Tafuta

Vatican News
Uchumi lazima uhudumie binadamu na siyo kunyonya na kuiba rasilimali zake. Leo hii tuaalikwa kutazama hata uwezekano wa teknolojia iliyo mbele yetu Uchumi lazima uhudumie binadamu na siyo kunyonya na kuiba rasilimali zake. Leo hii tuaalikwa kutazama hata uwezekano wa teknolojia iliyo mbele yetu 

Papa:Wote tunapaswa kuwajibika kwa ajili ya mwingine!

Baba Mtakatifu ametoa ushauri kwamba,wafuate mfano wa Mtakatifu Francisko wa kutunza kile kicho kidhaifu na kuwa na ekolojia fungamani ya kuishi kwa furaha na udhati. Uchumi lazima uhudumie binadamu na siyo kunyonya na kuiba rasilimali zake. Leo hii tuaalikwa kutazama hata uwezekano wa teknolojia iliyo mbele yetu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 1 Septemba 2018 wakati Kanisa Katoliki na makanisa mengine, wanaadhimisha Siku ya IV ya  maombi  kwa ajili ya huduma ya viumbe duniani,  Baba Mtakatifu Francisko amepata fursa ya kukutana mjini Vatican  na kikundi cha  wawakilishi wa wafanyakazi ambao wanashiriki Mkutano kuhusu siku hii. Katika hotuba yake, amewakaribisha wote na kufurahia kutokana na kujikita katika safari ya kutafakari mwisho wa wiki hii kwa namna ya pekee siku ya Dunia kuombea huduma ya Viumbe , mkutano wao unaoongzowa na Waraka wake wa Laudato Si, yaani Sifa kwa Bwana. Kadhalika anawasifu kwa ajili ya juhudi zao za dhati katika kusaidia manedleo endelevu. Amemshukuru  kwa dhati Bwana Peter Kurth Mwenyekiti wa wawakilishi hao kutokana na hotuba na sala zake.

Baba Mtakatifu ametoa ushauri kuwa wafuate mfano wa Mtakatifu Francisko wa kutunza kile kicho kidhaifu na kuwa na ekolojia fungamani ya kuishi kwa furaha na udhati. ( taz. Laudato si’ 10). Kwa upande wa Mtakatifu Francisko, anaongeza: kila aina ya mguso wa mtu na mambo ya dhati yalikuwa yanageuka kuwa mkutano na Muumba. Ni kwa imani yake na Mungu ambayo ilitokana na utume wake wa haki, kwa ajili amani na kuheshimu viumbe!

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anashauri , hata kila mmoja wenu anao wajibu kwa ajili ya wengine na kwa wakati endelevu wa sayari yetu. Ikiwa ni pamoja na inayo fanana na  hiyo, uchumi lazima uhudumie binadamu na siyo kunyonya na kuiba rasilimali zake. Leo hii tunaalikwa kutazama hata uwezekano wa teknolojia iliyo mbele yetu, kwa matumizi mema ya rasilimali, na kusaidia kwa namna ya pekee nchi zilizokumbwa na umasikini,na kuwa na uwezekano wa kutafuta njia za kupyaisha na katika maendeleo endelevu na fungamani.

Baba Mtakatifu amehitimisha hotuba yake akiwa na matumaini ya kwamba, wanaume na wanawake wa nyakati hizi, kwa utambuzi, kuwa wote ni wana wa Baba na Muumba wa mbingu na dunia wanaweza kutoa mchango daima na zaidi, kwa udhati ili wote kwa pamoja kuwa na uwezo wa kushirikishana rasilimali zenye thamani ya ardhi. Anawatia moyo waendelee kutoa lengo hilo maalum kwa namna ya pekee ili kusaidia. Amehitimisha akiwabariki wao na kazi zao kwa Baraka Takatifu. Amewashukuru na kuomba sala kwa ajili yake kama kawaida yake.

01 September 2018, 14:36