Vatican News
Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana amesema, Yesu yuko karibu na mtu na muungano na Baba Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana amesema, Yesu yuko karibu na mtu na muungano na Baba  (ANSA)

Papa:Mbele ya machungu ya ndugu zetu tusibaki bubu na viziwi!

Tujifungulie katika mahitaji ya watu wanaoteseka na tuisiwabauge, kwa kufikiria kuwa ni matatizo, kwa kufanya hivi tunawezakushiriki hata sisi katika maajabu yaliyozungumzwa katika Injili ya Marko. Hayo ni maelezo ya Papa Francisko kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana Jumapili tarehe 9 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tendo la Yesu kuponya kiziwi na kuponya magonjwa yaliyokuwa yanabaguliwa na ambayo yanatuzunguka, ndiyo umekuwa moyo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini na mahujaji  wote waliounganika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican Jumapili tarehe 9 Septemba 2018 wakati wa sala ya Malaika wa Bwana.

Wema hutenda bila kilele

Mtume anaelezea juu ya kiziwi ambaye watu walimpeleka ili Bwana aweze kumwekea mikono yake wakati anatembea akitokea mipaka ya Tiro, na kupita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Deakapoli. Baba Mtakatifu anasema, Jambo moja  ambalo Yesu anatufundisha, katika tendo la kumpeleka mtu faraghani ni kwamba daima mema hutendwa bila kelele au kuonekana. Kwa maana: katika fursa hii, kama hata fursa nyingine, Yesu anatenda daima faraghani. Yeye hapendi kushtua watu, Yeye hatafuti umaarufu au kujulikana, bali anatamani tu kutenda  yaliyo mema  kwa watu. Na kwa tabia hiyo yeye anatufundisha kuwa wema hutendeka bila kujulikana hata bila kilele, bila kupiga tarumbeta. Kwa maana hiyo ni kutunza ukimya.

Yesu yuko karibu na mtu na muungano na Baba

Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya maana ya ishara ambayo Yesu anaitenda kwa binadamu na ishara ambayo inaonesha ukaribu wa binadamu ambao ni umoja na Mungu. Yeye alitia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, “Funguka”.

Ishara hiyo inakumbusha Neno kufanyika mwili. Mwana wa Mungu ni mtu aliyewekwa katika hali halisi ya ubinadamu: alijifanya mtu, kwa namna hiyo ya kuchukua hali ya huruma ya mtu mwingine na kufikia kwa ishara ambayo inaunganisha ubinadamu halisi. Na wakati huo huo, Yesua anataka kutuonesha kuwa miujiza inatokea kwa sababu ya kuwa na muungano wake na Baba: na ndiyo maana anatazama macho yake juu mbinguni.

Mateso siyo tatizo lakini ni fursa

Baba Mtakatifu akisistizia juu ya miujiza iliyotendwa amebainisha kuwa, uponyaji wake yeye ulikuwa ni katika kufungua  wengine na dunia. Na ndiyo maana moyo wa masimulizi haya  unajikita kuunganisha  hata sisi sote  juu ya dharura ya uponywaji mara mbili ambapo Baba Mtakatifu anendelea kufafanua ya kuwa hayo  ni mateso ya kimwili ijapokuwa zipo juhudi za kisayansi, lakini siyo rahisi kufikia moja kwa moja uponyaji  katika upeo huo; labda huo ndiyo uponyaji ulio mgumu zaidi,ambao ni ule wa kuogopa, yaani hofu yetu , ambayo inatoa msukumo wa kubagua aliye mgojwa, kubagua mateso na  mlemavu.

Kuna aina nyingi za kubagua Baba Mtakatifu anaongeza, hata kwa njia ya kutoa vijisadaka au namna ya kuondoa tatizo; inabaki kuwa bubu na kiziwi mbele ya machungu ya watu ambao ni wagonjwa, wenye uchungu na matatizo. Mara nyingi wagonjwa na wanaoteseka wanageuka kuwa tatizo, wakati wanapaswa kuwa fursa ya kujionesha kwao ule  uelewa na mshikamano wa jamii mbele ya walio wadhaifu zaidi.

Tuwe nasi mstari wa mbele wa Efata:

Ni wito wa Baba Mtakatifu, kwamba hata sisi tugeuke  kuwa mstari wa mbele wa Effata, wa miujiza na ufunguzi ambao Yesu anatimiza: Hii inajikita kujifungulia juu ya mahitaji ya ndugu wanaoteseka na wenye kuhitaji msaada, kwa kuhepuka ubinafsi na kujifunga moyo binafsi, Ni moyo wa dhati yaani kiungo cha kina ndani ya moyo ambao Yesu alikuwa akifungua na kutoa uhuru ili wote wawe na uwezo wa kuishi kikamilifu katika mahusiano na Mungu na wengine. Yeye alijifanya mtu, ili mtu ambaye alikuwa ni kiziwi cha dhambi aweze kusikiliza sauti ya Mungu, sauti ya Upendo ambao unaongea katika moyo wake na hivi ajifunze kuzungumza kwa mara nyingine lugha ya upendo na kuitafsiri katika ishara za ukarimu, na kujitoa binafsi.

Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha tafakari lake akisema: Awe Mama Maria ambaye alijifungua kabisa katika upendo wa Bwana kuweza kutusaidia ili nasi tufanye uzoefu kila siku, kwa imani, miujiza ya Efata, ili kuishi na muungano na Mungu na ndugu zetu.

10 September 2018, 11:15