Tafuta

Vatican News
Rais wa  Vietnam Tran Dai Quang amefariki dunia Rais wa Vietnam Tran Dai Quang amefariki dunia   (ANSA)

Rambirambi kutoka kwa Papa kufuatia kifo cha Rais wa Vietnam

Katika telegram ya Papa, anaonesha masikitiko yake na kuwahakikishia maombi yake kwa rais wa Vietnam, bwana Tran Dai Quang, aliyekufa akiwa na umri wa miaka 61

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kufuatia  kifo cha Rais wa Vitnam Tran Dai Quang, Papa Francisko ametuma salam za rambirambi. Anaonesha masikitiko yake na kuwahakikishia maombi yake kwa rais wa Vietnam, Tran Dai Quang, aliyekufa akiwa na umri wa miaka 61. Rais Tran Dai Quang alichaguliwa kunako tarehe 2 Aprili 2016.

Ziara yake

Tarehe 23 Novemba 2016 alipata fursa ya kukutana na Papa Francisko.  Katika maongezi yao, yaliyokuwa yametolewa na vyombo vya habari Vatican yanaonesha mahusiano mema yaliyopo baina ya Vatican na nchi ya Vietnam, kwa kuongozwa na roho ya umoja katika mazungumzo na msimamo wa pamoja, na  katika kutafuta zana muhimu ili waweze kuendelea zaidi katika ulewanao na walionesha pia ushirikiano kati ya Kanisa na serikali kwa mantiki nyingi za kijamii mahalia.

22 September 2018, 09:29