Tafuta

Vatican News
Papa anasema Mang’amuzi ya kweli yanahitaji kuelimishwa juu ya kuwa na uvumilivu wa Mungu na nyakati zake, ambazo siyo za kwetu Papa anasema Mang’amuzi ya kweli yanahitaji kuelimishwa juu ya kuwa na uvumilivu wa Mungu na nyakati zake, ambazo siyo za kwetu 

Ni kufanya mang'amuzi ili kufikia mapenzi ya Mungu!

Kuanzia tarehe 5 – 8 Septemba unafanyika Mkutano wa XXVI wa kiekumene kimataifa wa tasaufi ya Kiorthodox katika Jumuiya ya Wamonaki wa Bose. Katika Telegram ya Papa Francisko, anawashauri kuendelea kukuza ule uwezo wa kung’amua na elimu ya uvumilivu katika utambuzi wa nyakati za Mungu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mang’amuzi ya kweli yanahitaji kuelimishwa juu ya kuwa na uvumilivu wa Mungu na nyakati zake, ambazo siyo za kwetu. Ndiyo maneno msingi yanayo someka katika Telegram ya Papa Francisko, iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, ambayo imetumwa kwa waandaji wa Kongamano la XXVI la Kiekumene kimataifa la Tasaufi ya kiorthodox ambalo limenza tarehe 5 na litamalizika tarehe 8 Septemba 2018 katika Jumuiya ya Wamonaki wa Bose.

Baba Mtakatifu akiwatumia Baraka Takatifu, anawatakia mema katika siku hizi za kukabiliana kindugu ili siku hizo ziweze kukuza ile hali ya kutafuta dhana ya mang’amuzi binafsi na kijumuia, iliyo ya lazima katika kufikia utambuzi na mapenzi ya Mungu yenye makao yake kwa kila ujazo wa maisha.

Mang’amuzi  na maisha

Mang’muzi na maisha ya kikristo ndiyo mada ya ambayo imegeuka kuwa sehemu ya kuu ya mazungumzo na urafiki na Makanisa ya kiorthodox. Kutambua maana yake kufanya mang’amuzi na ishara za nyakati ni sehemu msingi ya maisha ya kikristo na mkristo ambaye anapaswa afuate na kutambua upyaisho, pamoja na kwamba bado inabaki  imesimikwa mizizi ya imani kwa ajili ya kujibu changamoto za sasa.

Kazi ya mkutano huo ambao ni sehemu yaKanisa na wataalam wakuu kwa ngazi ya dunia kama vile hata wawakilishi wa kiekumene wakimuimishwa na Padre Enzo Bianchi , Mwanzilishi wa Monasteri ya Wamonaki kike na Kiume huko Bose, Askofu wa Kiorthodox Irinej wa Sakramenti ambaye atatoa mada juu ya ukuu wa Biblia na historia ya kufanya mang’amuzi.

Utambuzi wa vizingiti na dhambi

Katika tukio hili anashiriki hata Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Ushauri na kuhamasisha umoja wa wakristo atakayejikita katika ujumbe wake juu ya mantiki mbili za mang’amuzi, kiroho, kitaalimungu, na kichungaji, kwa kuonesha namna ya kuweka mikono katika madonda ya Kristo kama vile alivyofanya Mtakatifu Tomas  ili kuimarisha imani na kutafuta kwa udhati ubinadamu ulio jeruhiwa.

Pamoja na hayo upo hata  waraka uliotumwa na Patriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli Bartholomeo I ambaye ameleza  juu ya mang’amuzi kama jambo muhimu cha maisha ya Kanisa, na zawadi yenye thamani ya Mungu aliye mwanzilishi na fadhila ya Kanisa na akiendelea kulisha na kuonesha kila aina tokeo  kwa njia ya ushuhuda wa Kanisa katika ulimwengu, na si katika mang’amuzi peke yake, anaongeza, bali ni hata katika utambuzi wa vikwazo vyetu na hali halisi ya dhambi.

 

 

 

 

05 September 2018, 15:29