Papa Francisko amekutana na maskofu walio udhuria Semina iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu Papa Francisko amekutana na maskofu walio udhuria Semina iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu 

Papa kwa Maaskofu:Mungu kamwe hajawahi kunyamaza,wasiogope!

Kila mmoja wetu, lazima kwa unyenyekevu aingie kwa kina ndani mwake binafsi na kujiuliza, je afanye nini ili uso Mtakatifu wa Kanisa uonekane. Ni sehemu ya hotuba ya Papa Francisko kwa maaskofu waliodhuri semina yao mjini Vatican , ambao amekutana nao tarehe 13 Septemba 2018. Kama wamisionari wasiogopa mbele ya majeraha ya majeruhi ya dhambi

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake, ameomba maaskofu kuwa na umakini kwa ajili ya makelri na waseminari. Amesisitizia hayo kwa  maaskofu karibia 130 aliokutana nao mjini Vatican, tarehe 13 Septemba 2018 ambao kwa siku hizi wameudhuria semina yao iliyo andaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu. Papa Francisko katika mkutano huo ameeleza maneno ya wazi na kuwashauri waweze kusasisha michakato ya uchaguzi, kusindikiza na kutathimini, akikumbusha kuwa utakatifu unajikita katika kugusa mwili wa Mungu.

Katika kufafanua suala la kugusa mwili amesema, Maaskofu kwa wasiwe na aibu ya kugusa mwili wa Makanisa yao na kuingia kwa dhati katika mazungumzo na maswali yao ya ndani. Baba Mtakatifu akisisitizia juu ya maswali na majibu amesema: majibu yetu yatakosa wakati endelevu iwapo hayaweza kufikia  udhati wa kitasaufi na katika kesi kama hiyo, imeweza kutoa kashfa ya udhaifu. Amewashauri wasikae kimya maana hata Mungu kamwe hakuwahi kunyamazishwa na kufanya kana kwamba ndiyo namna ya kuishi.

Kufanya kazi kwa umoja

“Kila mmoja wetu, lazima kwa unyenyekevu aingie kwa kina ndani mwake na kujiuliza, je afanye nini ili  uso Mtakatifu wa Kanisa uonekane” anasema Papa na kuongeza “ haisaidii kunyoshea kidole wengine na kutengeneza kiwanda cha mbuzi wa hupelelezi, badala yake ni  kufanya kazi pamoja na muungano”.  Ni kwenda mbele kwa kuhifadhi moyo wa kondoo, hata kama umezungukwa na mbwa mwitu, wanatambua kuwa watashinda kwasababu wanahesabu msaada wa wachungaji “ na kumweka  Mungu katika kitovu ambacho kinatoa maisha kwa ukamilifu.

Kutawaliwa na vishawishi

Msiache kutawaliwa na vishawishi vya majanga ya maelezo au unabii wa siku za mwisho, kwani kinachohesabiwa ni kuhifadhi na kuzuia ubaridi wa upendo (taz Mt 24,12) na kuendelea kutazama juu kwa Bwana ( tz Lk 21 , 28) kwani Kanisa si la kwetu, ni  la MUngu ! Yeye alikuwa  kabla yetu na atakuwapo hata baada yetu sisi! Hatima ya Kanisa ambalo ni zizi dogo ni la ushindi uliojificha katika msalaba wa Mwana wa Mungu.

Wamisionari wasiogopa mbele ya majeraha ya majeruhi ya dhambi

 “Haina haja ya kutumia nguvu zote kwa ajili ya kuhesabu kile ambacho kimeshindwa na hata kuhamaki kwa hasira” kwa kuruhusu hivyo nafsi yako itapunguza moyo wako na  upeo wako.”Kristo awe ndiye furaha yenu” anasema Papa kwa kuwatia moyo watafute mwanga wake kwa mfano katika familia, mahali ambamo maisha yatunzwa na kulishwa, kuna wema ambao ni msamaha ulio na nguvu ya upatanisho, ni  mahali ambamo wawekwa wakfu wengi kwa ukimya wao wamejitoa binafsi.

Watavumilia kwasababu ya utambuzi ya kwamba, wema mara nyingi haupigi kelele, hauogopi blog na hata habari inayotokea katika ukurasa wa kwanza amesisitiza Baba Mtakatifu!“Msiogope anaongeza, mbele ya majeraha ya mwili wa Kristo, daima kuna majeraha ya dhambi na si mara chache hao ni wana wa Kanisa”.

13 September 2018, 15:38