Papa Francisko akihutubia Patrons wa Sanaa za Majumba ya Makubusho Vatican Papa Francisko akihutubia Patrons wa Sanaa za Majumba ya Makubusho Vatican 

Papa kwa Patrons Sanaa ni mahitaji ya dunia na kisima amani!

Baba Mtakatifu amekutana na viongozi Wakuu katika Sanaa wa Makumbusho ya Vatican, wafadhili wa ukarabati wa kazi za sanaa za Makumbusho ya Papa ambao wanaadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa chama chao. Katika hotuba yake, amewaalika “kuzingatia sanaa nzuri, kwani ni mfano wa imani, unaotusaidia kupokea mambo muhimu katika maisha”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

"Sanaa ni ya pili katika maisha  katika kutoa ushahuda kwa Bwana, kwa sababu inatuwezesha kupata imani zaidi ya maneno na mawazo mengi, kwani imani inashirikisha  njia sawa  na ile ya uzuri”. Kwa sababu hiyo, “katika ulimwengu uliojifanya chini ya ubaya wa ubinafsi na mantiki ya madaraka, sanaa inawakilisha” mahitaji ya ulimwengu wote, kwa sababu, ni kisima cha maelewano na amani. Ndiyo hotuba ya Baba Mtakatifu alipokutana na viongozi Wakuu katika Sanaa wa Makumbusho ya Vatican, wafadhili wa ukarabati wa kazi za sanaa za Makumbusho ya Papa ambao wanaadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa chama chao.

Kuendeleza utamaduni wa sanaa kwa karne nyingi

Baba Mtakati akiendelea na hotuba yake anasema,ukarimu wao, “umechangia sana kwa kurejesha vitu vingi vya sanaa vilivyotumiwa katika Makumbusho ya Vatican, na kuendeleza  utamaduni wa wale ambao walioanzisha shughuli hiyo kwa zaidi ya karne nyingi kwa mfano wa picha nyingi za ukutani na kama vile sarcophagi katika catacombs, Makanisa Makuu ya Kirumi na gothic, kazi za Michelangelo, Raphael, Bernini na Canova”.

Sanaa ina imani na sawa na njia pia ya uzuri

Kadhalika Baba Mtakatifu amesema, sanaa, katika historia, ilikuwa ya pili  kwa maisha katika kushuhudia  Bwana. Kwa dhati  ilikuwa, na ni, njia  kuu ambayo inaruhusu kupata imani zaidi ya maneno na mawazo mengi, kwa sababu kwa imani inashirikisha njia sawa na  ile ya uzuri. Ni uzuri,wa sanaa, ambao ni uzuri kwa maisha na kuunda muungano. Papa akiendelea amesema, sanaa huunganisha Mungu, mwanadamu na uumbaji katika muungano mmoja, inaunganisha zamani, sasa na hata  baadaye, na wakati huo huo “huvutia mahali  na inahusisha watu na watu tofauti katika jicho moja, lakini kwa  umbali; kwa maana hiyo Papa amesisitiza kuwa “utume wa Patrons, wa kulinda uzuri ambao ni wema kwa ajili ya binadamu ni muhimu”.

Kuhifadhi uzuri kwa ajili ya wema wa mtu ni muhimu

Baba Mtakatifu akihitimisha amesema, kutafakari ukuu wa sanaa, kielelezo cha imani, ikinasaidia kwa namna ya pekee kutafuta kile tu kinachohesabika katika maisha. Sanaa ya kikristo kwa dhati ndani yake inajiinua yenyewe: inakupeleka katuka upendo wa yule aliyetuumba,katika huruma inayotuokoa, katika Matumaini tunayosubiri. Kwa njia hiyo katika ulimwengu, uliyojaa wasiwasi kwa habati mbaya leo hii, na mgawanyiko, ulioisha uzuri wake kutokana na ubinafsi na dhana ya madaraka, Sanaa inawakilisha, labda bado kuliko zamani, mahitaji ya ulimwengu, na kama ilivyo kisima cha umoja, na amani. Na sanaa hiyo inaelezea ukuu wa bure!

 

28 September 2018, 15:18