Cerca

Vatican News
kalenda imetolewa ya Maadhimisho ya misa za Papa kwa siku zijazo kalenda imetolewa ya Maadhimisho ya misa za Papa kwa siku zijazo   (AFP or licensors)

Kalenda ya maadhimisho ya Papa Novemba - Januari 2019!

Maadhimisho ya Papa Francisko kwa mwezi Novemba 2018 hadi Januari 2019, yametolewa. Maelekezo yanaanza siku ya Ijumaa tarehe 2, kwa Ibada ya misa ya kuwaombea marehemu wote katika makaburi ya Laurentino mjini Roma, saa 10.00 jioni masaa ya Ulaya

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mwadhimishaji Mkuu wa Misa za Papa mjini Vatican Monsinyo Guido Marini ametoa kalenda ya maadhimisho ya Misa za Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia mwezi Novemba 2018, hadi Januari 2019.  Maadhimishao hayo yananza na siku ya Ijumaa tarehe 2 Novemb 2018, ambapo Baba Mtakatifu ataadhimisha misa katika makaburi ya Laurentino mjini Roma, saa 10.00 jioni masaa ya Ulaya kwa ajili ya marehemu wote.

Jumamosi tarehe 3 Novemba 2018, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu ataadhimisha misa Takatifu saa 5. 30 asubuhi majira ya Ulaya kwa ajili ya makardinali marehemu walioaga dunia kwa kipindi cha mwaka mzima. Tarehe 18 Novemba 2018, Jumapili ya XXXII ya kipindi cha kawaida, itakuwa ni maadhimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya Siku ya Masikini dunia saa 10.00 asubuhi.

Katika Mwezi Desemba

Jumamosi, tarehe 8 katika ni Sikukuu ya Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, Papa Francisko anatarajiwa kwenda katika Uwanja wa Hispania kama ilivyo utamaduni, saa 10.00 jioni masaa ya Ulaya, kutoa kuweka shada la maua kwa heshima ya Bikira Maria. Tarehe 12 Desemba 2018, ni sikuu ya Bikira Maria wa Guadalupe, ambapo Papa Francisko anatarajia kuadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 12.00 jioni.

Jumatatu 24 Desemba ni mkesha wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, Misa inatarajiwa kuadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 3.30 za usiku. Jumanne 25 Desemba 2018 ni Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa maana hiyo saa 6.00 mchana, Baba Mtakatifu anatarajiwa kutoa Baraka ya Urbi et Orbi Mbele ya kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Jumatatu tarehe 31 Desemba, ni sikukuu ya Maria mama wa Mungu, ambapo la ya masifu na utenzi wa Shukrani vinatarajiwa kufanyika saa 11.00 Jjoni masaa ya Ulaya. Jumanne tarehe 1 Januari 2019, ni sikukuu ya Mama Maria mama wa Mungu na Siku ya Amani duniani. Saa 4.00 asubuhi, inatarajiwa kufanyika misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Jumapili tarehe 6 Januari 2019 ni sikukuu ya Epifania. Misa Takatifu inatarajiwa kufanyika saa 4.00 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Dominika, baada ya Epifania tarehe 13 Januari 2019 ni sikuu ya Ubatizo wa Bwana kwa maana hiyo katika Kanisa la Sistina itafanyika Misa Takatifu ya ubatizo wa baadhi ya watoto saa 9.30 asubuhi masaa ya Ulaya. Jumatano tarehe 23 hadi Jumatatu 28 Januari 2019 itakuwa ni ziara ya Kitume chini Panama.               

23 October 2018, 15:05