Bado hata leo hii  vita inaendelea nchini Siria Bado hata leo hii vita inaendelea nchini Siria  

Papa:Wito wa Papa kwa jumuiya kimataifa kwa ajili ya Siria!

Papa Francisko amesema, ni uchungu wa kuona bado kuna upepo wa vita kutokana na habari ambazo zimefika zinazo ashiria juu ya hatari ya uwezekano wa majanga ya kibinadamu nchini Siria, katika Wilaya ya Idlib.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ndugu kaka na dada,  jana huko Košice Slovakia  alitangazwa Mwenye heri Anna Kolesárová, bikira na shahidi , aliyeuwawa kutokana na kupinga ya yule aliyetaka kumwondolea hadhi yake na usafi wake. Ni kama vile Maria Goreti wetu wa Italia. Msichana huyo jasiri awasaidie vijana wakristo kuwa kidete katika uaminifu wa Injili hata kama inawataka kwenda kinyume na hali halisi kufikia kulipa gharama binafsi… Tumpigie makofi Mwenye heri Anna Kolesarova…..

Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Sala ya malaika wa Bwana katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, mjini Vatican, Dominika tarehe 2 Septemba 2018, akiwaeleza mahujaji na waamini waliofika katika uwanja huo kutoka pande zote za dunai.

Wito wa Papa kwa ajili ya kusaidia nchi ya Syria

Akiendelea, Baba Mtakatifu anasema, ni uchungu: ambao bado kuna upepo wa vita kutokana na  habari ambazo zimefika zinazo ashiria  juu ya hatari ya uwezekano wa majanga ya kibinadamu nchini Siria, katika Wilaya ya Idlib. Anarudia kutoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa, kwa hata wadau wengine wanaohusika ili kwa kutumia zana za kidiplomasia, za mazungumzo na michakato, wanawez kweli kuheshimu haki za kimataifa za kibinadamu na kwa ajili ya kuokoa maisha ya raia.

Amewasalimia ndugu wote mahujaji waliotoka nchini Italia na sehemu mbalimbali za dunia. Kwa namna ya pekee amewapa salam makatekista wa Cerano ya Mtakatifu Marko, vijana wa Montirone, vijana wa Rovato  na wengine waliofika kutoka nchi ya Huispania, baada ya safari yao ndefu, pia kwa namna ya pekee muunganiko wanaclub ya pikipiki ya aina ya Vespa waliokuwa uwanja huo kuungana naya katika sala na  amewakaribisha. Kwa wote ameawatakia Jumapili njema na kuomba kama  kawaida yake  wasali kwa ajili yake.

 

 

03 September 2018, 09:45