Tafuta

Vatican News
Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video kwa washiriki wa Mkutano wa 5 wa wakatoliki kutoka Hispania huko Marekani Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video kwa washiriki wa Mkutano wa 5 wa wakatoliki kutoka Hispania huko Marekani 

Papa:Kukutana kwa tamaduni ni ishara ya matumaini!

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya video wa washiriki wa Mkutano wa tano wa kitaifa kwa wakristo kutoka Uhispania wanaoishi nchini Marekani na kusema kuwa: “kwa njia ya mkutano huu wa tano ninyi mnatafuta kuunda utamaduni wa makutano ambao unatoa matumaini ya kukutana”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tamaduni nyingi na jinsi ya kuishi, kufikiria na kukutana na kutambua kwa matumaini. Ninyi mmeweza kujikita katika kutoa mapendekezo ya kufikia mtindo tofauti wa namna ya kuwa, pia kuwa na mahusianao ambayo yanatia moyo wa kila mtu na kila kikundi katika kushirikishana utajiri wa tamaduni binafsi, utajiri wa uzoefu binafsi na ili kuangusha kuta kwa kujenga madaraja. Ndiyo msisitizo uliopo katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa kitaifa wa wakatoliki uliofunguliwa tarehe 21 Septemba 2018.

Katika mkutano wa kitaifa wa wakatoliki kutoka nchi ya Uhispania, wanaoishi Marekani ambao unatarajiwa kufungwa tarehe 23 Septemba huko Grapevine, mjini Texas, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, anaona mkutano huo wa tano kama mtindo wa dhati wa Kanisa la Marekani katika kujibu changamoto za kuondokana na kila aina ya kuishi maisha ya raha tu na kukimbilia katika  kutafuta mizizi na kubadilika kama chachu katika umoja wa wote ambao wanatafuta wakati ujao wa matumaini, hasa vijana na familia nyingi zinazoishi katika pembezoni mwa jamii.

Kutoa nguvu wahamiaji wengi

Kadhalika anathibitisha jinis gani anajua mchakato huo wa mkutanomwa tano ulivyo watia nguvu wahamiaji wengi wanaoishi katika hali ya hofu na ukosefu wa msimamo. “Mkutano huo unatoa kwa namna ya pekee maana ya jumuia, urafiki na msaada. Pia ni chambomcha neema ambacho kinatoa uongofu wa mioyo ya watu wengi na zaidi katika uongofu wa hali ya kichungaji na uongofu wa masuala ya uchungaji katika Makanisa maalumu, kwa njia ya mikutano na kwa maana ya kuabudu Yesu Kristo”. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa njia ya video pia anasema kuwa, anao utambuzi wa mchango mkubwa wanao utoa jumuiya kihispainia kwa maisha ya taifa na anasli ili mkutano wa tano u endelekutoa mchango wa upyaisho wa jamii na utume  wa Kanisa la Mrekani .

Mkutano wa wakatoliki wa Uhispania huko Marekani

Mkutano unaofanyika huko Grapevine mjini Texas unajikita katika mada ya Mitume wamisionaii : ushuhuda wa Mungu”. Lengo kuu msingi katika mkutano  huo ni ule wa kutafuta maang’amuzi  ya Kanisa la Marekani katika kujibu uwepo wa wageni kutoka nchi ya Uhispania na Amerika ya Kusini. Kipaumbele kingine ni kile cha kuongeza nguvu kwa wale wote wanaohusika katika maisha ya Kanisa kama mitume wa kimisionari. Wakati wa maandalizi na kabla ya kufungua mkutano huo,zaidi ya maparokia 5,000 wameshiriki mchakato wa katiba ya pamoja na maelfu ya maparokia kutoka Bara zima la Amerika ya kusini ambao wanatoka katika tamaduni na mataifa tofauti.

21 September 2018, 14:04