Tafuta

Vatican News
Katika vijiji vya Afrika ipo shida ya  ukame , umaskini na maji Katika vijiji vya Afrika ipo shida ya ukame , umaskini na maji 

Papa:kuheshimu maji, tunu msingi na haki ya hupatikanaji wake!

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe Mosi Septemba 2018 wakati wa kuadhimisha mwaka IV wa Siku ya kuombea huduma ya viumbe duniani, iliyo anzishwa na yeye tangu mwaka 2015, ametoa ujumbe wake kwamba, ni lazima kutambua ya kwamba hatukujua kulinda kazi ya uumbaji kwa uwajibikaji

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu kaka na dada, katika Siku ya Maombi ninayo shauku, awali ya yote kumshukuru Bwana kwa zawadi ya nyumba yetu ya pamoja, na kwa ajili ya watu wenye mapenzi mema, wanao jikita kuilinda. Ninao utambuzi wa mipango mingi iliyo anzishwa ya  kuhamasisha mafunzo na kulinda mkakati ya ecolojia, ili kuongeza nguvu ya mwelekeo wa maendeleo ya kilimo endelevu na  kuongezeka zaidi uwajibikaji, hasa kwa kuanzisha aina mbalimbali za mafunzo ya elimu, kiroho na kiliturujia, ambayo inajihusisha na utunzaji wa viumbe kwa wakristo wote duniani.

Huo ni utangulizi wa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko, alioutoa tarehe 1 Septemba 2018, wakati wa kuadhimisha mwaka IV wa Siku ya kuombea huduma ya viumbe duniani, iliyo anzishwa na yeye tangu mwaka 2015. Ni Katika siku hii ya maombi ya huduma ya viumbe inaongozwa na mada ya  maji kwa maana ya mantiki mbili: kuheshimu maji, kama jambo msingi na upatikanaji wa maji kama haki ya binadamu.

Kuwa na utambuzi

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ujumbe wake, anasisitiza kuwa ni lazima kutambua  kwamba hatukujua kulinda kazi ya uumbaji na uwajibikaji. Hali ya mazingira kwa ngazi ya dunia, na kama ilivyo katika sehemu nyingine maalum, haiwezi kufikiriwa kuwa inaridhisha. Kuna sababu na ulazima wa kupyaisha ule uhusiano ulio  msafi kati ya binadamu na huduma ya viumbe , kutokana na kukiri kwamba katika maono ya binadamu yaliyo ya dhati na fungamani, inawezekana kuruhusu kutunza vema sayari yetu kwa ajili ya wema kwa  wakati wa sasa, hata kwa kizazi kijacho, kwasababu hakuna, “ekolojia bila elimu ya kutosha ya binadamu (soma : Waraka wa kitume Laudato si 118)

Majini ni jambo msingi , ni tunu

Katika Siku hii ya Maombi ya dunia kwa ajili ya huduma ya viumbe, ambayo Kanisa Katoliki kwa miaka kadhaa linaadhimisha kwa muungano na ndugu, kaka na dada wa Kiorthodox, na kuungwa mkono na makanisa mengine, na Jumuiya za Kikristo, baba Mtakatifu anaongeza: ninatamani kutoa wito  kwa umakini juu ya suala la maji,  jambo rahisi sana na tunu  ambayo kwa bahati mbaya inatokea kuwa wengine walio wengi hawana uwezo wa kupata. Wakati huo huo uwezekano wa maji safi na salama ni haki ya binadamu na msingi, na katika dunia kwasababu inajieleza namna ya watu kuishi, kwa maana hiyo inashurutisha kujikita katika hali kwa ajili ya zoezi  la haki nyingine za kibinadamu. Dunia hii ina deni kubwa sana la kijamii dhidi ya maskini ambao hawana uwezo wa kupata maji ya kunywa , kwa maana hiyo ni kukataa haki yake ya maisha yaliyosimika mzizi katika hadhi yao ( Laudato Si' , 30)

Maji yanatoa mwaliko wa kutafakari asili yetu

Suala la maji linatoa mwaliko wa kutafakari asili yetu. Katika mwili wa binadamu sehemu kubwa ni maji: na ustaarabu mwingi katika historia imechimbuka katribu na  mtiririko wa maji na ambayo yametoa utambulisho.  hiyo pia inathibitishwa katika mwanga , mfano uliotolewa katika Kitabu cha Mwanzo, ambapo tunasoma kumba asili ya Roho ya MUNGU  ilikuwa ikitanda juu ya maji  (Mw 1,2)

Baba Mtakatifu akiendelea na ujumbe wake anasema, akifikiria msingi wa ardhi ya Muumba na katika maendeleo ya binadamu, anahisi ulazima kumshukuru Mungu kwaajili ya “dada maji” rahisi, na ya lazima ambapo hakuna lolote laweza kukidhi  maisha katika sayari hii. Kwa namna hiyo kutunza vyanzo na  visima vya maji ni dharura kubwa. Leo hii na zaidi unahitaji mtazamo ambao unakwenda zaidi ya upeo  na kwa haraka ( taz laudato si, 36) mbali na hayo, ipo hata mantiki ya matumizi ya kutosha na uzalishaji wa faida binafsi ( taz, Laudato 159). Hata hivyo kuna haja ya mipango ya kushirikishana na ishara za dhati , ambazo zizingatie kuwa kila ubinafsishaji wa wema wa asili  ambao binadamu hawezi kugusa, haukubaliki, Baba Mtakatifu ameonya!

Kwa wakristo maji ni kilelezo msigi za utakaso na maisha

Kwa wakristo, Baba Mtakatifu anathibitisha, maji yanawakilisha kielelezo msingi cha utakaso na maisha. Wazo kuu linakwenda katika Ubatizo ambao ni sakramenti ya kuzaliwa kwetu upya. Maji yaliyotakaswa kwa Roho ni kitu ambacho Mungu amefanya tuishi na kupyaishwa; ni kisima kilichobarikiwa na maisha ambayo hayafi tena. Ubatizo unawakilisha hata kwa upande wa wakristo wa imani nyingine, sehemu ya kweli ya kuanzia na ambayo haiwezekani kukataliwa kwa ajili ya kuishi udugu, daima ulio wa kweli katika mchakato wa safari ya kulekea umoja. Katika kipindi cha utume wa Yesu, alitoa ahadi ya maji kuwa yatamwondolea mwanadamukiu daima , (Yh 4,14) na alitabiri: “ Aliye na kiu na aje kwangu anywe” (Yh 7,37). Kwa maana hiyo,  kwenda kwa Yesu, na kunywa kwake ,maana yake ni kukutana naye binafsi kama Bwana na kuchota Neno lake kwa maana ya maisha, anathibitisha Baba Mtakatifu. Maneno aliyotamka Yesu juu ya msalaba “ Naona kiu", (Yh 19,28)  anaongeza,  yatoe mtingisho kwetu. Bwana anaomba kwa mara nyingine  tena kuwa, bado anayo kiu, ni kiu ya upendo. Anatuambia tuwapatie maji wengi ambao wana  kiu leo hii, na kutuambia baadaye: “Nilikuwa na kiu na mkanipatia maji ya kunywa” Mt 25,35). Kuwapa maji ya kunywa katika kijiji cha ulimwengu siyo ishara tu binafsi ya upendo, bali ni uchaguzi wa dhati na wajibu unaoendelea ili kuhakikisha kuwa wote wanapata wema msingi wa maji.

Shukrani kwa Mungu kwa ajili ya Bahari na visiwa

Kadhalika Baba Mtakatifu amependa kugusia juu ya suala ya bahari na visiwa. Ni wajibu wa kumshukuru Muumba kwa ajili ya kazi yake kubwa na zawadi ya maajabu ya maji mengi na kile kilichomo ( Mw 1,20-21: zab 146,6) na kumshukuru  kwa ajili alivyoipamba ardhi kwa visiwa (taz. Zab 104,6). Baba Mtakatifu Francisko ameomba kuelekeza mawazo yetu katika  bahari zilizo tanda na katika mwendelezo wa kuzunguka, na kwamba  unawakilisha kwa maana nyingine hata fursa ya kumfikiria Mungu ambaye daima anasindikiza kazi yake ya uumbaji na kuifanya iendelee mbele, kwa kuhifadhi uwepo wake (Katekesi ya Mtakatifu Yohane Paulo II 7 Mei 1986)

Changamoto za kuhifadhi

Kutunza kila siku wema huo usio kuwa na kifani, unawakilisaha leo hii uwajibikaji , ukweli na changamoto: Hii inahitaji ushirikiano kati ya watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya kushirikishana katika kazi inayondelea ya Muumba. Juhudi nyingi, Baba Mtakatifu anabainisha: kwa bahati mbaya zinashia ukingoni kutokana na kukiuka  sheria na kukabiliana na matokea hasa kwa mtazamo wa ulinzi wa maeneo ya bahari, mbali na mipaka ya mataifa (taz, laudato si’, 174). Hatuwezi kuruhusu Bahari na visiwa vikajaa kwa kiasi kikubwa plastiki zinazoelea. Kwa maana hiyo  dharura, Baba Mtakatifu anasisitiza, wote tunaalikwa kuwajibika  na kuwa na ubunifu kiakili , kwa maana ya kuomba kama vile yote yanatokana na Mungu na kufanya kazi kama vile inategemea na sisi.

Maombi ya Baba Mtakatifu

Tusali ili maji yasiwe chanzo cha utengeno kati ya mataifa, bali makutano kwa ajili ya jumuiya ya binadamu. Tusali ili kuwepo na uangalizi wa yule aliye katika hatari ya maisha yake kufunikwa na dhoruba kali  akitafuta wakati endelevu. Tumwombe Bwana kwa wale ambao wanatoa huduma ya kisiasa ambayo ni masuala nyeti zaidi  katika  nyakati zetu, kama yale yanayojihusisha na uhamiaji, mabadiliko ya tabia nchi, haki kwa ajili ya wema wa mambo msingi, vyote viweze kukabiliwa kwa uwajibikaji, kutazama mipango ya kudumu ya wakati endelevu, kwa ukarimu na roho ya kushirikiana, zaidi kati ya Nchi ambazo sehemu kubwa wako tayari.

Tusali kwa ajili ya wale wanaojikita katika utume baharini, kwa wale wanaosaidia kutafakari juu ya matatizo ambayo yanakumba mfumo mzima wa maji, kwa ajili ya wanaotoa mchango kufanya kazi, na utungaji wa sheria za kimataifa zinazohusu maji;  na kwamba zinaweza kuwalinda watu; kwa ajili ya nchi, mali, rasilimali asili,  kwa mfano, anafikiri uoto wa mimea  yote ardhini,  hata iliyoko majini au wanyama baharini , ili kuhakikisha maendeleo fungamani katika mantiki ya kufanya kazi kwa ajili ya kulinda sehemu zote za bahari na kulinda visiwa vyote na uoto wake wote, ili zoezi hili lifanyike kwa ufasaha na kwa ukarimu.

Hatimaye ujumbe wa Baba Mtakatifu unawalekea vijana:

Kizazi cha vijana kipo rohoni , Baba Mtakatifu anathibitisha,na kwamba kwa ajili yao, tusali ili waweze kukua na utambuzi,  kwa kuheshimu nyumba ya pamoja, wakiwa wanafikiria kutunza wema msingi wa maji kwa faida ya wote. Ni matarajio ya Baba Mtakatifu kwa ajili ya Jumuiya nzima ya kikristo kutoa mchango mkubwa zaidi na daima wa dhati, ili wote waweza kweli kujinufaisha katika rasilimali msingi, kulinda kwa heshima kubwa zawadi iliyotolewa na Muumba, kwa namna ya pekee, maji yanayotitiririka, ya bahari na visiwa.

01 September 2018, 13:45