Tafuta

Taalumungu ya wema katika Papa Francisko Taalumungu ya wema katika Papa Francisko  

Papa:Taalimungu ya wema si ya kufikirika tu bali ni halisi!

Taalimungu inaitwa kutangaza udhati wa upendo wa Mungu. Wema ni maisha ya kweli ili kutafsiri katika nyakati zetu zenye matokeo ambayo Bwana anatumwilisha sisi. Ni sehemu ya hotuba ya Papa Francisko tarehe 13 Septemba 2018 alipokutana na wajumbe wa Mkutano unaojikita juu ya Mada ya Taalimungu ya Wema wa Papa Francisko

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hivi karibuni mjini Asisi katika Kituo cha Kiroho cha Domus Pacis unafanyika mkutano wa Kitaifa , uliondaliwa na Kituo cha Familia Kiitwacho Cara della Tenerezza, ambapo wamejikita katika mada ya “Taalimungu ya wema wa Papa”. Mkutano huo umewaona watoa mada wa taalimungu, wanabiblia, na masomo ya binadamu. Huo ni mkutano ambao umeanzishwa na Ofisi ya Kitaifa ya Uchungaji wa Familia wa Baraza la maaskofu Italia, Baraza la Maaskofu wa Umbria, Taasisi ya Kitaalimungu Assisi, Shirika la ndugu wadogo wafranciskani wa Asisi na Taasisi ya Elimu ya Sayansi ya dini huko Assisi

Na katika fursa hiyo ya Mkutano, wajumbe wa Mkutano wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Septemba 2018 mjini Vatican, mahali ambapo Baba Mtakatifu Francisko amewakaribisha kwa shangwe kuu na kumshukuru Kardinali Gualtiero Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia kwa hotuba yake kwa niaba ya wajumbe wote. Amepta pongezi ya kusasishwa juu ya shughuli yao wanayoitenda. Kadhalika anasemasiku chache ziliopita wametafakati juu ya taalimungu ya wema, ki urahisi tu amesema, “mara nilipopata taarifa juu ya mada hiyo,nilianza kusoma. Na nilisoma kitabu ili niweze kutambua Rocchetta…ana akili… (wajumbe wamempigia makofi…)

Mapendekezo matatu: Baba Mtakatifu katika kuendelea na hotuba yake, ametaka kuwaelezea mambo matatu: kwanza jambo linalotazama juu ya kilelelezo cha taalimungu ya wema. Taalimungu na wema ni kama maneno mawili ambayo yako mbali: la kwanza ni kama kuingilia dhana ya kisomo na  jambo la pili ni kama kuingia katika mahusiano binafsi.  Katika hali halisi, imani yetu inatoa msukumo wa pamoja bila kuachana. Taalimungu kwa dhati, haiwezakani kuwa ya kufikirika, maana kama ingekuwa hivyo, basi hiyo ingekuwa ni itikadi, na kwa maana hiyo  inatokana utambuzi wa kuishi, inazaliwa kutokana kukutana  na Neno kufanyika mwili! Taalimungu inaitwa kwa maana hiyo kutangaza udhati wa upendo wa Mungu. Wema ni maisha ya kweli  ili kutafsiri  katika nyakati zetu zenye matokeo ambayo Bwana anatumwilisha sisi.

Leo hii, kwa dhati, umakini ni kidogo kulinganisha na nyakati zilizopita, juu ya dhana au mazoezi na zaidi juu ya "hisia”, Baba Mtatifu anabainisha. Inawezakana husipende, lakini ni ukweli: tunaanza kutoka kile tunachosikia. Taalimungu haiwezi kupunguzwa kwa hisia, lakini haiwezi hata kupuuza kwamba katika sehemu nyingi za ulimwengu, njia ya masuala muhimu ya maisha  haianzishwi  tena kwa maswali ya mwisho au madai ya kijamii, bali kwa  kile ambacho mtu huhisi kihisia.

Taalimungu inaongozwa na mwanga wa Neno la Mungu: Taalimungu  inaalika kuongoza utafiti wa kuishi  kile ambacho kimeletwa na mwanga ambao unatokana na Neno la Mungu. Na taalimungu nzuri ya huruma inaweza kupungua upendo wa Mungu kwa maana hii. Inawezekana, kwa sababu upendo wa Mungu sio msingi wa kawaida, lakini ni wa binafsi na halisi, kwamba Roho Mtakatifu huwasiliana kwa ndani. Roho huyo anafika na kubadili hisia na mawazo ya mtu.  Je! Ni mafundisho gani yanaweza kuwa katika  taalimungu  ya wema?  Kwa upande wa Baba Mtakatifu anasema ni  mawili ambayo yanaweza kuwa muhimu kwake. Ametoa ushauri wa aina mbili. Kwanza ni uzuri wa hisia ya kuhisi kupendwa na Mungu na hisia ya kupenda kwa jina la Mungu

Hisia ya kupendwa : huo ni ujumbe unakuja kwa nguvu katika nayakati hizi za mwisho, kutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu wa huruma na huruma kama jambo msingi ya Utatu Mtakatifu na maisha ya kikristo. Liturujia ya leo hii, ilikuwa inakumbusha Neno la Yesu: “muwe na huruma kama alivyo Baba yenu wa hruma” (Lk 6,36) Wema unaweza kulekezwa katika mtindo wetu kwa namna hiyo ya kuhisi leo hii huruma ya Mungu.

Wema unajionesha kwetu karibu na uso wa Baba, na ule wa Mwana wa Mungu anayempenda binadamu na ambaye anatupenda kwa upendo upeo,zaidi ya upendo mkuu ambao Mama anapenda mwanae (taz Is 49,15). Kila chochota mba cho chaweza kutukia, kile tufanyacho, tunao uhakika ya kwamba Mungu yu karibu, mwenye huruma, tayari kulia na sisi. Wema ni neno la baraka na kinga ya hofu kwa mtazamo wa Mungu, kwani “ katika upendo hakuna hofu”. (1Yh 4,18) kwa maana imani inashinda hofu. Kuhisi kupenda maana yake ni kujifunza kuamini Mungu na kumwambia kama yeye anavyopenda tusema: “Yesu ninakutumaini”.

Hayo na pia mambo mengine yanaweza kusaidia katika utafiti na ili kuweza kuipatia Kanisa Taalimungu ya haki, kwa ajili ya kutusaidia tuishi imani kwa utambuzi na shauku ya upendo na matumaini; kwa ajili ya kutushauri tupige magoti, tulioguswa na kujeruhiwa na upendo wa Mungu. Kwa maana hiyo wema unatupeleka moja kwa moja katika Mateso.

Msalaba kwa dhati: ni mhuri wa wema wa Mungu, ambao unachotwa katika madonda ya Bwana. Majeraha yanayoonekana ndiyo madirisha ambayo yanafungua wazi upendo wake usioonekana. Mateso yake, yanatualikia kubadili mioyo yetu migumu kama mawe ili kuwa ya nyama na kuwa na shauku ya Mungu na  kwa binadamu kwa ajili ya upendo wa Mungu.

Hisia ya kupenda : Baba Mtakatifu akiendelea na ufafanuzi huo juu ya hisia ameelezea mapendekezo yake ya kuhusu hisia ya kupenda. Binadamu anapohisi kweli amependwa, anahisi hata kupenda. Hata hivyo kama Mungu ni mwema zaid , hata binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wake anao uwezo wa wema. Wema kwa maana hiyo mbali na hisia za mapenzini hatua ya kwanza ya kushinda kunjia katika binafsi , ili kuweza kuondokana na ubinafsi,  ambapo hufungua uhuru wa binadamu. Wema  wa Mungu hutuongoza kuelewa kwamba upendo ni maana ya maisha. Kwa hiyo tunaelewa kwamba mizizi ya uhuru wetu haitakuwa kamwe na maoni ya kujitegemea binafsi.

Na tunahisi kuitwa kwa kutangaza katika ulimwengu upendo uliopokelewa kutoka kwa Bwana, kuuweka katika Kanisa, katika familia, katika jamii, kwa kujikita katika kuutafisri  katika kuhudumia na kujitoa wenyewe. Yote haya si kwasababu wajibu, lakini pia ni kutokana na upendo, kwa ajili ya upendo wa yeye ambaye tunapendwa kwa upendo upeo.

Taalimungu katika safari: Baba Mtakatifu akihitimisha, maelekezo mafupi ya taalimungu katika safari amesema. Inatakiwa taalimungu ambayo inatoka nje ya ufinyu wake ambao wakati mwingine imefungwa, kwa nguvu na kutembea kuelekea kwa   Mungu,kwa kushikana mkono  wa mtu;  taalimungu isiyo ya kibinafsi, lakini inayolenga huduma ya jamii; taalimungiu  ambayo haifurahi kurudia vielelezo vya zamani, bali yenyekuwa na Neno lililofanyika mwili. Kwa hakika ni neno la Mungu ambalo si bubu ( taz Eb 1,1-2:13,8), lakini mwili ambao umeitwa kujikita ndani mwake, unabadilika kila nyakati. Kuna kazi kubwa kuleta maana ya taalimungu na kwa ajili ya utume wake leo hii. Ni kufanya Neno la Mungu lifanyike mwili kwa ajili ya Kanisa, kwa ajili ya binadamu wa millenia ya tatu. Leo hii na zaidi inahitajika mapinduzi ya wema. Na hilo litatuokoa.Tukabidhi tafakari yenu ya kazi kwa Bikira Maria Mama mwema.

 Amewabariki  pamoja na jumuiya mahali ambapo wote wanatoka na kuwaomba wasali kwa ajili yake .

13 September 2018, 14:31