Tafuta

Papa Francisko na washiriki wa Mafunzo kuhusu ndoa na familia Papa Francisko na washiriki wa Mafunzo kuhusu ndoa na familia 

Papa:Shuhudieni uzuri wa ndoa na ukaribu na familia zenye kipeo!

Akikutana na washiriki wa mafunzo juu ya ndoa na familia, Papa Francisko amewataka wawe wakatekumene wa kudumu kwa ajili ya familia. Anatoa wito pia kuwasaidia wale ambao wanajikuta katika kipeo cha ndoa, ili kurudia kwa upya neema ya Sakramenti, hata kuwaelekeza njia ya kufuta wakati wa mchakato wa kubatilisha ndoa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, ametoa hotuba yake kwa washiriki wa Jimbo, kwa Mafunzo  juu ya ndoa na familia, Semina iliyoandaliwa na Jimbo Kuu la Roma na Mahakama Kuu ya Kanisa. Mkutano na Baba Mtakatifu umefanyika Alhamisi jioni tarehe 27 Septemba 2018. Katika Hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki karibia 850 wa mafunzo kuhusu ndoa na familia, amegusia juu ya kuwa na utambuzi wa kuchagua, familia ya ndoa vijana wasiachwe katika upweke,kuwa maandalizi mema na baadaye kuwasindikiza baada ya kufunga ndoa, hali za vipeo na michakato ya kubatilisha ndoa, hatimaye mapokezi kwa wale ambao wanaamua kuishi bila kufunga ndoa. Baba Mtakatifu kadhalika ametoa wito wa kujikita katika safari ya kushirikishana kwa mapadre na wahudumu wa kichungaji na wanandoa wakristo na wawe na utambuzi wa kuchagua.

Akianzia juu ya siku ya mafunzo na tafakari inayohusu kutathimini changamoto na mipango ya kichungaji Papa anatafakari kwa upana na ugumu wa nyanja hiyo ya kutume, kuhusu familia, na kufikiria jinsi gani kanisa la nyumbani na dhabahu la maisha, lilivyo msingi  na lisilobadilishwa kwa ajili ya wema wa pamoja wa watu.  Katika kusisitiza zaidi, amethitisha ni  jinsi gani mada hiyo alivyoendeleza kwa marefu na mapana katika Wosia wake wa Kitume wa Amoris Laetitia, yaani Furaha ya ndoa ndani ya familia, na kuweka suala hili kama kituvo cha dharura, hasa katika maandalizi ya kufunga ndoa ya kikristo, na ambayo anasema isipunguzwe na kuishia katika mikutano tu.

Utambuzi wa kuchagua: Ndoa siyo tukio tu la “kijamii” bali ni Sakramenti ya kweli ambayo ni lazima iwe na maandalizi ya kutosha na yenye utambuzi  wa maadhimisho hayo. Kifungo cha ndoa kwa dhati kinahitaji sehemu zote mbili za wachumba kuchagua kwa utambuzi  wa dhati na kuweka moto zaidi katika utashi wa kujenga kwa pamoja jambo ambalo kamwe lisiweze kusalitiwa au kuachwa! Anathibitisha Papa.

Familia ya ndoa vijana wasiachwe katika upweke,

Katika majimbo mengi duniani kote, Baba Mtakatifu anadhihirisha kwamba, yanajikita kuendeleza na kuanzisha mada hiyo  kwa udhati, katika hali halisi ya maisha ya familia kichungaji, kwa kufanya semina, mafungo ya kiroho na sala; wakiwahusisha wanandoa, ili waweze kuwa na uzoefu msingi wa kifamilia kwa kusaidiwa na wataalam katika masuala ya kisaikolojia.

“Mara nyingi anabainisha, mzizi wa mwisho juu ya  matatizo ambayo yanakuja katika mwanga mara baada ya maadhimisho ya Sakramenti ya ndoa, ni ile ya kutafuta si tu ukosefu wa ukomavu uliojificha ndani na ambao utaibuka tu nje kwa gahafla, lakini zaidi ni ule udhaifu wa imani ya kikristo na ukosefu wa kusindikizwa kikanisa, ambapo hubaki na upweke wanandoa hao wapya, kwa kuwachwa pekee mara baada ya arusi ya kufunga ndoa.  Ndoa hizo zinavunjika mara baada ya kukabiliana kila siku maisha yao ya pamoja ambayo yanawaalika wanandoa wakue katika safari ya kujitoa wao bianafsi kwa mwingine na kwa sadaka, ambapo,  ndipo wanagundua ya kwamba hawakuweza kutambua kwa ukamilifu kile ambacho walikuwa wanakwenda kukabiliana nacho.

Maandalizi mema na baadaye kuwasindikiza baada ya kufunga ndoa,

Kadiri ya maandalizi yatakavyokuwa ya kina na kwa muda mrefu, Papa Francisko anaeleza, ndivyo wachumba vijana wanataweza kujifunza na kujibu neema na nguvu ya Mungu kwa kukomaa ili kuweza kukabiliana na vipindi vya matatizo ambayo haviwezi kamwe kukosekana hata mizigo mizoto ya kuelemewa katika maisha ya wanandoa na familia. Lakini hata hivyo hiyo haitoshi kwa maana inahitaji kitu zaidi ambacho ni shughuli ya kichungaji.

Udhati wa shughuli za kichungaji, unatimilizika, mahali pale wanaposindikiza. Siyo tu mara baada ya maadhimisho ya kufunga ndoa baba Mtakatifu anasisitiza, bali ni kuwasindikia angalau hata miaka ya kwanza ya kuanza familia mpya. Wakati wa mazungumzo na wanandoa, binafsi na hata kipindi cha kukaa katika kujumuiya. Hiyo ndiyo namna ya kuwasindikiza vijana na kuwapa zana na msaada wa kuweza kuishi wito wao; na hiyo inawezekana  kutimizwa tu, kwa njia ya michakato katika kukua kwa imani ya wanandoa wenyewe.

Hali za vipeo na michakato ya kubatilisha ndoa

Kwa mtazamo wa wanandoa wambao wanafanya uzoefu wa matatizo katika mahusiano yao na wanajikuta katika kipeo, Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kusema, inahitaji kuwasaidia waishi imani na kugundua neema ya Sakramenti kwa upya; katika kesi nyingine  ni kutathimini kwa dhati na unyeti wa mienendo yao na uhuru wao wa kuunda familia pia , kuwaelekeza njia gani ya kuchukua, hasa katika mchakato wa ubatilishwaji. Kwa wale ambao wameweza kugundua kuwa, tendo la muungano wao, halikuwa ni sakramenti ya kweli ya ndoa na wanataka kuondokana na hali hiyo, wanaweza kwenda kwa Askofu, mapadre na kwa wahudumu wa kichungaji kwa wajili ya ulazima wa kuwasaidia,wajielezea na si kama kutoa taarifa ya kanuni za kisheria, bali hawali ya yote ni ile tabia ya kusikiliza kwa makini na uelewa.

Katika suala hili la sheria juu ya mchakato mpya wa ndoa Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa, ni chombo  halali, ambacho kinahitaji kutumiwa kwa usahihi na kuchaguliwa na wote, katika kila ngazi ya Kanisa, kwa maana ya kuwa na sababu yake kuu ambayo ni salus animarum! yaani ( kwa ajili ya wokovu wa roho) Baba Mtakatifu anongeza kusema, “nimepata furaha ya kujua kwamba maaskofu wengi na Wasaidizi wa  mahakama walivyokuwa tayari kupokea na kutekeleza mchakato mpya wa ndoa, ili kufariji amani ya dhamiri, hasa masikini na walio mbali na jumuiya zetu za Kanisa”.

Mapokezi ya wale ambao wanaamua kuishi bila kufunga ndoa.

Akikimbuka wokovu wa roho milele, Baba Mtakatifu hatimaye, ni magemeo yake kuw,a upeo wa huduma ya kichungaji wa familia kijimbo unaweza kuwa mpana zaidi hasa katika kuchukua mtindo wake wa  Injili, ili “kukutana na kukaribisha hata wale  vijana wanaochagua kuishi pamoja bila kufunga ndoa”. Kwa sababu, anahitimisha ni “lazima kuwahubiria uzuri wa ndoa”.

28 September 2018, 09:15