Cerca

Vatican News
Watawa wa wa Shirikisho la Wabenediktini Kimataifa wakutana na Papa Francisko Watawa wa wa Shirikisho la Wabenediktini Kimataifa wakutana na Papa Francisko  (Vatican Media)

Papa:Kupokea,sala kwa wanaoteseka, njaa, vita na wasio na haki

Leo hii katika dunia wapo watu wanaotafuta kuishi kwa ukarimu, upendo, huruma na makaribisho ya Yesu katika maisha yao. Papa amenena hayo tarehe 8 Septemba alipokutana na wawakilishi wa Mkutano wa Shirikisho la Kimataifa la watawa Wabenedikitino mjini Vatican. Amewshukuru kwa kjuhudu yao ya kukaribisha na utunzaji bora wa mazingira

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Padre Abate Mkuu, Sista Judith Ann, na wamonaki na Watawa wa Benediktini, ninawakaribisheni Roma! Ninamshukuru Padre Mkuu kwa maneno ya utangulizi wake: nimemwambia kuwa amejitahidi katika lugha ya kiitalino! Mkutano wenu Mkuu ni fura mwafaka kwa Wabenedikiti wa dunia nzima ili kuishi kipindi cha sala na kutafakri juu ya mambo mbali mbali ambayo Tasaufi ya Mtakatifu Benedikto hasa baada ya miaka mia tano kuona inaendelea kupiga kengere na kutenda kazi leo hii. "Niko karibu nanyi kiroho, katika siku hizi za mkutano wenu”.

Huo ni utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 8 Septemba 2018, alikutana na wawakilishi wa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho  la Wabenediktino mjini Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba hiyo amesema, kama walivyo chagua tema ambayo ni wosia wa kutoka katika Sura ya 53 ya Mwongozo wa Mtakatifu Benedikto, isemayo: Ili wote wakaribishwe kwama Kristo”. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, hiyo ni kielelezo kilicho chukuliwa na Shirika la Wabenediktini, katika mtindo wa wito wa kukaribisha, katika utii wa kufuata Neno la Bwana Yesu ambaye anakuwa sehemu fungamani ya kanuni yake na mwenendo” ambao umetolea katika Injili ya Matayo kwamba: “ Nilikuwa mgeni, mkanipokea “ ( Mt 25, 35 ; na katika wosia wa Kitume wa Gautede et exsultate , 102-103) yaani Furahini na shangilieni.

Tasaufi ya kibenediktini ni makaribisho, sala na ukarimu

Leo hii katika dunia wapo watu wanao tafuta kuishi kwa ukarimu, upendo, huruma na makaribisho ya Yesu katika maisha yao. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, kwa upande wao, wanatoa tunu ya thamani katika ushuhuda wao hasa wanapokuwa vyombo vya ukarimu wa Mungu kwa wale ambao wanahitaji. Makaribisho yao kwa watu tofauti ya utamaduni wa dini, yanachangia kupeleka mbele ule upako wa tasaufi ya kiekumene na mazungmzo ya kidini. Kwa karne nyingi maeneo ya kibenediktini yanajulikana kama maeneo ya makaribisho, maombi na ukarimu wa kupokea. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisisko anawatakia matashi mema ya kuwa, kwa kutafakari kwa pamoja tema hiyo na kushirikishana uzoefu, wanaweza kweli kutafuta na kutoa mitindo mbalimbali ambayo iwafanye waendelee, katika monasteri zao, shughuli yao ya lazima ya kiinjili.

Ora et Labora:

Nembo yao “Ora et labora” yaani kazi na sala, Baba Mtakatifu anabaisha kuwa inajikita katika sala kuwa kitovu cha maisha yao. Maadhimisho ya Misa Takatifu yao na masifu ya kila siku, inawaweka katika moyo wa maisha ya Kanisa. Kila siku, katika maombi yao, yanatajirisha kwa namna ya kusema mvuto wa Kanisa. Ni sala ya kusifu, ambayo wao wanatoa sauti ya ubinadamu wote hata kwa Mungu. Ni sala ya kushukuru kwa mambo mengi, hata mengi ambayo Bwana anaendelea kutoa. Ni sala ya kuomba kwa ajili ya mateso na mahangaiko ya wanaume na wanawake wa nyakati zetu, hasa maskini. Ni sala ya kuomba kwa wale kwanaoteseka na ukosefu wa haki, vita, vurugu, nguvu na wanaona kila siku kwa ukiukwaji wa haki zao. Wote hao wanakutana nao moja kwa moja, lakini pia ni dada katika imani na Mwili wa Kristo. Thamani ya maombi yao, haiwezi kuhesbaiwa, lakini kwa hakika ni zawadi kubwa na tunu msingi. Mungu anasikiliza daima wenye moyo wa unyenyekevu na kujaa upenod.

Shukrani kwa utunzaji wa mazingira zawadi ya Mungu:

 “Ninasema asante kwa namna ya pekee katika utunzaji na huduma ya mazingira mliyo nayo na kwa ajili ya juhudi ya kuhifadhi zawadi ya ardhi, kwasa sababu iweze kushirikishwa na wote”. Baba Mtakatifu ameongeza, ninatambua kuwa, wamonaki na watawa wa kibenediktini duniani ni makini hasa katika shughuli za kutunza zawadi ya Mungu. Kama wanawake, anasema “hisi kwa namna ya kupongezwa uzuri na umoja wa uumbaji. Katika Monasteri zao, daima kunapatikana maeneo makubwa na mazuri, mahali ambapo watu wanakwenda kusali na kupata faraja katika ukimya,wakati wa kutafakari maajabu ya uumbaji. Anawatia moyo wa kuendelea na mtindo huo na kutoa huduma hiyo ili kazi ya Mungu iweze kutoa mshangao na kufanya watu waongee juu yake.

Maisha ya kijumuiya ni ushuhuda: 

Baba Mtakatifu akusendelea amethibitisha kwamba maisha yao ya jumuiya ni kushuhudia umhimu wa upendo na kuheshimiana. Kwa dhati wao wanatoka katika maeneo na uzoefu tofauti, wao pia ni tofauti kati yao, kwa maana hiyo wanapokeana wao kwa wao, ambayo ndiyo ishara ya wanayo itoa katika dunia ambayo inashindwa kuishi thamani hiyo. Sisi sote ni wana wa Mungu na sala zao, Kazi zao, mapkezi yao, ukarimu wao, unajikita katika kuonesha umoja katika utofauti ambao unajieleza matumaini ya Mungu katika dunia: umoja ambao unatengenezwa na amni, mapokezi ya pamoja na upendo kidugu.

Baba Mtakatifu amehitimisha hotuba yake, akiwawakikishia kuwasinidkiza kwa sala. Wao wanapeleka zawadi yenye thamani katika maisha ya Kanisa kwa ushuhuda wa wema wa kike, imani na ukarimu, kuiga mfano wa Mtakakati Mama wa kanisa Bikira Maria. Wao ni Picha ya Kanisa na ya Mama Maria: wasisahau amehimiza Papa. Picha: Anaye tazama wao atazame Kanisa Mama, na Mama Maria Mama wa Kristo. Kwa njia hiyo amehitimisha akisema, tumsfu Bwana na amewashukuru, amewabariki wote, jumuiya za ona wote ambao wanawahudumia kwa jina la Kristo na kuowaomba wasali kwa ajili yake pia.

08 September 2018, 13:18