Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na wawakilishi wa Chama cha  Tensho Kenoh Shisetsu Kenshoukai kutoka nchini Japan Papa amekutana na wawakilishi wa Chama cha Tensho Kenoh Shisetsu Kenshoukai kutoka nchini Japan  (Vatican Media)

Papa:Ni matarajio yake Papa kwenda nchini Japan

Papa Francisko ametangaza utashi wa kwenda haraka nchini Japan. Ameyasema hayo bila kuandika, asubuhi ya tarehe 12 Septemba, katika Ukumbi mdogo wa Mwenyeheri Paulo VI alipokutana na baadhi ya wajumbe wa Chama chaTensho Kenoh Shisetsu Kenshoukai cha kutoka nchini Japan

“Kwa kutumia fursa ya ziara yenu, ninataka kuwaambia utashi wangu wa kutembelea Japan mwaka kesho. Ni matumaini ya kuweza kufanya hivyo”. Ametamka maneno hayo Baba Mtakatifu na kutoa mshangao mkubwa, wakati wa salam yake ya mwisho asubuhi ya tarehe 12 Septemba alipokutana katika Ukumbi mdogo wa Mwenyeheri Paulo VI  na baadhi ya wajumbe wa Chama cha"Tensho Kenoh Shisetsu Kenshoukai" cha Japan waliosindikizwa na Padre Renzo De Luca e Shinzo Kawamura.

Kumbukumbu ya safari kwanza ya wajapan 4 barani Ulaya: Papa Francisko amekumbuka kuwa miaka 400 iliyopita yaani kunako mwaka 1585, vijana wanne wa Japan walifika Roma , wakisindikizwa na baadhi ya wamisionari wa Kijesuit, kumtembelea Papa wakati ule alikuwa Gregorio XIII.” Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kikundi cha wawakilishi wa nchi yenu kubwa kufika Ulaya” na kusisitizia juu ya mapokezi makubwa waliyopokea si tu Roma: Watu wa Ulaya walikutana na Wajapan, na wajapan wakakutana  Ulaya na moyo wa Kanisa Katoliki”. Mkutano wa kihistoria kati ya tamaduni mbili kubwa na utumaduni wa kitasaufi, ambao ni haki ya kuhifadhi kumbukumbu, kama vile wafanyavyo chama chao amesema Baba Mtakatifu

Muwe mabalozi wa urafiki na thamani kubwa: Safari ya wawakilishi ha oleo hii ilikuwa ni fupi lakini, Papa amesema: “Ninaimani ya kwamba mnahisi kupokelewa na Papa kama jinsi ilivyo kuwa kwa wale walio watanguliwa  na kwa njia yao onjeni furaha ya mkutano huu na mtiwe moyo wa kurudi katika nchi yenu kama mabalozi wa urafiki na wahamasishaji wa thamani kubwa za kibinadamu na kikristo”.

Dini, utamaduni na uchumi vinaweza kushirikiana: Vijana wale,kwa  miaka 400 iliyopita walikwa na uwezo wa kuunganisha dini utuamaduni na uchumi kwa maana: “ mwingine alikuwa padre, mwingine akashuhudia hadi kifo dini kwa ajili ya imani yake na leo hii ni mwenyeheri”.

Baba Mtakatifu ametia moyo jitihada za chama hicho na zaidi kwa ajili ya kuwezesha mfuko wa mafunzo kwa ajili ya vijana, yatima, na kutoa shukrani hata  kwa michango ya mashirika tofauti. Hayo yote anathibitisha ya kuwa : Ni maonesho ya kwamba dini, utamaduni na dunia ya uchumi vinaweza kushirikiana kwa amani ili kuunda dunia ya ubinadamu zaidi, yenye tabia ya ekolojia fungamani. Na ndiyo hitimisho la Baba Mtakatifu kwamba: “Ni njia ya haki kwa ajili ya wakati endelevu wa nyumba yetu ya pamoja”.

Shughuli ya Chama cha kijapan: Chama cha "Tensho Kenoh Shisetsu Kenshoukai" cha Japan kinahamasisha mipango ya utamaduni na mshikamano, kilichoundwa kwa ajili ya kukumbuka utume wa mara ya kwanza ya  kidiplomasia  nchini Japan Barani Ulaya. Mkutano uliofanikiwa kwa njia ya mapadre wa Kijesuit, wanaoishi katika nchi ya Japan tangu mwaka 1585. Vijana wanne wakristo wa Japan walifika Roma wakisindikizwa na baadhi ya wamisionari wakijesuit ili kukutana na Papa Gergorio XIII, na ilikuwa ni safari maalum iliyodumu zaidi ya miaka 8.

12 September 2018, 14:22