Tafuta

Ziara ya Kitume ya Papa Francisko Jimbo la Armerina na Palermo Ziara ya Kitume ya Papa Francisko Jimbo la Armerina na Palermo  

Hatua ya kwanza ya Papa Francisko katika Uwanja wa Armerina!

Katika Uwanja wa Armerina, Papa Francisko ametambua misalaba na mateso ya eneo la Sicilia na kutoa wito katika kutoa maisha la Kanisa la Upendo wa kimisionari ambao hauishii tu kama dhana ya ufadhili wa kupenda watu wote

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu ameamua kukumbatia watu wa Kisiwa cha Sicilia, kwa kuanzia katika uwanja wa Armerina  wa jimbo.  Amegusa eneo hili la katikati ya Kisiwa mnamo saa 2.40 za Asubuhi ya tarehe 15 Septemba 2018 kwa kutua katika Uwanja wa mpira wa Mtakatifu Ippolito, mahali ambapo amepokelewa na Askofu  Rosario Gisana, Mkuu wa Wilaya ya Enna, Maria Antonietta Cernigli na  Meya wa mji Nino Cammarata katika uwanja wa Armerina. Wakati akiwa njiani kuelekea  katika Uwanja wa Ulaya, amelakiwa na shangwe kuu za waamini walio kuwa pembeni mwa barabara na  uwanjani  kwa vyombo vya muzini na nyimbo za Jumuiya ya vijana.

Papa awatia moyo jumuiya hai:  Mbele ya mateso makubwa, jumuiya ya Kanisa ni hai na ya kinabii wakati Kanisa likitafuta njia za kutangaza na kutoa huruma. Ndiyo maeneno kuitia moyo ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo wambia waamini wote waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Armerina, ambao wamepokea kwa furaha kubwa wakati wa kutoa hotuba yake ya kwanza. Kadhalika amewaelekeza matumaini mara baada ya kupokea salam kutoka kwa Askofu Rosario Gisana ambaye amekumbuka juu ya uchaguzi wa umaskini wa Kanisa mahalia, ambapo hata Papa mwenyewe amesisitiza juu ya  matatizo ambayo yanaleta “vizingiti vya utulivu wa eneo hilo”.

Majanga ya Sicilia:  “Majanga ya Sicilia yanayoikumba siyo machache, Papa anakumbusha kuwa: “Hayo yana jina”, na kuyataja kwamba ni “ ukosefu wa maendeleo ya kijamii na utamaduni; unyonyaji wa wafanyakazi, ukosefu wa hadhi ya ajira kwa vijana; uhamiiaji wa familia nzima; kula riba; ulevi, na madwa ya kulevya; mchezo wa kamali; mtatanuo wa mahusiano ya familia”.

Baba Mtakatifu anaendelea kuwa, “ kufikiria majanga ya jamii na ya Kanisa siyo tendo la dhana  ya uharibifu na kuona mambo yote ni mabaya” na hivyo anatoa ushauri kwa wote kuwa na  juhudi “ kwa ajili ya uinjilishji mpya katika eneo hilo la katikati, kuanzia katika misalaba na mateso binafsi”. Utume unaweza kushinda kwa mara nyingine  katika “ kupendekeza uso wa Kanisa la Umoja na  la Neno; Kanisa la Upendo wa Kimisionari; na Kanisa jumuiya ya Ekaristi”.

Kanisa lenye huruma: “ Kanisa lenye huruma, daima ni aminifu zaidi katika Injili na liko wazi kukaribisha  wote wanaohisi kushindwa kimwili na kiroho, au wale waliobaguliwa pembezoni mwa jamii”. Kutokana na hilo ,Baba Mtakatifu ameendelea kukumbushia juu ya  nafasi  ya  “Kanisa la upendo wa Kimisionari” ambalo linatimiza hilo linapohisi “ huruma ya Kiinjili kwa magonjwa mengi ya wat, na kugeuka kuwa mitume wa huruma inayotembea katika eneo zima.”

Upendo wa Kikristo siyo ufadhili: Papa Francisko akiendelea kufafua zaidi,  amewatia  moyo wa kuendelea katika huduma ya Kanisa ambayo inajieleza katika “matendo ya dhati”, lakini ameonya ya kwamba wasiangukie katika upendo wa kikristo kama dhana ya ufadhili. Na kwa maana hiyo ni lazima kutoa msukumo  “ kwa mitume na Jumuiya nzima kujikita katika kutafuta kwa dhati sababu za taabu hizo”.

Vijana wa furaha ni wasanii wa riziki yao: Hata hivyo Papa Francisko amesisitiza kuwa “ dhana ya upendo wa kimisionari ni ile pia ya  kujitoa kwa ajili ya vijana na matatizo yao”. Akiwasalimia vijana waliokuwa katika uwanja wa Armerina, amesema “ wawe na furaha ya kisanii kwa ajili ya riziki yao”. “ tambueni kuwa Bwana anawapenda: Yeye ni rafiki wa kweli na mwaminifu ambaye hatawaacha kamwe; Kwake yeye mnaweza kutumaini”!

Kwa mapadre: wasihubiri zaidi ya dakika 8 : Baba Mtakatifu pia amerudi katika Tema ya Kanisa kama jumuiya ya Ekaristi  na akifafanua hilo amasema: “ Kutoka katika Ekaristi, tunachota upendo wa Kristo ili kuupeleka katika njia za dunia, kwenda Naye ili kukutana na ndugu”. Kutokana na hili Baba Mtakatifu amewashauri ya kutoangaikia zaidi ya kuwa na namba kubwa ya wanao udhuria katika Misa Takatifu kwamba: “ Ninawapa wito wa kuishi heri za udogo; kama vile kuwa, mbegu ya aladali, zizi dogo, fungu la chachu ndogo, mwanga imara, na chembe ndogo ya chumvi”. Aidha akuwageukia mapadre, na kusema kuwa, katika Misaa: “ wakati mwingine kuna anayesema: mimi siendi Misa, kwa maana mahubiri yanadumu dakika 40, ninakerwa, lakini hiyo siyo vizuri: Misa nzima lazima idumu dakika 40! Mahubiri yanayodumu zaidi ya dakika 8 siyo vizuri”. Kadhalika kwa mapadre amewapa ushauri: “ iwapo unamalizia siku ukiwa umechoka sana, hiyo ndiyo dalili nzuri”

Mapadre na maaskofu kuitwa katika umoja: Baba Mtakatifu hakukosa kulalamika kuwa, katika Ekaristi , na  Padre ambaye anaadhimisha ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutengana na hivyo amewashauri mapadre kushikana pamoja na maaskofu kati yao: “ Mmeitwa kuwa wa kwanza kuishinda boma la nguzo, na machukizo ambayo hutengenisha; mmeitwa kuwa wa kwanza kutafakari kwa unyenyekevu mbele ya historia ngumu ya matatizo ya ardhi hii”.

Kumbukumbu ya padre Pino Puglisi: Katika hitimisho lake, akisalimia waamini wote,amekumbuka kwa shukrani kuwa Padre mfiadini Pino Puglisi na ambaye Baba Mtakatifu anaadhimisha  Misa Takatifu  Palermo kwamba: “ Nimejua kuwa miaka 25 iliyopita, mwezi mmoja kabla ya kuwawa kwake, yeye aliishi siku kadhaa katika Uwanja wa Piazza Armerina”, hivyo padre aliyeuwawa, “  ni maaisha ya  kinabii, kwa maana yeye alijikabidhi, si kama padre tu, lakini kwa  ajili ya waamini wa jimbo hili: kwa ajili ya upendo wa Yesu, katika kuhudumia ndugu hadi mwisho”!

15 September 2018, 10:49