Tafuta

Vatican News
Baba Matakatifu ameweka mawaridi eneo alipo uwawa Padre Pino Puglisi na kusali Baba Matakatifu ameweka mawaridi eneo alipo uwawa Padre Pino Puglisi na kusali 

Maombi ya Papa mbele ya eneo alipo uwawa Padre Puglisi

Katika mtaa wa Branacaccio, mahali ambapo Padre Pino Puglisi aliwawa, Papa Fancisko amejikita kwa kimya katika sala mara baada ya kuweka mawaridi mbele ya medali ya shaba mahali pale ambapo palitokea janga la kuwawa kuhani huyo.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mtaa wa Branacaccio, mahali ambapo Padre Pino Puglisi aliwawa, Papa Fancisko amejikita kwa kimya katika sala mara baada ya kuweka mawaridi mbele ya medali ya shaba mahali pale ambapo palitokea janga la kuwawa kuhani huyo.

Baba Mtakatifu amefika katika Uwanja uitwao Anitha Garibald Brancacio, mahali ambapo Padre Pino Puglisi aliwawa, na kupokelewa na umati wa watu kwa furaha kubwa. Alitelemka katika gari, na baada ya kuwasalimia baadhi ya watu, amemkaribisaha msichana mlemavu aliye mzawadia mawaridi.

Ndugu wawili wa Padre Pino mbele ya nyumba kukaribisha Papa

Baada ya kubariki, amekaa kimya kwa sala mbele ya medali ya shamba, mahali ambapo padre Puglisi aliuwawa na Giuseppa Grigoli, kwa kutumwa na kikundi cha kihalifu cha mafia. Baba Mtakatifu baadaye aliptanda katika jumba la makumbusho lilipewa jina la Padre Pino akisindikizwa na Askofu Mkuu Corrado Lorefice wa  Palermo. Na nje ya jengo hili, alisubiriwa na kaka zake wawili wa Padre Pino, Gaetano na  Franco Puglisi,  wakiwa na wake za ona familia  zao.

16 September 2018, 11:26