Vatican News
Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa  Chama Katoliki Italia Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Chama Katoliki Italia   (Vatican Media)

Papa:Wazazi na walimu wapeleke mbele agano la kuelimisha watoto!

Familia kwa sasa haitoi sifa tena kwa shule na walimu kama ilivyo kuwa kipindi cha kazi ya walimu zamani, kwa maana hiyo inahitajika kukazia elimu kwa watoto, mazungumzo pia kuwa na imani ya shule. Hayo ni maono ya Papa Francisko wakati wa kukutana na wawakilishi wa Chama cha Wazazi nchini Italia tarehe 7 Septemba 2018 katika Ukumbi wa Papa Paulo VI

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ninayo furaha ya kuwapokea ninyi nyote wawakilishi wa  Chama cha Wazazi Italia na wazazi ambao mwaka huu mntimiza miaka 50. Ni mstazamio mazuri! Ni fursa ya kwa  kuthibitisha kwenu sababu ya shughuli hiyo kwa ajili ya familia na elimu. Ni shughuli ambayo mnapeleka mbele kwa mujibu wa misingi ya maadili ya kikristo ili familia iwe daima jambo linalotambulika na kuwa mstari wa mbele katika maisha ya jamii.

Huo ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Septemba 2018, wakati alipokutana na wawakilishi wa Chama cha Wazazi nchini Italia katika Ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI mjini Vatican. Akiendelea na hotuba yake anasema: Ni nguvu zao  ambazo wanajikita na kuwa karibu na kusaidia wazazi kwenye shughuli yao ya elimu hasa kwa mtazamo wa shule ambayo daima imekuwa msingi wa ushiriki wa familia katika kuwafunza watoto.  Kile wanachokitenda katika uwanja huo kwa hakika kinastahili sifa. Leo hii kwa hakika wanapozunguza juu ya agano la elimu kati ya shule na familia, ni kuzungumzia tu hasa juu ya kuripoti madhaifu: hiyo ni kutokana na kwamba Familia kwa sasa haitoi sifa tena kama ilivyo kuwa katika kipindi cha kazi ya walimu zamani, na ambapo kwa sasa hao pia wanahisi kama vile usumbufu unao wakera wa uwepo wa wazazi katika shule, hadi kufikia kuweka pembezoni au kufikiriwa kama maadui, wakati huohuo wao wanalipwa hata  mishahara midogo.

Walimu na wanapeleka agano mbele

Katika kubadili hali halisi hiyo, inahitaji mtu mmoja mmoja awe wa kwanza kupiga hatua ili kushinda ile hofu ya mwingine na kunyosha mikono ya ukarimu. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anawaalika kukuza  na kuongeza daima imani kwa ajili ya shule na walimu. Anasisitiza kwamba, bila ya walimu, ipo hatari ya kubaki wapweke katika matendo yao ya elimu,  pia kutokuweza kuwa na  uwezo wa kukabiliana changamoto mpya za elimu ambao zinatokana na utamaduni wa sasa, kama vile katika jamii ya mitandao ya kijamii  na teknolojia mpya. Walimu ni kama wazazi, anabainisha Baba Mtakatifu na kuongeza kusema, wao wanajikita kila siku katika huduma ya kuwaelimisha watoto wao.  Iwapo kuna haki ya kilalamika katika vikwazo vya matendo yao , labda  ingekuwa vizuri na ni wajibu wa kuwatia moyo, kama watu wenye thamani ya agano la uwekezaji wa elimu ambayo kwa pamoja wao wanapeleka mbele.

Mfano wa mapatano kati ya wazazi na walimu

Baba Mtakatifu ametoa raia kwa wanachama hao kwani, hakukosa kutoa mfano wake binafsi, ya kwamba alipokuwa  na umri wa miaka 10 siku moja alisema neno moja  baya kwa mwalimu, na mwalimu huyo alimwita mama yake.  Kesho yake mama yake alikwenda shuleni,na kupokelewa na mwalimu huyo. Ofisini walizungumza na baadaye akaitwa. Mbele ya mwalimu huyo, Papa alikaripiwa na kuambiwa na mama yake, aombe msamaha kwa mwalimu. Na alifanya alivyo, na pia kuambiwa na mama ampe hata busu. Mama yake alirudi nyumbani. Papa wakati huohuo ndani ya darasa alikuwa mwenye furaha na historia ikaishia hapo. Kwa mkazo zaidi ametaka kuonesha kuwa huo ndiyo “ushirikiano” katika kuelimisha mtoto kati ya familia na walimu!

Uwajibikaji na utayari ni ishara ya upendo 

Baba Mtakatifu akiendelea kukazia hilo amesema, uwepo wa uwajibikaji na utayari , ni ishara ya upendo ambao si kwa ajili ya watoto wao tu, bali hata kwa ajili ya wema wa wote ambao wapo shuleni na ambao utawasaidia kushinda zile tabia za migawanyiko na kutokuwa na uelewa katika mantiki hiyo, ili kuwafanya watambue katika familia nafasi msingi ya elimu na mafunzo kwa watoto na vijana. Anaongeza Baba Mtakatifu “ Iwapo ninyi wazazi mna shida na walimu, hata shule inawahitaji ninyi, na haiwezi kufikia malengo yake bila kutimiza mazungumzo yenye kujenga  na yule ambaye ndiyo wa kwanza kuwajibika katika kukuza wanafunzi wake”.

Kama Wosia wa Amoris Latitia unavyokumbusha kuwa, “ Shule haiwezi kuondoa  nafasi ya wazazi, lakini ina uwezo wa kuongezea na kuchangia. Huo ndiyo msingi wa kwanza ya kwamba kila mshiriki katika mchakato wa elimu lazima utendwe kwa jina la mzazi, kwa ruhusa yao na kwa vipimo kadhaa hata juu ya kuwajibika (84). Uzoefu wao wa chama kwa hakika umewafundisha namna ya kuaminiana kwa pamoja. Baba Mtakatifu Francisko ametumia msemo mmoja wa hekima ya mwafrika mmoja kwamba, “ Ili kuelimisha mtoto inajitajika kijiji” Kwa maana hiyo anaongeza, elimu ya shule haiwezi kamwe kukosa ushirikiano baina ya  watu mbalimba wa jumuia ile ile  ya elimu na bila mawasiliano ya mara kwa mara na bila imani ya pamoja, siyo rahisi kujenga jumuiya na bila jumuiya siyo rahisi kuelimisha.

Kanisa linasaidia kuondoa upweke katika elimu

Baba Mtakatifu anafafanua ya kuwa kuchangia kuondoa upweke wa elimu katika familia  ni kazi hata ya Kanisa, kwa maana hiyo anawaalika kuhisi kuwa daima Kanisa liko upande wao katika utume wa elimu kwa ajili ya watoto wao na jami iwe  mahali pa vipimo vya familia, ili kila mmoja aweze kuwa na uwezo wa kujikamilisha na kuwa mwenyewe katika makuzi ya pamoja.  Wao wana nguvu mbili Baba Mtakatifu anasema: ya kwanza ni ile itokanayo na kuwa mwanachama, yaani mtu ambaye anaunga mkono na siyo dhidi ya mtu mwingine, bali kwa ajili ya wema wa wote, na nguvu ya pili ni ile ambayo wanaipokea kutokana na mahusiano na jumuiya ya kikristo mahali ambao wanachota imani na msaada.

Watoto ni zawadi  ya thamani

Watoto ni zawadi ya thamani waliyoipokea, kwa maana hiyo watambue kuilinda kwa kuwajibika na ukarimu, kadhalika wawape uhuru wa lazima kwa ajili ya makuzi na kukomaa kama watu ambao siku moja nao watajifungulia zawadi ya maisha. Umakini walio nao kama chama, wawalinda na hatari ambazo zinasonga maisha hasa walio wadogo zaidi, lakini hatari hizo zisiwazuie kutazama ulimwengu kwa imani, kwa utambuzi wa kuchagua na kuwalekeza watoto wao fursa bora za makuzi ya kibinadamu, kizalendo na kikristo. Wawafundishe watoto wao kung’amua kiutu na , kimaadili. Hilo ni jambo jema kwa maana haipo ile hali ya kusema huyo ni mwema na huyo ni katili. Kwa maana ni wao watatambua namna ya kutofautisha, lakini suala hili lazima lifundishwe nyumbani na kufundishwa shuleni ni kusema sehemu zote mbili.Amehitimisha kwa kuwashukuru Mkutano huo na kuwabariki kwa moyo wote, familia za ona vhama vhao. Wakati huo huo anawakimbuka katika sala na wao vilevile wasisahau kusali kwa ajili yake.

 

 

 

 

 

07 September 2018, 14:25