Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekumbuka kwa namna ya pekee waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Indonesia Papa Francisko amekumbuka kwa namna ya pekee waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Indonesia  (Vatican Media)

Indonesia:Papa amesali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko!

Papa Francisko amesali kwa waathirika wa tetemeko. Inasadikika ni waathirika zaidi ya 800 wa tetemeko la adhi nchini Indonesa, lakini baadhi ya maeneo ya Kisiwa cha Sulawesi inakuwa vigumu kufika. Na hilo ni tetemeko lililotokea Ijumaa 28 Septemba na Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi hadi kufikia urefu wa mita 6

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya watu wa Indonesa katika Kisiwa cha Sulawesi, kilichokuwa na tetemeko la ardhi na matokeo ya Tsunami siku ya Ijumaa 28 Septemba 2018. “Ninasali kwa ajili ya marehemu, ambao kwa bahati mbaya ni wengi” amesema Baba Mtakatifu  na kusali sala ya  Sala ya Salam Maria , “kwa ajili ya majeruhi na wote waliopoteza nyumba na kazi. Bwana awafariji na kuwapa nguvu wote ambao wanajikita katika kupeleka msaada”.

 Thamini wa wathirika inazidi kuongezeka

Kwa mujibu wa shirika la majanga la kitaifa linathisha kuwa takriban watu 832 wameuawa baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kupiga kisiwa cha Indonesia cha Sulawezi. Hata hivyo takwimu hivyo Shirika hilo liloongeza kuwa eneo lililoathiriwa lilikuwa kubwa kuliko iliyodhaniwa. Watu wengine waliripotiwa kukwama kwenye vifusi vya mango yaliyoporomka siku ya Ijumaa iliyopita. Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6. Waokoaji wamekuwa wakichimba kwa mikono wakiwatafuta manusura kwenye mji wa Palu.

Kuna wasi wasi kuhusu hali ya mji wa Donggala ambapo kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Shirika la msalaba mwekundu limekuwa likikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wameathiriwa na tetemeko hilo la ardhi na tsunami lililotajwa kuwa janga ambalo litazidi kuwa baya zaidi. Makamu rais nchini Indonesia Jusuf Kalla alisema idadi kamili ya watu waliouawa inaweza kufika maelfu lakini hadi sasa idadi kamili bado.

Mitetemeko midogo ya ardhi imekuwa ikiendelea kupiga kisiwa hicho tangu siku ya Ijumaa 28 Septemba 2018. Rais Joko Widodo yuko Palu na amekagua maeneo yaliyoathiriwa na janga hili zikiwemo fukwe za Talise, eneo kuu la kitalii lililoathiriwa vibaya na tsunami. Miili imekuwa ikitapakaa kwenye mitaa ya mji na waliojeruhiwa wanatibiwa kwenye mahema kwa sababu hospitali ziliharibiwa. Walionusurika mjini Palu walilala nje siku ya Jumamosi kufuatia onyo la kuwatahadharisha wasirudi makwao.

Jitihada za Caritas mahalia na kwingineko

Hata hivyo juhudi za Caritas ya Manado na Makassar  mahalia, ambao wako karibu na maeneo yaliyoathirika wanaendelea kutuma vikundi vya dharua. Kwa mujibu wa Padre Banu Kurnianto Mkurugenzi wa Caritas wa Indonesia, amethibitisha kuwa, shughuli hiyo siyo rahisi. Hata serikali inaendelea kukusanya data ili kuweza kuhakikisha msaada wa haraka, na kuwaomba msaada mashirika yote. Na Caritas nchini Italia, tayari imetenga kiasi cha fedha elfu 100,000 kwa ajili ya mahitaji ya dharura.

 

01 October 2018, 09:02