Tafuta

Vatican News
Mwenyeheri Sr. Alfonsa Maria Eppinger aliyetangazwa tarehe 9 Septemba 2018 Mwenyeheri Sr. Alfonsa Maria Eppinger aliyetangazwa tarehe 9 Septemba 2018  

Papa:Mwenyeheri Alifonsa Maria Eppinger ni jasiri na shuhuda!

Papa ameomba kushangilia kwa makofu na salam kwa mwenye heri mpya ambaye ametangazwa tarehe 9 Septemba huko Strasbourg, Alifonsa Maria Eppiner , Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa kike wa Mkombozi Mtakatifu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu ametaja  maadhimisho na baadhi ya mambo yaliyoanzisha kwa ajili ya familia yanayoendelea katika madhabahu ya kimataifa ya Mama Maria huko Loreto, kufuatia  fursa ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Mama Maria ambayo Kanisa linaadhimisha kila ifikapo tarehe 8 Septemba ya kila mwaka.

Aidha ameomba kushangilia kwa makofu na salam kwa mwenye heri mpya ambaye ametangazwa tarehe 9 Septemba huko Strasbourg, Alifonsa Maria Eppiner , Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa kike wa Mkombozi Mtakatifu. Baba Mtakatifu amesema kuwa, alikuwa ni mama jasiri, akiteseka, akisali, akishuhudia upendo wa Mungu na zaidi waliokuwa wagonjwa katika mwili na kiroho.

10 September 2018, 11:24