Tafuta

Vatican News
Papa akizungumza na vijana wa Sicilia Papa akizungumza na vijana wa Sicilia  (Vatican Media)

Papa:vijana wa Sicilia wanaalikwa kujenga wakati ujao na kukaribisha!

Papa alipokutana na vijana, swali la kwanza lilikuwa ni jinsi gani ya kusikiliza sauti ya Bwana? Papa anajibu kuwa ni “kuchagua kwa Imani, kuchagua Kanisa, kuchagua Mediterranea, kwa maana ya kujibidisha kuishi katika ardhi hiyo na kujikita katika kukaribisha, kulinda, kuhamasisha na kushirikisha

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kituo chake cha mwisho cha Papa Francisko huko Palermo kwenye ziara yake ya kichungaji, amewaalika vijana kuota ndoto ya utamaduni wa matumaini , wa furaha na mapokezi na siyo kuangukia katika kumaini kushindwa na mantiki zinakufana uone kuwa hakuna kinachowezekana: badilika, kutembea, kutafuta, kuota na kuhudumia kwa kukutana na kusikiliza Bwana ndiyo mambo msingi aliyosisitiza kwa vijana .

Mchana wa joto huko Palermo, katika Uwanja wa Poleteama, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na vijana alfu tano wa Sicilia, katika kituo chake cha mwisho wa ziara yake ya kitume, mahali ambapo amewaalika hawali ya yote kujikita katika safari ndefu, kwa maana amesisitiza kwamba, si rahisi kusikiliza Bwana wakati umekaa kwenye sofa. Amesema hayo wakati wa kujibu maswali yao, ambapo imekuwa kama desturi sasa  vijana kuuliza maswali na Papa kuwajibu kwa urahisi kama Baba. Taarifa inathiniotia kuwa, vijana tangu saa 9 alasiri walikuwa wakimsubiri mbele Jumba la michezo la Sicilia wakiwa mstari wa nbele kwenye Mkutano wa Kanda, ulioongozwa na mada “ Mwalimu unaishi wapi?”.

Swali: ni jinsi gani ya kusikiliza sauti ya Bwana?: Kijana aliyeuliza swali, Baba Mtakatifu amejibu, “kuchagua kwa Imani, kuchagua Kanisa, kuchagua Mediterranea, kwa maana ya kujibidisha kuishi katika ardhi hiyo na kujikita katika kukaribisha, kulinda, kuhamasisha na kushirikisha. Mungu anasilikizwa wakati ukiwa safarini na katika kumtafuta: Neno la Mungu halisimami, na iwapo wewe umesimama huwezi kulisikia. Mungu anagunduliwa ukiwa katika  hija, kwa maana Bwana anazungumza kwa yule anayetafuta. Anayetafuta anatembea.

Ni bora kuwa  katika utafiti daima ulio mwema; kuhisi umesha fika, hasa kwa upande wao ni hatari Baba Mtakatifu amebainisha, kwa manaa, Yesu anatoa ushauri wa kusikiliza Sauti ya Bwana na kusema :“ Tafuteni na mtapata”. Lakini je ni wapi mahali pa kutafuta? Jibu la Papa anasema, si katika simu ya mkononi.  Kwenye simu hakuna sauti inayofika kwa Bwana. Na hakuna hata katika luninga, mahali ambapo Bwana hana masafa (Chanel). Na hata muziki wa nguvu unaokufanya usisikie. Pale mtandao wa mbingu umekatika! Bwana hatafutwi hata mbele ya kioo, mahali ambapo uko wewe peke yako unajihatarisha  kubaki umekata tamaa ya kubaki jinsi mlivyo.

Je unataka kufanya jambo ambalo linaokuogopesha? Baba Mtakatifu anasisitiza, “Fanya na uwe na uvumulivu. Wote tumefanya mengi. Kupoteza sura katika hilo siyo tatizo la maisha. Tatizo la maisha ni pale unaposhindwa kujaribisha maisha. Hilo ndilo janga kama uoti maisha! Ni bora kuchagua ndoto nzuri za mawazo, badala ya kuwa mvivu wa hali halisi: ametumia msema wa kilugha chao kuwa: “bora kuwa na Don Chisciotte che Sancho Panza!

Oteni ndoto kubwa na fanya lolote kwa ajili ya wengine: Oteni ndoto kubwa, kwa maana katika ndoto kubwa, utapata hata maneno mengi ya Bwana ambaye yupo  anazungumza kitu kwako. Na fanyeni kitu chochote kwa ajili ya wengine, msijikunyate ninyi binafsi. Na wale wenye kuitwa jina la umimi, na mimi, na kwa ajili yangu na watu wanaoishi kwa ajili yao binafsi , mwisho wake wanaishia kuwa asidi.

Mkristo hasiye kuwa na mshikamano siyo mkristo: Kadhalika Baba Mtakatifu akijibu swali la msichana, Gaia wa Caltanissetta ameipongeza Sicilia kwa kusema : “ni jinsi gani anahesabika mkristo anayepokea na kutoa hadhi ya binadamu katika ardhi kama ya Sicilia , ambayo daima ndiyo kituo cha watu wa mataifa! Wao ni watu wa makutano ya utamaduni wa watu. Hiyo si kwamba ni jambo la utamaduni mzuri wa tamaduni tu, bali ni ujumbe wa imani. Kwa maana hiyo wito wao utakuwa kwa hakika wa wanaume na wanawake wa makutano. Kukutana na kufanya wengine wakutane; kukuza mikutano kwa sababu dunia ya leo iko katika vita na mivutano”.

“Ninyi ni watu na utambulisho mkubwa na mnapaswa kufunguka kwa ajili ya watu wote ambao kwa nyakati zote wamwekuwa wanakuja kwenu. Na kazi ya ushirikishwaji, ya kukaribisha, kuheshimiana hadhi ya wengine, mshikamano kwenu ninyi si mapendekezo mema kwa watu walio elimika, lakini ni jambo la kawaida kwa mkristo. Na mkristo hasiye kuwa na mshikamano siyo mkisto”.

Kujenga wakati endelevu wakiwa wanachafua mikono: Baba Mtakatifu akiendelea: “ mnapswa kuwa wajenzi wa wakati endelevu ambo uko mikononi mwenu! Fikirieni vizuri. Hamwezi kuchukua simu ya mkononi na kuita kampuni iwatengenezee wakati endelevu: wakati endelevu lazima uutengeneza wewe na mikono yako, moyo wako, upendo wake, shauku yako na ndoto zako. Na wengine, kwa kukaribisha na kutoa huduma kwa wengine”.

Wanahitajika wanaume na wanawake wanaotoa taarifa ya mambo mabaya: Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito kwa vijana waweze kutoa taarifa ya mambo mabaya kama vile unyonyaji kwa mana anasema: “ tunahitaji wanaume na wanawake wa kweli na msiwe na hofu ya kutoa taarifa, hata kuwakaripia! Maisha ni mapamban, kutoa taarifa na kujadiliana , kujiweka katika mchezo wa maisha kwa ajili ya wazo halisi.” Vijana wameitwa kuwa mapambazuko ya matumaini: Swali la mwisho lilikuwa linahusu juu ya kuishi katika ardhi hiyo kama kijana, ambapo Baba Mtakatifu amejibu ya kwamba wao wanaitwa kuwa mapambazuko ya matumanini. Matumaini ya mapambazuko huko Palermo katika kisiwa cha Sicilia, Italia na Kanisa, lakini kwanza ni kuanzia kwao. Na ameonya kuwa wasiangukie katika mantiki ile ya kuona kuwa hakuna lolote la kufanya kwa maana hiyo ni dhana potofu na mbaya amesisitiza Baba Mtakatifu!

Tafuteni mzizi na kuiishi. katika nyakati hizi za kipeo, Baba Mtakatifu ameuliza je ninyi mnayo mizizi? Kila mmoja ajibu kimya rohoni mwake: mzizi yangu ni ipi au umeipoteza? Je mimi ni kijana mwenye kuwa na mzizi au ambao haupo tena: Sina mzizi hata kidogo kuwa mwenye asidi? Akifafanua amengoeza: lakini mizizi hiyo inatokana na kukutana na utamaduni, katika mazungumzo na wengine na zaidi kwa kuzungumza na wazee. Ni wazee ambao wanaweza kuwapatia mzizi. Siyo rahisi kuunda matumaini bila kuwa na mzizi na hivyo tafuteni mizizi. Kuota na kuishi utamaduni wa matumaini, utamaduni wa furaha, utamaduni wa kuwapo katikati ya  watu, katika familia, utamaduni unaotambua kujifunza kutoka katika mzizi thabiti  kwa ajili ya kuchanua wakati ujao.

 Sala ya Papa kwa vijana: Kabla ya kuwaacha vijana, Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya vijana: Ee Bwana, tazama vijana hawa. Wewe unatambua walivyo na utashi wa kwenda mbele ili kutengeneza dunia iliyo bora. Ee Bwana wasaidie wawe watafutaji wa mema na furaha, wajikite katika matendo ya hija na makutano ya wengine, wawe wahudumu kwa dhati  na  wanyenyekevu wa kutafuta mizizi na kuipele mbele ili kutoa matunda na kuwa na utambulisho wa uwepo wao katika ardhi. Ee Bwana wasindikiza vijana wote katika safari na uwabariki wote.

 

16 September 2018, 12:15