Cerca

Vatican News
Papa Francisko anathibitisha, Sinodi iwe zaidi udhihirisho wa pekee na ufanisi katika utekelezaji kwa msukumo wa nguvu ya mabaraza yote ya Maaskofu wa makanisa mahalia Papa Francisko anathibitisha, Sinodi iwe zaidi udhihirisho wa pekee na ufanisi katika utekelezaji kwa msukumo wa nguvu ya mabaraza yote ya Maaskofu wa makanisa mahalia 

Papa:Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya huduma ya Watu wa Mungu!

Wiki mbili kabla ya kuanza Sinodi ya Maskofu kwa ajili ya Vijana, imetolewa Katiba ya Kitume ya Papa Francisko, Episcopalis communio juu ya muundo wa kiungo cha Katiba kilichoanzishwa na Papa Paulo VI kunako 1965!

 Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kushauriana kwa Watu wa Mungu na Kanisa la pamoja ambalo hata utendaji wa urithi wa Petro unaweza kupata mwanga zaidi. Ndiyo mbiu ya sifa za Katiba ya Kitume “Episcopalis communio” juu ya Muundo wa Sinodi ya Maaskofu ambayo Papa Francisko ameitoa katika  tarehe ya 15 Septemba, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza Sinodi ijayo ya Maaskofu, inayotarajiwa kunako tarehe 3 Oktoba 2018, ikiwa ni mwanzo wa Sinodi ya XV ya Maaskofu itakayoongozwa na mada,“vijana, imani na maang’amuzi ya miito”. Katika Katiba hiyo vipengele muhimu vimeelezwa kwa uwazi na ufasaha  na kwa ufupi unatazama, msisitizo  juu ya mkutano wa maaskofu kwa ajili ya wema wa Kanisa, kuelezea maana ya Sekretarieti kuu, utendaji wa maaskofu kwa makanisa yote, namna ya maaskofu kusikiliza watu wa Mungu, pia masuala ya umoja wa wakristo wote.

Muungano wa Maaskofu kwa ajili ya wema wa Kanisa

Baba Mtakatifu katika Katiba hiyo Episcopalis communio, mara baada ya kukumbuka jinsi gani Katiba ilikuwa imetolewa uamuzi na Papa Paulo VI, tarehe 15 Septemba 1965, na kubaki moja ya urithi wa thamani wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, anasisitizia juu ya “ufanisi wa ushirikiano” wa Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Roma,  katika masuala makuu muhimu  hasa yanayotakiwa kuzingatiwa kidhamiri na busara kwa ajili ya wema wa Kanisa zima”. “Katika kipindi cha kihistoria, na kuonesha mahali ambapo Kanisa linajikita kwa upya katika “hatua ya uinjilishaji” kwa njia ya “uwepo wa utume wa kudumu”, Sinodi ya Maaskofu, inatwa,“ kuwa zaidi na zaidi mfereji  unaofaa” kwa ajili ya uinjilishaji wa dunia leo hii. Baba Mtakatifu athibitisha.

Sekretarieti Kuu

Papa Montini tayari alikuwa amekwisha ona ya kwamba , kadiri kipindi kinavyopita , katiba hiyo ingeweza kupyaishwa kwa maana hiyo hata, kuna  Mwaka 2006, toleo la mwisho la “Ordo Synodi,” lililotangazwa na  Papa Benedetto XVI.  Kwa namna ya pekee liliwekwa na kwa taratibu, kutiwa nguvu katika shughuli zake binafsi za Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu, inayojumuishwa na Sekretarieti Kuu na moja ya Baraza Kuu ka Ushauri la Maaskofu.

Utendaji wa Maaskofu kwa Makanisa yote

Kisha kutazama ufanisi wa hatua za matendo ya sinodi “ mbele ya masuala yanayotaka kuingiliwa kwa wakati na kwa muafaka wa wachungaji wa Kanisa”,  “katika miaka hii kumeongezeka utashi ya kuwa, Sinodi iwe zaidi udhihirisho wa pekee na ufanisi wa utekelezaji kwa msukumo wa mabaraza yote ya maaskofu wa Makanisa yote mahalia “yanayojikita kusimamia juu ya imani imara”  na kwamba “wachungaji wote wameundwa kwa ajili ya huduma kwa Watu wa Mungu, mahali ambamo wao wenyewe wamo kwa mujibu wa Sakramenti ya Ubatizo”.

Kusikiliza

Akinedelea katika Katiba hiyo, Papa anathibitisha, Askofu ni wakati huo huo“ mwalimu na mfuasi” katika wajibu ambao ni pamoja na utume na kusikiliza sauti ya Kristo ambaye anazungumza kwa njia ya Watu wa Mungu, kwa namna ya kuwafanya wasipotee wakati wanaamini”. Kwa maana hiyo hata Sinodi,“ lazima daima iwe chombo mwafaka cha kusikiliza Watu wa Mungu”, kwa njia ya ushauri wa waamini wa Makanisa mahalia, na ili kama ndiyo kweli, kiungo msingi wa kiaskofu, ina maana ya ukweli kwamba haiwezekanu kuishi kwa kutengana na waamini wanaobaki”.

Sinindo kwa maana hiyo  ni chombo kinachostahili cha kutoa sauti kwa Watu wote wa Mungu kwa njia ya Maaskofu”, “ kulinda, kutafsiri na kushuhudia imani”, na  kuonesha mkutano ndani ya Mkutano  kama kielekezo cha Upamoja wa Kanisa lenyewe, mahali ambapo wanajitazama katika muungano wa tamaduni tofauti. Na zaidi, shukrani ya Sinodi ya Maaskofu, ambayo itakuwa wazi  na kuonesha kuwa kuna “ushirikiano wa kina” ndani yake iwe kati ya Wachungaji  na waamini, na hata kati ya Maaskofu na Papa.

Umoja wa wakristo wote

Katika Katiba hiyo, Episcopalis Communio, matumaini ya Papa Francisko ni kwamba shughuli ya Sinodi hiyo inaweza kuwa “ kwa namna nyingine ili kuchangia kuundwa upya kwa umoja kati ya wakristo wote, kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu”. Kwa kufanya hivyo, umoja huo utasaidia Kanisa Katoliki, kwa mujibu wa maombi ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyo uwezea katika Waraka wa Ut unum sint, maana yake ili tuwe na umoja “ili  kupata mtindo wa zoezi la juu ambalo   bila kukataa kwa namna yoyote umuhimu msingi wa  utume wake,ambao unafunguka katika hali mpya”.

18 September 2018, 15:49