Cerca

Vatican News
Papa Francisko amekutana na Chama cha kitaifa cha wafanyakazi walemavu (Anmil) Papa Francisko amekutana na Chama cha kitaifa cha wafanyakazi walemavu (Anmil)  (Vatican Media)

Papa kwa ANMIL: Binadamu siyo bidhaa, tangazeni utamaduni mpya

Dunia ifungue macho na kuona watu wadhaifu walioko mbele yetu kuwa siyo bidhaa bali ni binadamu na ndiyo anawashauri kuiga daima ushirikiano na mshikamano katika msimamo thabiti hasa kwa wafanyakazi waathirika wa ajali kazini

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 20 Septemba 2018 mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko  amekutana na Chama cha kitaifa kati ya wafanyakazi ANMIL wenye ulemavu na walemavu waliopata ulemavu kazini. Ameungana na wote wanaosaidia wale wote ambao walipata ulemavu wa viungo au walemavu katika kazi, katika juhudi ya kuhamasisha utamaduni na hata msimamo wa umakini wa afya na usalama.

Watu wangapi wameumia kazini: Katika hotuba yake, Baba mtakatifu amekumbuka “watu wangapi wameumia kazini  na matokeo yake ni walemavu na kuishi hali ambayo kwa namna ya pekee ya mateso na hasa ulemavu ambao unawakosesha wasiweze kuendelea kufanya kazi au kuangaikia familia zao kama walivyo kuwa wakifanya hawali”. Kwa wote hao ameonesha ukaribu wake , na kwamba “ Mungu anafariji anayeteseka, kwa maana Yeye mwenyewe aliteseka na anakuwa karibu na kila aina ya hali na kwa unyenyekevu. Kwa nguvu yake, kila mmoja anaalikwa kujahidi kuwa na mshikamano na kuwasaidia ambao ni waathirika wa  kazini; usaidizi huo uweze kupanuka hadi katika familia ambao wamekumbwa na kuhitaji msaada wa dhati.

Dunia ifungue macho na kuona watu walioko mbele yetu  siyo bidhaa bali ni binadamu: Mafundisho ya Kanisa, Baba Mtakatifu anasema ndiyo anawashauri kuiga daima kwa maana yanawaalika kuwa na msimamo huo kati ya mshikamano na ushirikiano. Na hiyo lazima kuitafuta na kujenga kila wakati na mantiki za kijamii, ili kwa upande mwingine isikosekane na kwa upande mwingine isiwe ni vizingiti vya mazoezi, kwa wale ambao bado wanaweza kuwa muhimu katika kutoa mchango wa Kanisa, bali kujikita kwa ari  katika matendo hai ya kutoa matunda na uwezo wake.

Baba Mtakatifu akiendelea kusifu chama hicho ANMIL kisicho choka kwa ajili ya kutafuta haki za wafanyakaz, kuanzia wale wadhaifu zaidi kama vile walemavu  wa viungo, hata  mara nyingi ni  wanawake, wazee na waliobaguliwa. Dunia yetu anasema Baba Mtakatifu, inahitaji kweli kisikia sauti ya ubinadamu ambao inaweza kuwafanya wafungue macho na kuona  wadhaifu walioko mbele yetu na kwamba  siyo bidhaa, bali ni watu ambao ni  kaka dada wa ubinadamu

Shukrani kwa waziri wa kazi: Baba Mtakatifu pia amepongeza juhudi za kazi ambazo zinajikita katika ushirikiano na taasisi za kiraia  na kwa namna ya pekee Waziri wa Kazi, wa Elimu, Vyuo Vikuu na Utafiti. Anathibitisha ya kuwa wametoa maisha kwa mipango mingi ya mafunzo, hasa yanayotazama wanafunzo ya shule , maabara, wakuu na wahusika wa kamampuni kwa namna ya kuweza kwajibika na kuwa na dhamiri ya mahitaji ya usalama, kutetea na kulinda afya ya wafanyakazi.

Katika mkakati huo umeweza kutoa hatao katika miaka kumi iliyopita Waraka muhimu wa pamoja juu ya usalama na mahali ambapo katika kuutendea kazi, wote wanaalikwa kuulinda. Uangalizi huo wa kina kwa mantiki ya kisheria, zaidi juhudi ya mshikamano, Baba Mtakatifu amesema, inaonesha kwa upande wao kuwa na utambuzi wa kuunda utumaduni mpya wa kazi ambao hauwezi kufanya kidogo labda kama hakuna mswada wa sheria unaostahili na mabao unatoa jibu halisi ya mahitaji ya wafanyakazi na zaidi kwa kina katika utambuzi wa dhamiri ya kijamii juu ya matatizo ya kulinda afya na usalama na  kwamba bila sheria hiyo  zitabaki waraka uliyokufa

Kwa hayo  yote anawasifu Papa Francisko kwamba  ni mapamba  ambayo wamepeleka mbele kwa miaka 75 ya juhudi. Na uamuzi ambao hauhusishi tu wale ambao wameathiriwa kazini au kufanya kazi za hatari na  za uchovu, bali kila mzalendo, kwa sababu pamoja na utamaduni wa kazi na usalama, vipo katika mchezo wa hali halisi yenyewe ya demokrasia ambayo inajumuisha heshima na ulinzi wa maisha ya kila mmoja.

20 September 2018, 15:09