Waamini na mahujaji wakipokea zawadi ya Msalaba iliyotolewa na Papa Francisko tarehe 16 Septemba mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, mjini Vatican Waamini na mahujaji wakipokea zawadi ya Msalaba iliyotolewa na Papa Francisko tarehe 16 Septemba mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, mjini Vatican 

Zawadi ya Papa: Msalaba ni ishara ya Upendo wa Mungu na jirani!

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa kushangaza watu wote waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 16 Septemba 2018, Baba Mtakatifu amesema ni siku mbili zimepita mara baada ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, kwa maana hiyo nimefikiria kuwazawadia msalaba ninyi nyote mliopo katika uwanja huu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Siku chache mara baada ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, iliyoadhimishwa kunako tarehe 14 Septemba, na hivyo kufuatia fursa hiyo imetolewa zawadi ya msalaba katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro Mjini Vatican, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 16 Septemba 2018.

Ni zawadi maalum ambayo Papa Francisko amependa kuwazawadia waamini na mahujaji wote waliofika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro, kusali naye. Ilikuwa ni maelfu ya misalaba ambayo imegawiwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, wakiwa ni watawa, maskini, wahamiaja na watu wa kujitolea ambao wanashirikiana na mfuko wa Sadaka ya Vatican.

Kuhusiana nazawadi: msalaba huo ulikuwa umewekwa katika mfuko na wakati kuna karatasi ndani iliyo andikiwa maneno yaliyotamkwa na Papa Francisko wakati wa Kufanya Njia ya msalaba wa Vijana nchini Brazil 2013: Maneno yalikuwa, Katika Msalaba wa Kristo kuna upendo wote wa Mungu, kuna huruma kuu isiyo na kifani.

Ushuhuda wa vijana na watu wa kujitolea: Baadhi y a vijana na watu wa kujitolea ambao wamepata kuhojiwa na Vatican news, wakati wanagawa zawadi ya Baba Mtakatifu Francisko, kila mmoja alionesha furaha na kuguswa kwa namna ya pekee ya zawadi hiyo, kama ishara ya mshikamano  na ushirikishwaji, hasa kwa upande wao wahamiaji na wakimbizi ambao wametoka katika sehemu mbalimbali, na kila mmoja akiwa na historia yake binafsi ya kusikitisha na kushangaza!

 

17 September 2018, 11:02