Tafuta

Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 

Papa:Mwamini aliye na ubatili, uchu na kiburi ni mnafiki!

Papa amesama, waandishi na mafarisayo walitaka kwa ghafla kukandamiza ule uwezo wa Yesu kama Mwalimu kwasababu walisema: Hivi kwanini huyu Mwalimu anawaacha mitume wake bila kutumiza mapokeo ya utamaduni. Lakini Yesu anawajibu kwa kwa ukali na nguvu zote akisema, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki!

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ndugu kaka na dada habari za asubuhi! Katika Dominika ya hiii tujikite kutazama somo la Injili ya Marko. Katika somo la leo (taz. Mk 7,1.814-15.21-23), Yesu anakabiliana na tema muhimu kwetu sisi waamini: udhati wa utii wetu katika Neno la Mungu, dhidi ya kila aina ya ambukizo la malimwengu au mitindo ya kisheria. Simulizi linafunguka likionesha utii ambao waandishi na malisayo wanauliza Yesu, kwa kusingizia mitume wake ya kwamba hawafuati mapokeo ya sheria za kawaida  kwa mujibu wa utamaduni wao. Huo ni utangulizi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyo itoa Dominika tarehe 2 Septemba wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika toka pande za dunia katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

 Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari ya Injili ya siku ya Mtakatifu Marko, anasema: kwa namna hiyo, waandishi na mafarisayo walitaka kwa ghafla kukandamiza ule uwezo wa Yesu kama Mwalimu kwasababuw walisema: “Hivi kwanini huyu Mwalimu ana waacha mitume bila kutumiza mapokeo ya utamaduni”. Lakini Yesu anawajibu kwa nguvu akisema  Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, na kama ilivyo andikwa: Watu hawa huniheshimu kwa midomo ila moyo yao iko mbali nami” (Mk 7, 6-7), Baba Mtakatifu Francisko anaongeza: “Yesu alisema hivyo”. Maneno hayo ni wazi na yenye nguvu!  Ni wanafiki ikiwa na maana ya kusema, neno lenye nguvu na ambalo Yesu analitumia katika Injili na kulitamka akiwaelekea walimu wa dini, yaani  walimu wa sheria  na waandishi… ya kuwa  wao ni “wanafiki”.

Kwa hakika Yesu anataka kutingisha dhamiri ya waandishi na mafalisayo, makosa ambayo yanayojitokeza, je hayo ni makosa gani? Baba Mtakatifu anajibu, ni ile ya hali ya kubadili mapenzi ya Mungu, kwa  kudharau amri zake na ili kufuata utamaduni wa kibinadamu.  Jibu la Yesu ni lenye ukali kutokana na wao kufanya mchezo: hii ina maana ya ukweli wa mahusiano kati ya binadamu na Mungu, udhati wa maisha ya dini. Mnafiki ni muongo na siyo mtu wa dhati, Baba Mtakatifu anabainisha! Hata leo hii Bwana anatualika kuhepuka  hatari ya kutoa zaidi umuhimu wa mitindo ambayo inatoa nafasi ya umbali. Injili inatualika kutambua daima kwa upya kile ambacho ni cha kweli na  chenye kiini katika uzoefu wa imani, yaani upendo wa Mungu na upendo wa jirani, kwa kujitakasa dhidi ya unafiki wa sheria na mapokeo ya ukawaida.

Hata leo hii, ujumbe wa Injili  unaongezwa nguvu pia na sauti ya Mtume Yakobo anaye tueleza kwa ufupi jinsi gani dini ya kweli inapaswa kuwa, ya kwamba; dini iliyo safi isiyo na taka mbele ya Mungu Baba ni hii: kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo na mawaa (Yak 1,27). Kutembelea yatima na wajane , maana yake ni kujikita katika matendo ya upendo kwa jirani kuanzia wale wanaohitaji zaidi, wadhaifu zaidi na waliobaguliwa zaidi. Hawa ndiyo watu ambao Mungu anawatazama kwa namna ya pekee, na kuomba hata sisi tufanye hivyo na zaidi..

“Tujilinde na kutiwa mawaa na dunia hii” Baba Mtakatifu anafafanua: haina  maana ya kujibagua na kujifunga binafsi kutoka katika hali halisi. Hapana, na wala haina maana ya kuwa na mtindo wa kijujuu, bali wa kiundani, kwa maana ya kukesha kwasababu namna yetu ya kufikiri na kutenda, isije kupata mawaa na kuambukizwa na tabia za malimwengu, au ubatili, uchu, na ukiburi. Kwa hakika, mwanaume na mwanamke anayeishi kiubatili, kiuchu na ukiburi, na wakati huohuo anajiamini na kujifanya aonekane kuwa wa dini, hadi kufikia kuhukumu wengine, ni mnafiki!  kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anashauri kutafakari ndani ya dhamiri  binafsi ili  kuona jinsi gani tunapokea Neno la Mungu hasa katika  Siku ya Domenika tunapoudhuria Misa.

Iwapo tunasikiliza kwa namna ya kijujuu au isiyofaa, neno hilo halitasaidia lolote. Tunapaswa badala yake kupokea Neno kwa ajili na moyo ulio wazi  kama vile ardhi nzuri, ili iweze kuzaa matunda katika maisha ya dhati. Yesu anasema kuwa, Neno la Mungu ni kama ngano, ni mbegu ambayo lazima ikue katika matendo yaliyo ya dhati.  Na kama jinsi Neno lenyewe litakasavyo  moyo na matendo, uhusiano wetu na Mungu na watu wengine, kwa maana hiyo  tunaokolewa dhidi ya unafiki. Na kwa mfano na maombezi ya Bikira Maria, atusaidie na kuheshimu Bwana daima kwa moyo, kwa kushuhudia upendo wetu kwa Mungu katika uchaguzi wa dhati kwa ajili ya wema wa ndugu.

03 September 2018, 09:33