Tafuta

Vatican News
Katekesi ya Papa Jumatano 5 Septemba 2018 Katekesi ya Papa Jumatano 5 Septemba 2018  (Vatican Media)

Papa:Dominika ni siku ya kufanya amani ya historia binafsi!

Dominika ni siku ya kufanya amani na historia yako binafsi. Mapumziko siyo mkusanyika wa raha tu na likizo bali ni kubariki hali halisi. Ndiyo kiini cha Kateksi ya Papa Francisko tarehe 5 Septemba 2018 katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, akifafanua juu ya Amri ya Mungu ya pumziko siku Takatifu ya Mungu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu katika katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 5 Septemba 2018, ameendelea na ufafanuzi juu ya amri ya Mungu, hasa kwa kujikita katika  amti ya kutakatifuza sikukuu yani “pumziko la  siku  Takatifu ya Mungu”. Na kwamba amani ya kweli haipatikani katika kubadili historia binafsi, bali kuikubali na kuithamanisha. Kadhalika anasema, amani lakini inachaguliwa na hailazimishwi, wala kuipata kwa bahati mbaya. Yeye anafikiria kuwa, hiyo ni amri rahisi ya kutimiza, japokuwa  sio jinsi ilivyo kwa sababu kuna pumziko lililo rahisi na lingine ni gumu la kutimiza.

Kiwanda cha chechele, siyo pumziko la kweli

 

Jamii ya sasa kwa dhati ina kiu ya kujipatia raha na kwenda kupumzika kwa kujifurahisha katika kiwanda  cha chechele ambacho katika ulimwengu ndiyo chenye kuchukua nafasi ya mawazo, kwa mfano  katika uwanja wa michezo mahali ambapo wote wanafurahia,lakini pamoja na hayo Baba Mtakatifu  anatoa onyo na kuuliza je safari ndefu  nyingineza za matembezi ya mbali yanajaza moyo kweli? Wakati mwingine kuna mitndo, ambayo inapendekezwa, kama vile kusikia mtu huyo anafanikiwa anajulikana na kuruhusu nafasi kubwa za raha. Mantiki hii lakini inapelekea kutoridhisha maisha, kwa maana kwa maana siyo mapumziko ya kweli bali ni katika kuikimbia hali halisi.  

Dominika ni siku ya kufanya amani na maisha. Na inaelezea hali halisi ya pumziko ya kwamba  ni kipindi cha kusifu, ni  kipindi cha kutazama hali halisi na kusema: “ ni jinsi gani maisha yalivyo mazuri!”. Amri ya Mungu inapinga kupumzika wakati unaikimbia hali halisi badala yake inaonesha kwamba kupumzika ni kama “kubariki hali halisi”. Na kwa wakristo kiini cha siku ya kupumzika yaani Dominika ni siku ya Ekaristi, maana yake ni kushukuru.

Dominika sio siku ya kufuta siku nyingine, bali ni kuzikumbuka, kuzibariki na kufanya amani ya maisha. Baba Mtakatifu anauliza swali, ni watu wangapi, wengi ambao wanao uwezo wa kujifurahaisha, lakini hawaishi kwa amani. Dominika ni siku ya kufanya amani na kusema kuwa maisha ni tunu; japokuwa  siyo raisi, Papa anasisitza kwamba wakati mwingine ni uchungu lakini ni tunu.

Amani haishurutishwi, inachaguliwa

Wakati ikiwa ni  rahisi kusali kwa moyo ukiwa hauna furaha, katika kubariki na kufurahia ni kinyume kwa babubu ni mzunguko moyo ulio komaa ambao unafungulia wema. Wema kwa hakika haulazimishwi bali unachaguliwa, anasisitiza Baba Mtakatifu na kuongeza kusema: hiyo ni kama ilivyo amani ambayo “ inachaguliwa na haiwezekani kushurutishwa, wala kupatikana kwa bahati mbaya”.

Ni lazima kujipatanisha na historia binafsi , kwa matendo yasiyo kubalika na katika sehemu ngumu za maisha. Ameongeza swali: “kila mmoja wenu je  anajipatanisha na historia yake binafsi? Hilo ni swali la kutafakari: “je mimi ninajipatanisha na historia yangu?  Amani ya kweli kwa hakika inabadilisha historia binafsi, lakini inatakiwa kuipokea na kuithamanisha kama jinsi ilivyo.

Akiendelea na ufafanuzi wake, Baba Mtakatifu ametoa mfano wa wakristo wangonjwa wanaojifariji kwa utulivu na ambao haupatikani kwa wale ambao wanatafuta  kwa nguvu zote mambo ya raha ya maisha zitolewazo, utajiri na sifa. Maisha yanaaza kuwa mazuri inapofikia hatia ya kuanza kufikiria vema historia binafsi , yaani unapoanza kuona zawadi ya wasiwasi na hasa kwa yule anaye ona kila kitu ni neema, kuwa na mawazo matakatifu yanayoanza kutengeneza nguzi ya kutotosheka na  kutamani  pumziko la kweli. Kwa neno moja iwapo unagunda kile ambacho mzaburi anasema: “ Ni kwa Mungu tu moyo wangu utapumzika; hii ni Zaburi nzuri amehitimisha Baba Mtakatifu Kateksi yake kuhusu Amri ya Pumziko la siku ya Mungu na kuitakatifuza!

 

 

05 September 2018, 13:01