Ziara ya kitume ya Papa Francikso  Jimbo la Palermo, Sicilia Ziara ya kitume ya Papa Francikso Jimbo la Palermo, Sicilia 

Papa:Mapadre na maaskofu wanaalikwa kuungana pamoja

Baba Mtakatifu anawakumbusha mapadre na maaskofu kuwa, katika Ekaristi na Padre ambaye anaiadhimisha ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutengana na hiyo amewashauri mapadre kushikana pamoja na maaskofu kati yao kwa maana wameitwa kuwa wa kwanza kuishinda boma la nguzo, na machukizo ambayo hutengenisha

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika Ekaristi na Padre ambaye ana adhimisha ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutengana na hivyo Baba Mtakatifu mewashauri mapadre kushikana pamoja na maaskofu kati yao: “ Mmeitwa kuwa wa kwanza kuishinda boma la nguzo, na machukizo ambayo hutengenisha na ; mmeitwa kuwa wa kwanza kutafakari kwa unyenyekevu mbele ya historia ngumu ya matatizo ya ardhi hii”. Amethibitisha hayo wakati wa hotuba yake ya kwanza katika Uwanja wa Armerina tarehe 15 Septemba 2015 katika ziara yake ya kitume kutembelea Kisiwa hiki cha Sicilia. 

Kumbukumbu ya padre Pino Puglisi

Katika hitimisho lake, akisalimia waamini wote,amekumbuka kwa shukrani kuwa Padre mfiadini Pino Puglisi na ambaye Baba Mtakatifu anaadhimisha  Misa Takatifu  Palermo kwamba: “ Nimejua kuwa miaka 25 iliyopita, mwezi mmoja kabla ya kuwawa kwake, yeye aliishi siku kadhaa katika Uwanja wa Piazza Armerina”, na hivyo padre aliyeuwawa ni “  hata ya kinabii, kwa maana yeye alijikabidhi,, si kama padre tu lakini kwa  ajili ya waamini wa jimbo hili: kwa ajili ya upendo wa Yesu, katika kuhudumia ndugu hadi mwisho”! 

15 September 2018, 10:09