Tafuta

Vatican News
Katika ukumbi mdogo wa Papa Paulo VI , Papa amepokea wawakilishi wa mabingwa wa mchezo wa mashindano ya kuendesha pikipiki Katika ukumbi mdogo wa Papa Paulo VI , Papa amepokea wawakilishi wa mabingwa wa mchezo wa mashindano ya kuendesha pikipiki  (Vatican Media)

Papa:michezo inashinda ubinafsi, inaunda urafiki na kuheshimiana

Papa amesema,Matukio ya mchezo kwa dhati yanasisimua na kuwa na usafi wa kujishinda binafsi, dhidi ya ubinafsi; inatoa zoezi la roho ya sadaka, na kama ikifanyika vizuri, kwa hakika inatoa hali halisi ya mahusiano kati ya wengine katika kujenga urafiki na kuheshimu sheria.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumatano tarehe  5 Septemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa mashindano ya kuendesha  Pikipiki ambako amesema, kuwa siku zijazo  wataanza mashindano yao ya kugombea ushindi wa  tuzo iitwayo Octo ya Mtakatifu Marino katika  mwambao wa  Rimini nchini Italia. Amewasalimu kwa upendo, wakuu na wasukani, mafundi  na kuwashukuru kwa matembezi yao. Kadhalika kwa namna ya pekee Rais wa  Kamati ya Olimpiki ya Taifa nchini Italia (CONI) Bwana Giovanni Malagò kwa maneno ya hotuba yake.

Faida za michezo kushinda ubiafsi, kuunda urafiki na kuheshimu sheria

Uwepo wao anaongeza Baba Mtakatifu, unampatia fursa ya kusisitizia juu ya umuhimu wa mchezo hata katika jamii ya sasa. Kanisa linafikiria kuwa  shughuli ya mchezo inajikita katika kuheshimu sheria na zana inayofaa ya elimu hasa hasa kwa vijana wa kizazi, na zaidi isiyoweza kubadilishwa na kingine chochote.  Matukio ya mchezo kwa dhati yanasisimua na kuwa na usafi wa kujishinda binafsi, dhidi ya ubinafsi; inatoa zoezi la roho ya sadaka, na kama ikifanyika vizuri, kwa hakika inatoa hali halisi ya mahusiano kati ya wengine katika kujenga urafiki na kuheshimu sheria.

Mchezo unaunganisha watu na kukuza mazungumzo na makaribisho

Ni muhimu kwa wale wanaojikita katika mchezo, kwa ngazi mbalimbali, kuhamasisha zile thamani za kibinadamu na kikristo ambazo zipo katika msingi wa jamii iliyo na haki zaidi na mshikamano. Huo ndiyo uwezekano kwa sababu tukio la mchezo hujieleza kwa lugha ya ulimwengu, ambayo inatoka juu hadi mipaka, lugha, rangi, dini na itikadi. Hayo yote yanaoneshwa hasa mchezo unapopendwa, kutoka ndani ya moyo. Na zaidi mchezo unao uwezo wa kuunganisha watu na kukuza mazungumzo na makaribisho.

Tangazeni thamani ya mchezo

Baba Mtakatifu anawatia moyo na kuwataka watangaze thamani ya mchezo: kwa kufanya hivyo watachangia kujenga jamii ili ya haki na mshikamano. Kadhalika amesisitizia juu ya maneno mawili ambayo amesema Rais wao. La kwanza kuwa na shauku ya upendo mkuu, kwa sababu anaongeza “ ninapo soma habari za vijana kujua na ni nyingi ! je kumetoke kitu gani pale? Landa kwa upande wake anasema “ninaweza kusema kuwa huyo alikuwa anakosa shauku ya upendo mkuu katika maisha yake , labda kuna ambaye hakuweza kupanda shauku ya upendo mkuu wa kuishi. Na baadaye matatizo hayo yakaondoa ile shauku ya upendo mkuu huo”.

Kuwa bingwa wa maisha na shauku kuu ya upendo

Kwa maana hiyo amesisitiza kwa wanamichezo hao  waambukize kwa hamu kubwa  upendo mkuu kwani dunia hii ina shauku na hamu kuu ya  upendo. Kuishi kwa upendo mkuu na siyo kama nayechukulia maisha kama mzigo mzito. Upendo mkuu ni kwenda mbele. Jambo la Pili Baba Mtakatifu amesema  kwamba: kuwa bingwa wa maisha. “Ndiyo mmoja anaweza kuwa bingwa wa mchezo na kujulikana, bingwa wa kikundi na mengineyo…. Lakini bingwa wa maisha ni yule anayeishi kwa shauku kuu ya upendo na anayeishi kwa ukamilifu anao uwezo wa kuishi hivyo. Kwa maana hiyo shauku wa upendo mkuu na ubingwa wa maisha ni maneno na mawili mazuri! Kwa maneno hayo Baba Mtakatifu amewatakia mema na hata familia zao akiwakumbuka katika sala na kuwabariki na Baraka Takatifu!  

 

 

 

 

05 September 2018, 13:30