Cerca

Vatican News
Zawadi ya misalaba iliyotolewa na Papa kwa ajili ya waamini na mahujaji wote katika uwanja wa Mtakatifu Petro 16 Septemba 2018 Zawadi ya misalaba iliyotolewa na Papa kwa ajili ya waamini na mahujaji wote katika uwanja wa Mtakatifu Petro 16 Septemba 2018  (ANSA)

Papa:Salam na shukrani za kwa watu wa Palermo,Sicilia!

Papa Francisko baada ya kumaliza sala ya Malaika wa Bwana, amekumbuka kwa furaha kubwa ziara yake akiyoifanya tarehe 15 Septamba 2018 huko Palermo. Amewashukuru kwa ukarimu wao na kuwabariki. Wakati huo akatoa hata zawadi ya misalaba

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mara Baada ya kusali sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko amekumbuka siku ya Jumamosi 15 Septemba 2018, alipotembelea  huko Palermo na kuwashukuru wote walioshirikiana kwa pamoja kufanikisha ziara yake ya kitume na kwamba ni  “watu wa maajabu katika ardhi nzuri ya Sicilia, kwa makaribisho yao ya upendo” na kwa maana hiyo ameongeza: “kwa mfano na ushuhuda wa Padre Puglisi tuendelee kuangazwa sisi wote na kuthibitisha kwamba wema una nguvu zaidi ya ubaya, upendo ni wa nguvu zaidi ya chuki”. “Bwana awawabariki ninyi nyote wa Sicilia na ardhi yenu! Tuwapigie makofu watu wa Sicilia”, Baba Mtakatifu ameomba!

Papa uwanjani ametoa zawadi ya msalaba

Badaye kwa kushangaza watu wote waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 16 Septemba 2018, Baba Mtakatifu amesema “  ni siku mbili mara baada ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, kwa maana hiyo nimefikiria kuwazawadia msalaba ninyi nyote mliopo katika uwanjia huu. Msalaba ni ishara ya upendo wa mungu ambaye kwa njia ya Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Ninawaalika kuipokea zawadi hiyo na kuipeleka katika nyumba zenu, katika vyumba vya watoto au wazee…

Msalaba siyo kifani ni ishara ya dini

 “ kila mahali popote lakini uonekane katika nyumba. Siyo kitu kama  kifani, lakini ni ishara ya kidini kwa ajili ya kutafakari na kusali. Kwa kutazama Yesu msulibiwa, ni kutazama wokovu wetu. Si wa kununua. Iwapo mwingine atakueleza lazima ununue, basi anatumia ujanja, Baba Mtakatifu amebainisha na kusema hapana, kwa maana hiyo ni zawadi kutoka kwa Papa. Ninawashukuru watawa, amskini wakimbizi ambao kwasasa watawagawia zawadi hiyo ndogo lakini yenye thamani! Daima imani inatokana na mambo madogo na vitu vinyenyekevu.

17 September 2018, 11:10