Siku ya Viziwi Duniani:Papa anasema ushirikishwaji uwe mtindo!
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Ujumbe wa kuelezea ukaribu wakati anasubiri Mkutano wao, ndiyo sababu ambayo Papa Francisko ameandika ujumbe wake kwa Chama cha Kitaifa cha Viziwi (E.N.S) ambacho kimejikita katika kupambana na ubaguzi na kuhamasisha thamani ya maisha wakati wa kuadhimisha mwaka 60 wa Kimataifa Duniani kwa viziwi. Chama hicho kinajikita kwa kuanzisha mambo mengi yanayohusu mshikamano.
Jitihada, sadaka , mapambano ya kila siku
Katika Ujumbe wa Chama cha Kitaifa cha Viziwi (E.N.S) Papa Francisko anaandika: “ni historia iliyoundwa na watu ambao wameamini katika umoja, katika mshikamano na katika ushikirishano wa pamoja, kwa nguvu ya kuwa jumuiya ndani ya safari ya muda mrefu na nyenye maendeleo, ambayo haikosi sadaka na mapambano ya kila siku. Ni historia ya yule ambaye hakukata tamaa na kuendelea kuamini katika kujitegemea kwa watu viziwi. Hii ni matokeo mazuri, Baba Mtakatifu, akiwa anafikiria watu wengi viziwi na familia zao ambao, wanakabiliwa na changamoto ya ulemavu, na kwamba hawahisi tena kuwa peke yao”.
Watoto na wazee ni waathirika wa kubaguliwa
Hata hivyo katika ujumbe wa Papa Francisko anatazama pia maendeleo makubwa yaliyofikia kwa mantiki nyingi, lakini wakati huo huo, hata kuenea kwa “utamaduni wa hatari na usiyokubalika, kwa sababu ya mgogoro wa kupungua maadili ya kibinadamu ambayo kwa sasa haifai tena kwa maana ya kwamba haiweki mtu kuwa kitovu , bali inatafuta maslahi ya kiuchumi, madaraka na matumizi hovyo (taz Esort. ap. Evangelii gaudium, 52-53)."
Watu wenye udhaifu ni miongoni mwa “waathirika wa utamaduni huu”, anasisitiza Papa, hasa “watoto “ambao wana shida ya kuweza kushiriki katika maisha ya shule” na “wazee” ambao hupata upweke na kuachwa, “vijan” ambao hupoteza maana yao ya maisha na wanajiona kuibiwa wakati wao endelevu na ndoto zao bora”.Ameandika Baba Mtakatifu.
Thamani ya kutengeneza chama
Papa Francisko amesisitizia pia juu ya thamani ya kutengeneza na kuwa mwanachama. “Ninyi si jumla ya watu, lakini mmejiunga ili kuishi na kuonesha mapenzi ya kuwasindikiza na kuwasaidia wale, ambao, kama ninyi wako katika shida lakini hawali ya yote ni wabebaji wa mali isiyo na kifani na thamani ya kibinadamu. Leo hii kuna haja kubwa ya kuishi na furaha na kujitolea katika mshikamano: kuwa na umoja wa kukutana, uzoefu wa kubadilishana, mafanikio na kushindwa, kuunganisha rasilimali, yote haya huchangia kuongezeka urithi wa mwanadamu, kijamii na utamaduni wa watu”.
Hebu twende kinyume cha mawazo ya sasa
Baba Mtakatifu amewaomba kwa hakika waende kinyume na mawazo ya sasa, na ili kupambania hadhi ya mwanaume na mwanamke, kupokea na kujiwezesha mwenyewe. Changamoto ni ile ya kujumuishwa na kuwapokea ambayo ndiyo iwe hisia na utamaduni katika sheria na serikali zisikose kuwa sababu ya sasa ya dhati katika kutoa msaada. Kuna haki za kuhakikishia pamoja na vizuizi vya dhati vinavyopaswa kushinda: “Ni lazima tujitoe nafsi zetu”, anaandika Papa, “kuvunja vikwazo vyote vinavyozuia uwezekano wa uhusiano na mkusanyiko wa uhuru na kufikia utamaduni na utendaji halisi wa kushirikishwa na hii inatumika katika jumuiya za kiraia na jumuia ya Kanisa.
Umuhimu wa maono ya Kanisa
Papa ametoa hata mafanikio yaliyopatikana katika ngazi ya kijamii na kitaaluma kwa wanachama wengi wa E.N.S. ambao pia wanashiriki katika muktadha wa Kanisa, Papa anasema: “ jinsi gani nilivyo na furaha sana wakati ninapoona kuwa ninyi , pamoja na watu wengine wenye ulemavu, kwa nguvu ya ubatizo wenu mnafikia malengo hayo hata ndani ya Kanisa, hasa katika uwanja wa uinjilishaji! Mfano huo unageuka kuwa kichocheo kwa jumuiya za Kikristo katika maisha yao ya kila siku”.
Hitimisho la ujumbe wake ni ushirikiano katika kila jimbo kati ya watu viziwi na wahudumu wa wakichungaji walioandaliwa kwa ushirikiano kamili na hisia kamili. “Kwa sababu hiyo anaandika, huduma ya kiuchungaji inayojumuisha, inahitajika katika parokia, vyama vya kitume na mashuleni”. Kazi nyingi zimefanyika na mengi bado yanatakiwa kufanywa, anasisitiza Papa, “kwa kukuza watu viziwi ili kushinda kutengwa kwa familia nyingi na kuwakomboa wale ambao bado wanahusika na ubaguzi usiokubaliwa”.