Papa Francisko na  wafanyakazi Papa Francisko na wafanyakazi 

Papa kwa il Sole 24 Ore: Fedha za kweli zinatengenezwa kwa kazi!

Kufanya kazi kwa ajili ya faida tu, haitoa maana ya maisha ya kampuni: inahitajika mafunzo yenye thamani na maadili rafiki ya binadamu. Hayo ni mawazo ya Papa Francisko katika mahojiano leo hii katika gazeti la kila siku la Italia mahali ambapo amezungumzia juu ya uchumi ambapo anasema unaua kwa sababu binadamu si kiini tena cha maisha yake!

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Suala la uchumi na fedha , uundaji nafasi mpya za ajira, kuheshimu mazingira, kupokea wakimbizi ambao wanapita wote katika maadili rafiki ya binadamu, “uamsho wa nguvu” kwa ajili ya uongofu  “ambao tunahitaji”. Hiyo ni tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko , katika mahojiano na gazeti la kila siku la Italia liitwalo “il Sole 24 Ore mahojiano ambayo yametolewa tarehe 7 Septemba 2018.

Inakosekana dhamiri ya asili ya pamoja na ukosefu kuwepo katika mzizi wa pamoja wa kibinadamu na wa wakati endelevu wa kujenga pamoja. Utambuzi huo wa msingi unawezesha maendeleo mapya ya kuamini, tabia mpya na mitindo ya maisha. Maadili rafiki ya binadamu yanataka kushinda ule utofauti na ugumu kati ya hali halisi ya kutaka kupata faida na ile ambayo iko tayari na siyo katika upamoja wa mipango ya faida, kwa kuacha nafasi kubwa ya kazi ambayo inajenga na kutaka kuongeza kwa kile kinachoitwa sekta ya tatu.

Miungu iitwayo fedha: Uchumi wa leo ni ule ambao “unaua” kwa sababu, Papa anasema, “Mtu siyo kiini tena ”,bali  “ anatii fedha tu”, na kutengeneza fedha ndiko kunageuka kuwa suala ambalo liko mstari wa mbele peke yake”.  Kwa maana hiyo ni kama wanavyojenga “ mfumo wa maskini , utumwa na ubaguzi”.

Kiini cha shughuli ya sasa cha kujikita katika fedha kulingana na uchumi halisi, siyo kwa bahati mbaya. Nyuma yake, kuna uchaguzi wa mtu ambaye anafikiri, japokuwa kwa makosa, kwamba fedha zinatengenezwa kwa fedha. Lakini  Fedha za kweli zinatengezwa kwa njia ya kazi. Ukosefu wa ajira suala ambalo linajihusisha na nchi mbalimbali za Ulaya  ni matokeo ya mfumo wa uchumi ambao hauna tena  ule uwezo  wa kuunda ajira, kwa sababu wameweka  kwanza kiini cha miungu  kiitwacho  fedha!

Kazi inaunda kazi nyingine: Unapo muuliza mwekezaji kwa jinsi gani anaweza kuwa “mbunifu” wa thamani kwa ajili ya kampuni yake, na kwa ajili ya wengine, kuanzia katika jumuiya ambayo anaishi na kufanya kazi, kwa maana hiyo Papa anatoa taadhali ya kuona ni jinsi gani ilivyo muhimu “umakini wa mtu kwa dhati”, ikiwa na maana ya kumpatia kila mtu kilicho chake”, “kuwatoa uchungu mama na baba wa familia  ambao hawawezi  kuwapatia watoto wao  wakati endelevu na hata wakati uliopo”

Baba Mtakatifu anasema, hiyo ina maana ya kuongoza , lakini hata kusikiliza, kushirikisha kwa unyenyekevu na matumaini ya mipango na mawazo. Ina maana ya kufanya kwa namna ambayo kazi inaunda kazi nyingine, uwajibikaji, unaunda uwajibikaji mwingine, matumaini, yanaunda matumaini mengine na zaidi kwa ajili ya kizazi cha  vijana ambao leo hii wanahitaji zaidi kuliko hawali. Ni muhimu kufanya kazi pamoja katika kujenga wema wa pamoja,  kuwa na ubinadamu mpya wa kazi, kuhamasisha kazi ya heshima na  hadhi ya mtu ambayo haitazami faida tu, au mahitaji ya uzalishaji, lakini kuhamasisha maisha ya hadhi kwa utambuzi kuwa wema wa mtu na wema wa kampuni vinapaswa kwenda sambamba.

Maendeleo fungamani: Papa Francisko anato wito wa kuendeleza mshikamo na kufanya mpangilio wa uchumi ambao hautoi ubaguzi , kwa kutajirisha natendo ya kiuchumi ambayo yanakuwa na umakini kwa walio maskini na kupunguza ukosefu wa usawa”. Kwa maana hiyo  Papa anaongeza  “ tunahitaji kutiwa moyo na kuwa kweli wabunifu”. Mgawanyo na ushirikishwaji wa utajiri unaopatikana, kuanzishwa kwa  kampuni kwenye eneo , wahusika kijamii, ustawi wa kampuni, usawa katika mishahara kati ya  mwanaume na mwanamke, maelewano kati ya muda wa kazi na muda wa kujikita katika maisha, kuheshimu mazingira, utambuzi wa umuhimu wa binadamu ukilinganisha na mashine na utambuzi wa haki za mishahara , uwezo wa kupyaisha, yote hayo ni mambo muhimu ambayo yanazingatia uhai  wa ukuu wa jumuiya ya kampuni. Ili kundeleza maendeleo fungamani ambayo yanatakiwa umakini wa mada ambazo zimetajwa zote.

Kutenda kiucumi ni jambo la kimadili: Uchumi ulio safi, Baba Mtakatifu anabainisha , hautoi tofauti  na maana ya yule anayezalisha na  kutenda kiuchumi kwani daima ni tendo la kimaadili. Hubaki umeunganisha matendo na uwajibikaji, haki na faida, uzalishaji wa utajiri na mgawanyiko wake, shughuli za kufanya , na kulinganisha na mazingira ambayo yanakuwa ni kitu ambapo kwa wakati kinahakikisha maisha ya kampuni.

Bado kuna kazi ya kufanya kwa ajili ya maendeleo katika ukuu wa ekolojia: Kwa mtazamo huo, maana ya kampuni “inapanuka” na kuwa na utambuzi kwamba kutafuta faida tu hakuhakikishi zaidi maisha ya kampuni, wala hakuna uwezekano wa wahudumu wa kiuchumi ambao wanasikiliza masikini. Na ndiyo maana Papa anafikiria kuwa zaidi ya “mafunzo ya ufundi katika kampuni, inatakiwa hata mafunzo juu ya thamani” ikiwa ni, mshikamano, maadili, haki, hadhi, uendelevu  kwa ajili ya kujitajirisha kwa “mawazo na uwezo wa kubuni”. Kwa mantiki baadaye ya kuwa na maendeleo  katika ukuu wa ekolojia inayotazama juu ya kujikita katika matendo ya dhati  zaidi; kisiasa, kiutamaduni, kijamii, uzalishaji, hata hivyo kazi ya kufanya bado inabaki”.

Kushirikishana katika safari ya pamoja: Baba Mtakatifu amerudi katika suala la kilio cha maskini, kwa kukumbuka kuwa wao wanapoanza mwendo, wanaogopesha watu hasa wanaishi katika ustawi . Kwa maana hiyo Papa anasema, hakuna wakati endelevu wa amani kwa binadamu iwapo hakuna mapokezi ya utofauti na katika mshikamano na kufikiria ubinadamu kama familia moja. Ni wito wake kwa kutazama wahamiaji ambapo anasema, ni changamoto kwa wote leo hii. Safari yao wanayo timiza inaonesha wazi, na safari hiyo kwa hakika hufanyika wawili, hakuna haja ya kuwa na hofu ya kushirikishana nao matumaini. Hata hivyo kwa kutazama juu ya sheria nchini Italia na Ulaya kwa ujumla, Baba Mtakatifu ametoa wito wa kutazama mtu anayekimbia umaskini na njaa na kwamba wawekezaji wasikose kuwa na ujasiri wa kutoa mafunzo kwa watu hao, hata katika shule kwa ajili ya maendeleo ya kweli na mfumo wa utamaduni hasa wa kazi unaotazama wema wa nchi na zaidi ili kuweza kujenga jamii iliyo ya haki na ya kidemokrasia.

Ufungamani na mifumo ya hadhi: Na kwa upande wa wahamiaji, Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa, kuna ulazima wa kuheshimu utamaduni na sheria za nchi zinazo wapokea, ili  kwa namna moja kuweza  kufikia mchakato wa kushirikishwa na kushinda hofu na uchungu wao.  Anawakabidhi uwajibikaji huo hasa ule wa serikali kuwa makini , ili wapate njia za kushirikishana na  kutoa uwezekano wa mapokezi yenye hadhi kwa ndugu kaka na dada wanaohitaji msaada. Lakini pamoja na hayo, anaongeza kusema inawezakana kupokea kiasi cha watu, lakini bila kudharau namna yao ya kushirikishwa na kuwaandaa kwa njia iliyo na hadhi. Ni lazima pia kuwa makini kwa wafanya biashara haramu na wahalifu wanaijiingiza kwa utambuzi zaidi ya kwamba kupoke siyo jambo rahisi.

07 September 2018, 09:25