Cerca

Vatican News
Mwezi Oktoba ni mwezi wa Kusali Rosari Mwezi Oktoba ni mwezi wa Kusali Rosari  (©darval - stock.adobe.com)

Papa:Salini Rosari mwezi Oktoba ili kuomba neema dhidi ya mabaya

Sala ya Rosari iunganishwe na umoja na kitubio kama watu wa Mungu, kwa kumwomba Mama Maria Mtakatifu Mama wa Mungu na Mtakatifu Malaika Mkuu kulinda Kanisa dhidi ya shetani ambaye daima anataka kututengenisha na Mungu na kati yetu. Ndiyo maombi ya Papa Francisko akiwaalika waumini wote duniani kusali Rosari mwezi Oktoba

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ameamua kuwaalika waamini wota duniani kote kisali Rosari kila siku, wakati wa mwezi mzima wa Oktoba ambao ni wa Mama Maria. Sala hiyo iunganishwe na umoja na kitubio kama watu wa Mungu, kwa kumwomba Mama Maria Mtakatifu Mama wa Mungu  na Mtakatifu Malaika Mkuu kulinda Kanisa dhdi ya shetani ambaye daima anataka kututengenisha na Mungu na kati yetu.

Siku chache kabla ya kuanza Ziara yake ya Kitume katika Nchi za Kibaltiki, Papa Fransisko alikutana na Padre Frederic Forsnos, S. Mjesuit , ambaye ni Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mitandao ya Sala ya dunia kwa ajili ya Papa. Papa Francisko alimwomba kueneneza duniani kote  wito wake kwa waamini  na kuwaalika wanapohitimisha kusali Rosari wakumbuke kusali sala ya kizamani  iitwayo “Sub Tuum Praesidium” yaani tunaukimbilia ulinzi wako, na sala ya Malaika Mkuu Mikaeli ambaye anatulinda na kutusaidia  kupambana dhidi ya ubaya wa shetani mwovu (Uf 12, 7-12).

Hata hivyo Baba Mtakatifu katika misa yake ya asubuhi ya  tarehe 11 Septemba 2018, akitaja  kitabu cha kwanza cha Ayubu alisema, “ sala ni silaha dhidi na Mshitaki  mkuu ambaye anazunguka duniani kote akitafuta jinsi ya kushitaki.” Ni kwa njia ya sala tu, unaweza kumshinda. Watu walioiva katika sala yaani (Mystics) wa Urusi na watakatifu wakuu wa tamaduni zote, walikuwa wakishauri kuwa, wakati wa msongo wa kiroho, ni vema kujilinda chini ya vazi kuu la Mama Mtakatifu wa Mungu kwa kutamka kuomba kwa sala hii “Sub Tuum Praesidium”, yaani “Tunaukimbilia ulinzi wako”.

"Sub Tuum Praesidium" :“Sub tuum praesidium confugimus Sancta Dei Genitrix. Nostras deprecationes ne despicias in necessitatibus, sed a periculis cunctis libera nos semper, Virgo Gloriosa et Benedicta”.

Tunaukimbilia ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, tuokoe siku zote tuingiapo hatarini, Ee Bikira mtukufu mwenye baraka Amina.

Katika sala hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawaomba waamini duniani kusali ili Mama wa Mungu aweze kutuweka chini ya Ulinzi wa vazi lake kuu na kutulinda dhidi ya mashambulizi ya mwovu, mshtakiwa mkuu, na kutufanya wakati huo huo kuwa na utambuzi zaidi wa makosa, manyanyaso na ukiukwaji uliofanywa kwa sasa na  siku za nyuma na kufanya jitihada za  kupambana bila kusita ili uovu husiendelee kuenea.

Kadhalika Papa Francisko ameomba kumalizia sala ya Rosari kwa mwezi mzima wa Oktoba na sala iliyotungwa na Papa Leone XIII isemayo: “Sancte Michael Archangele, defende nos in proelio; contra nequitiam et insidias diaboli esto praesidium. Imperet illi Deus, supplices deprecamur: tuque, Princeps militiae caelestis, Satanam aliosque spiritus malignos, qui ad perditionem animarum pervagantur in mundo, divina virtute, in infernum detrude. Amen”.

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina.

 

 

 

29 September 2018, 15:01