Tafuta

Papa Francisko amechagua kauli mbiu itakayoongoza Siku ya Mawasiliano duniani 2019 Papa Francisko amechagua kauli mbiu itakayoongoza Siku ya Mawasiliano duniani 2019 

Papa:Kauli mbiu ya Siku ya Mawasiliano dunianiani 2019!

Tarehe 29 Septemba, Vyombo vya Habari Vatican wametoa kauli mbiu iliyochaguliwa na Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Mawasiliano duniani 2019, ambayo itaongozwa na maneno ya Mtakatifu Paulo kwa Waefeso “kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine (Ef 4,25). Kutoka katika jamii hadi Jumuiya”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine (Ef 4,25). Kutoka kwa jamii hadi  katika Jumuiya”. Ndiyo kauli mbiu ambayo Papa Francisko ameichagua kuongoza Siku ya Mawasiliano duniani kwa 2019. Kauli mbiu hiyo imetangazwa rasmi na Vyombo vya habari Vatican kwa njia ya msemaji mkuu wa Vatican kwa waandishi wa habari. Akifafanua amesema kauli hiyo, “inasisitiza umuhimu wa kurudisha mawasiliano kwa mtazamo mpana, na inajikita katika msingi wa mtu na kusisitiza thamani ya mwingiliano unaolenga daima mazungumzo na kama fursa ya kukutana na mwingine”.

Kutafakari hali halisi ya asili ya mahusiano katika vyombo vya habari vya kijamii

Katika kauli mbiu hiyo “inahitaji kutafakari juu ya hali ya sasa na asili ya mahusiano ya mtandao ili kuanza na wazo la jumuiya kama mtandao kati ya watu katika ukamilifu wao wa mawasiliano”. Taarifa inaendelea kueleza kuwa,“Baadhi ya mwenendo “unaoenea kwenye mtandao unaojulikana kijamii, ki ukweli, huuliza swali la msingi: Je kwa kiwango gani tunaweza kusema kuhusu jamii halisi katika uso wa mantiki ambayo inahusika na baadhi ya jamuiya katika mitandao ya kijamii? Kielelezo cha mtandao kama jumuiya ya mshikamano inamaanisha ujenzi wa sisi, unaosimamia msingi juu ya  kusikiliza mwingine, juu ya mazungumzo na matokeo yake, juu ya matumizi ya kiuwajibikaji katika ufanisi wa lugha”.

Inteneti ni mtandao wa watu, si mtandao wa waya

Katika Ujumbe wa Siku ya Mawasiliano duniani 2014, Papa Fransisko alikuwa tayari  amebainisha na kutoa wito juu ya mtandao ya kwamba, “ intenet iwe ni mahali penye utajiri wa ubinadamu na  sio mtandao wa nyuzi lakini wa watu”. Uchaguzi wa kauli mbiu ya Ujumbe wa 2019, unathibitishwa kwa thati,  “ umakini wa Papa Fransisko  kwa mazingira mapya ya mawasiliano na hasa, kwa Mitandao ya kijamii ambako Papa binafsi yupo mstari wa mbele kwa akaunti ya @Pontifex kwenye Twitter na  wasifu @Franciscus katika Instagram”.

29 September 2018, 15:16