Katekesi ya Papa tarehe 12 Septemba 2018 Katekesi ya Papa tarehe 12 Septemba 2018 

Papa: Mtumwa na mbinafsi hana uwezo wa kupenda!

Katika katekesi ya papa Jumatato 12 Septemba, ameendeleza kutafakari Amri ya Tatu ya Mungu: siku ya mapumziko, na kuelezea kwa kina utumwa wa dhambi:Wenye tamaa, wenye shauku, wenye mashaka, wenye hasira, wenye wivu, wenye ujanja, wenye kiburi na mengineyo, hao ni watumwa wa maovu yao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Wapendwa kaka na dada, habari za asubuhi! Katika katekesi ya siku ya leo, tunarudi kwa mara nyingine tena katika Amri ya tatu  inayohusu siku ya kupumzika. Katika Amri kumi za Mungu zilizoko katika Kitabu cha Kutoka, na pia zinarudijirudia katiak Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambapo kuna ufananisho, japokuwa katika Neno hili la Amri ya Tatu ni mahali ambapo linaonesha thamani ya utofauti: Katika kitabu cha Kutoka lengo la kupumzika lilikuwa ni kuonesha baraka ya kazi ya uumbaji  , wakatika katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati  neno hilo lilikuwa ni kufanya  kumbukumbu ya mwisho wa utumwa. Siku hiyo watumwa walilazimika kupumzika kama bwana wao, ili waadhimishe kumbukumbu ya Pasaka ya wokovu”.

 Huo ni mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko, Jumatano 12 Septemba 2018, wakati wa Katekesi yake kwa mahujaji na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtatifu Petro. Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua juu ya Amri ya tatu kuhusu  kupumzika  amesema, watumwa kwa maana kamili hawawezi kupumzika, lakini kuna aina nyingi za utumwa, zile zinazoonekana kwa nje na zile ambazo hazionekani. Kuna malazimisho ya nje kama vile, wanaosongwa; maisha ya waliotekwa nyara kwa nguvu  na aina nyingi zisizo za haki.

Kuna aina nyingi za utumwa: Kuna aina nyingi pia za vifungo vya ndani, kwa mfano kufungwa kisaikolojia, kuwa na mambo mengi, vikwazo vya tabia na mengineyo mengi. Katika hali hiyo je kuna kupumzika? Baba Mtakatifu  anauliza maswali, mtu aliyeko gerezani au anayesongwa anaweza kweli kukaa huru? Je mtu ambaye amegubikwa na matatizo ya kindani anaweza kuwa huru?

Kwa dhati, ndiyo wapo hata watu wanaoishi  gerezani, lakini wakiwa huru ndani ya roho zao. Ametoa mfano wa Mtakatifu Maximillian Maria Kolbe au Kardinali Van Thuan, hawa ni ambao walitambua kubadilisha msongamano wa giza, ukawa mahali pa mwanga. Lakini pia kuna hata watu ambao wanaishi maisha ya udhaifu wa kiroho na wanatambua kupumzika katika huruma, kadhalika hata kutambua kuionesha. Huruma ya Mungu inatoa uhuru. Iwapo unakutana na huruma ya Mungu, unao uhuru mkubwa wa ndani, hata kuwa na uwezo wa kuuonesha kwa nje. Kwa maana hiyo ni muhimu kuwa na uhuru mkubwa wa ndani, hata kuwa na uwezo wa kuuonesha! Na ndiyo maana ni muhimu kujifungulia katika huruma ya Mungu ili kuondokana na kubaki na utumwa ndani mwetu binafsi, amehimiza Baba Mtakatifu Francisko!

Je uhuru wa kweli ni nini? Je unajikita katika uhuru wa kuchagua? Katika kujibu swali hili Papa Francisko anasema, Hiyo ni  hakika kwa maana ni sehemu ya uhuru na tunalazimika kuwa na jitihada ya  kuhakikisha inakuwapo  kwa kila mwanaume na mwanamke  (taz Conc. Ecum. Vat. II, Cost. past. Gaudium et spes, 73).  Lakini ni kutambua vema ya kwamba ili kuweza kufanya kile ambacho tunatamani, haitoshi kuwa huru na  hata mwenye furaha, maana uhuru wa kweli ni mkubwa zaidi ya hilo. Hiyo ni kutokana na kwamba kuna utumwa ambao unafunga zaidi ya kuwa gerezani, zaidi ya kipeo cha kuchanganyikiwa, zaidi ya kulazimishwa na kitu kingine: Huo ni utumwa wa ubinafsi, Baba Mtakatifu anathibitisha. Ni kwa watu wale ambao utafikiri siku zima wameshinda wanajiangalia katika kioo ili kujitazama ubinafsi, na ubinafsi huo una kipimo kirefu zaidi ya mwili wa mtu huyo.

Mimi ni mtumwa wa ubinafsi: Ubinafsi unaweza kuwa mkali na kutesa mtu kila mahali alipo na unaleta msongo wa kina ambao unaitwa dhambi, hiyo si kwa bahati mbaya ukiukwaji wa kanuni, lakini ni kushindwa maisha na kuwa na hali halisi ya utumwa ( taz Yh 8,34). Hatimaye dhambi hiyo ni kusema ubinafsi. Ubinafsi unataka kufanya hilo na hilo… na hakuna kujali kama kuna mpaka, kama kuna amri au kujali kama kuna upendo. Ubinafsi ndiyo dhambi.

Tufikirie ubinafsi kwa mfano katika mapenzi ya kibinadamu: Wenye tamaa, wenye shauku, wenye mashaka, wenye hasira, wenye wivu, wenye ujanja, wenye kiburi na mengineyo… hao ni watumwa wa maovu yao, ambao huwafanyia wao dhuluma na kuwadhuru. Hakuna kikomo kwa wenye tamaa, kwa sababu koo lina unafiki wa tumbo, ambalo limejaa hadi pomoni, wakati huo huo linatufanya tuamini kuwa bado ni tupu. Tumbo la unafiki hutufanya tuwe na tamaa. Sisi ni watumwa wa tumbo la kinafiki. Hakuna kikomo cha wanye tamaa na shauku kwasababu ya kutaka kuishi kwa raha mstarehe: wasiwasi wa milki huharibu, daima wanapenda kurundika pesa na kuumiza wengine; moto wa hasira na mdudu wa wivu huharibu mahusiano; Pamoja na hayo watu wenye wivu…. Waandishi wanasema kuwa, wivu unakufanya ugeuka manjano ya mwili na roho. Kama vile mtu mwenye ugonjwa wa epatites, ambaye hugeuka majano. Wenye wivu wana roho ya manjano kwani hawezi kamwe kupata hewa mwanana kwa afya ya roho. Mwenye wivu uharibu. Baba Mtakatifu anongeza: Mwenye kinyongo ambaye hukwepa jitihada yoyote na humfanya hasiweze kuishi, kwa maana ni ubinafsi ambao amezungumza kwanza,  huyo  hujigamba na kuchimba shimo kati yanafsi yake na wengine

Mtumwa ni yule hasiye na uwezo wa kupenda: Ni yule ambaye hana uwezo wa kupenda! Na maovu yote hayoo , dhambi hzi kama ile ya ubinafsi , inatupeleka mbali na upendo na kutufanya tusiwe na uwezo wa kupenda. Sisi ni watumwa wenyewe binafsi, hatuwezi kupenda kwani upendo daima ni ule wa kuwapenda wengine. Amri ya tatu kwa maana hiyo, inayowaalika kuadhimisha siku ya mapumziko, katika uhuru, kwa ajili yetu wakristo, ni unabii wa Bwana Yesu, ambaye alivunja utumwa wa ndani wa dhambi na kutufanya kuwa watu wa kupenda. Upendo wa kweli ni ule wa uhuru: unaondolea umilki, hujenga mahusiano, unatambua kukaribisha na kumthamini jirani, unabadilisha zawadi ya furaha kwa kila aina ya ugumu na kutufanya kuwa na uwezo wa muungano. Upendo unatufanya kuwa huru hata katika Gereza, hata kama sisi ni wadhaifu na wenye vizingiti.  Huo ndiyo uhuru tunao upokea kutoka kwa Mwokozi Bwana wetu Yesu Kristo. Asante.

12 September 2018, 14:03