Papa Fancisko amekutana na wawakilishi wa Shirika la  Wana wa Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili Papa Fancisko amekutana na wawakilishi wa Shirika la Wana wa Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili  

Papa: Wasindikizeni vijana katika safari yao!

Papa Francisko amekutana na wajumbe 150 wa Shirika la Wana wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili na kuwapa ushauri wa kuwa karibu na kizazi kupya kwa kufuata nyayo za mwanzilishi wao Mtumishi wa Mungu Giuseppe Frassinetti

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wapende kizazi kipya na kuwa wasindikizaji katika safari yao kwa mfano wa Matakatifu John Bosco na Padre Giuseppe Frassinetti. Huo ndiyo wito wa Papa Francisko, alioutoa utoa katika hotuba yake, asubuhi ya tarehe 20 Septamba 2018, kwa wanashrika karibia 150 kutoka Shirika la Wana wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili ambalo ni shirika linalotoa huduma yake  katika nchi sita.  Papa Francisko amekutana na wajumbe hao wakiwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 150 tangu kifo cha mwanzilishi wa Shirika lao, Mtumishi wa Mungu Padre Giuseppe Frassinetti, ambaye amesema " kitovu chake kilikuwa ni wasiwasi  katika uchungaji wa mafunzo kwa ajili ya mapadre na kuthamanisha walei wa kike na kiume".

Kama Padre  Frassinetti na don Bosco

Akendelea na hotuba yake, Papa Francisko amewashauri kuendeleza nyayo za Mwanzilishi wao hasa ile hali ya kuhamasisha utume wa walei na undugu wa ushirikiano baina ya uklerio na Walei.  Ametoa hayo kwa kuongozwa na mtazamo wa Sinodi ya Maaskofu ijayo kuhusu vijana inayofunguliwa tarehe 3 Oktoba 2018.

"Padre Frassineti kama vile rafiki yake Don Bosco walitambua nafasi ya mkakati kwa ajili ya kizazi kipya kwenye jamii inayoendelea na kuelekeza maono ya wakati ujao", Baba Mtakatifu amesema. Katika dhana hiyo amewashauri " wapende kizazi kipya na kuwa wasindikizaji katika hija yao ambayo wakati mwingine imechanganyikiwa, lakini ikiwa imejaa utajiri wa ndoto ambazo ni sehemu ya wito wa Mungu".

Mtaguso wa Vatican II na watu wa Mungu

Katika Mtaguso wa Vatican II unathibitisha kuwa “ miito ya ulimwengu kwa waamini katika utakatifu imechimba mizizi katika Ubatizo". Kwa maana hiyo anawakumbusha kuwa, " watangulizi wake, waliendeleza mada hiyo kwa “utajiri mkubwa wakiwa na sababu na ubunifu wa maelezo”.  “Watangulizi hao,  kwa kusisitiza zaidi, walizungumzia juu ya kipimo kikuu cha maisha ya kikristo, ulazima wa kutangaza maisha mema ya Injili kwa huruma , busara na ujasiri” Na ndiyo hiyo hata Mtumishi wa Mungu Frassinetti ambaye katika karne ya XIX alipata nafasi kuu ya kutangaza mawazo ya utakatifu kwa Watu wa Mungu. Na  ni "mawazo ambayo yana matunda kwa wanachama wote wa Shirika la Wana wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili".

Uwajibikaji katika miito

Akihitimisha hotuba yake, amesema "kiini cha utume wao, uwe hata katika juhudi za miito. Kwa maana hiyo inahitaji ushirikiano na Mungu ili kuunda “ardhi nzuri” kama jinsi ilivyo muhimu kutoa mafundisho ya mwanzo, ya kudumu kwa wote walioitwa katika Uklero na maisha ya kitawa. Pamoja na hayo inahitaji uaminifu wa kuendelea katika utambulisho wa karama yao, kwa maana ya kuwa na msimamo wa kufanya mang’amuzi,  hata kusikiliza na mazungumzo.

20 September 2018, 16:10