Tafuta

Vatican News
Papa Francisko wakati wa mlo wa Pamoja katika Kituo cha  Missione di Speranza e Carita' Papa Francisko wakati wa mlo wa Pamoja katika Kituo cha Missione di Speranza e Carita'  (Vatican Media)

Papa Francisko amepata mlo na maskini na wafungwa!

Mara baada ya Misa katika Foro Italico Palermo, Papa Francisko amekwenda katika sehemu yenye Kituo cha Utume wa Matumaini na Upendo, kilicho anzishwa na ndugu Biagio Conte. Hapo amepata mlo na maskini, wafungwa na watu waliopembezoni mwa jamii

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kwaya ya watoto waliimba Francisko, Francisko, wimbo wenye jina la Mare, Mare yaani Bahari, bahari  ulioandikwa na sisita mmoja, pia kurusha mapuzo wakati wakimpokea Baba Mtakatifu katika kituo cha Utume wa “Matumaini na Upendo katika mtaa wa Decollati mjini Palermo. Katika kituo hicho Papa amepata  mlo wa mchana na maskini, wahamiaji, wafungwa walioachiwa na watu wa kujitolea. Lakini wakati huo huo hata , nje ya jengo hilo, kulikuwa na watu 1,300 walio kuwa wanakula wakati huo na Papa akiwa na watu wengine ndani ya jengo.

Wote tuko mtumbwi mmoja: Papa akisindikizwa na Askofu Corrado Lorefice wa Jimbo la Palermo, amewasalimia karibu watu zaidi ya 50, na ndani ya jengo hili kulikuwa na mtumbi uliotengenezwa na zana zilizochakachuliwa kwa kuwakilisha mtumbwi. Ni sanaa iliyoandaliwa na fundi selemara mmoja kutoka nchi ya Tunis na ni kiziwi. Wanajumuiya wa kituo hicho cha kimisionari ni wanawake kutoka mataifa mbalimbali , ambao wametengeneza baadhi ya sanamu dogo ndogo zinazo wakilisha  watu mbalimba wa mataifa duniani. Sanamu hizi ndogo zimewewa juu ya mtumbwi huo, kwa kutoa ujumbe kuwa “ wote tuko katika mtumbwi mmoja ili kujenga kwa pamoja dunia iliyo bora.

Chakula cha Papa: Mboga  ya matunda ya mizaituni iliyohifadhiwa, jibini, mkate, saladi ya wali, cous cous, kuku, saladi na keki zilizo andaliwa na watawa kutoka mataifa  mbalimbali ya kimisonari. Ni orodha iliyopendekezwa kwa Papa,  ambayo iliandaliwa na bidhaa zilizovunwa kutoka katika  shamba ka misioni ya Tagliavia, Scopello, na Villa Florio. Watu wa kujitolea na wanaume na wanawake ambao wamekaribishwa  katika utume wa Ndugu Biagio ndiyo waliotoa huduma ya Baba Mtakatifu.

16 September 2018, 10:35