati

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican News

Wapenda kaka na dada, habari za asubuhi! Katika hatua yetu ya katekesi juu ya Amri,  leo hii tumefikia Neno la Sita, linalotazama ukuu wa upendo na ngono, na neno hilo ni “usizini”. Huo ni mwaliko moja kwa moja wa uaminifu, kwani hakuna uhusiano wowote wa kibinadamu ni wa dhati bila kuwa na uaminifu na halisi. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 24 Oktoba 2018, kwa mahujaji na waamini wote kutoka pande zote za dunia ili kuunganika naye katika tafakari hii ya kila wiki, ambapo Papa Francisko anatafakari Amri Kumi za Mungu, na  amefikia amri ya sita ya Mungu ambayo ni “Usizini”.

Mapendo yanataka Baba Mtakatifu Francisko akendelea na ufafanuzi wa amri ya sita anasema: “Uwezi kupenda unavyoona namna nyingine; upendo unajidhihirisha zaidi ya kizingiti cha faida binafsi. Hiyo ni wakati unapojitoa kila kitu bila kubakiza. Kama Katekisimu Katoliki inavyothibitisha: “mapendo yanataka kuwa halisi; hayawezi kuwa na mpaka tukavyoona namna nyingine, maana, hutaka mungano usiovunjika,(1646). Uaminifu ndiyo tabia ya mahusiano, huru ya binadamu, aliye komaa na mwajibikaji. Hata rafiki anayejionesha wa dhati, kwa sababu anabaki jinsi alivyo, la sivyo hawezi kuwa rafiki. Kristo anaonesha upendo wa kweli, Yeye anayeishi upendo na Baba na  ndiyo nguvu hiyo ambapo ni rafiki mwaminifu anayetupokea hata tunapokosea, anataka wema wetu, hata kama hatusitahili.

Mwanadamu anahitaji kupendwa bila kuwekewa masharti

Tendo la kuwa bidamua linahitajo kupendwa bila masharti, na asiyepokea mapokezi hayo, upelekea ndani mwaka aina ya ukosefu wa ukamilifu na mara nyingi bila kutambua. Moyo wa mwanadamu hujaribu kujaza hili kwa utupu na maingiliano, akikubali ahadi unafiki ambao katika upendo una ladha tu isiyoeleweka. Hatari ni ni kuiita "upendo" wa mahusiano yasiyofaa ambayo ni mabichi na siyo komavu, pamoja na udanganyifu wa kupata mwanga wa maisha katika kitu ambacho, katika kesi nyingi hazina tija. Kwa namna hiyo mara nyingi  hutokea kwa mfano  wa kuvutiwa maumbo  ya mwili na ambayo kwayo ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini lengo lake  ni kuandaa njia ya uhusiano wa kweli na aminifu wa  mtu. Kama Mtakatifu Yohana Paulo II alivyo sema kuwa, mwanadamu,“ anaitwa katika uzima kamili na kukomaa kawaida kwa mahusiano”, ambayo “ kwa taratibu ni matunda yatokanayo na mang’amuzi ya ufahamu wa mwelekeo wa moyo wa mtu”. Ni kitu kinachopatikana hasa tangu kipindi ambacho, kila mwanadamu anatambu kuwa ni “lazima kwa uvumilivu na uthabiti wa kujifunza nini maana ya mwili”.(taz Catekiesi, 12 novemba 1980).

Wito wa  maisha ya wanandoa

Wito wa maisha ya ndoa unahitaji, kwa njia hiyo ufahamu makini juu ya ubora wa uhusiano na muda wa ushiriki katika uchumba ili kuthibitisha. Katika kuweza kupokea sakramenti ya ndoa, wachumba  wanaohusika wanapaswa kukomaa  uhakika kwamba katika dhamana yao kuna mkono wa Mungu, ambaye huwatangulia na atawawezesha wao kusema “Kwa neema ya Kristo ninaahidi  kuwa mwaminifu daima  kwako”. Hawawezi kuahidi uaminifu "kwa furaha na uchungu, katika afya na katika ugonjwa" na kupenda na kuheshimiana kila siku ya maisha yao, kwa misingi tu ya mapenzi mema au matumaini ambayo kwamba, jambo hilo litendeke”. Kwa maana hiyo Papa anathibitisha kuwa wao,“ Wanahitaji kujenga juu ya ardhi imara ya upendo mwaminifu wa  Mungu”.

Maandalizi ya ndoa hayawezi kuishia kwa kufanya mikutano mitatu au minne tu

Akifafanua zaidi juu ya maisha ya ndoa anasema: hii ndiyo maana kabla ya kupokea Sakramenti ya Ndoa, inahitahiji maandalizi ya dhati, na kuongeza kusema,  labda aseme, ukatekumeni  kwa sababu hapa ni suala linalohusu upendo wa maisha yote na katika upendo hakuna mchezo. Haiwezekani kujieleza mikutano mitatu au minne ya maandalizi ya ndoa  yanayotolewa parokiani; Hapana, hayo sio maandalizi, Papa anathibitisha na kuongeza: “haya ni maandalizi bandia”. Na wajibu wa yule anaye fanya hivyo,  inahangukia juu yake: juu ya paroko  wa parokia, kwa askofu anayeruhusu mambo hayo. Maandalizi yanapaswa yaliyokomaa pia yanachukua muda. Siyo tendo la kijujuu, ni sakramenti. Lakini pia ni lazima kutayatarisha na ukatekumeni wa kweli.

Kuna wazinzi wengi ambapo Neno la Sita linaweza kutuokoa

Baba Mtakatifu akiendelea  juu ya amri ya usizini anasema kuna wazinzi wengi ambapoi neno la sita lnaweza kutuokoa. Kwa hakika uaminifu ni njia ya kuwa, ni mtindo wa maisha. Ni kufanya kazi kwa hakika, kuzungumza kiukweli, ni kubaki katika ukweli katika mawazo na matendo. Maisha yanayojikita katika uaminifu yanajidhihirisha katika ukuu wake wote na uongozawanaume na wanawake waaminifu na kuwa wanaoaminika katika hali zozote zile.

Lakini ili kufikia katika maisha mazuri sana kama haya haitoshi hali yetu ya kibinadamu, bali ni muhimu kwamba uaminifu wa Mungu uingie katika uhai wetu na kutuambukiza. Neno hili la Sita ( Usizini) linatualika  kuwa na mtazamo kwake Kristo, ambaye kwa uaminifu wake anaweza kutondolea kwetu moyo wa uzinzi na kutupatia moyo mwaminifu. Katika yeye na ndani yake tu, kuna upendo bila kubakiza, bila majuto, kutoa kwa dhati bila kubakiza au kukaribisha na uwazi wa kupokea hadi mwisho. Baba Mtakatifu amehitimisha: “Kutoka katika kifo na ufufuko ndipo unafikia uaminifu wetu, kutokana na upendo wake usio na masharti unafika mara kwa mara mahusiano yetu. Kutoka katika muungano pamoja naye, na Baba na Roho Mtakatifu unafikia muungano kati yetu na uwezo wa kujua namna ya kuishi kwa uaminifu na vifungo vyetu.

 

 

 

 

 

24 October 2018, 14:15