Kardinali Sandri akiwa huko Venezia  katika Shirika la Warmeni mechitaristi Kardinali Sandri akiwa huko Venezia katika Shirika la Warmeni mechitaristi 

Il Papa kwa wa Mechitarista: Endelea kuangaza maisha ya watu wa Armeni

Ni mwaka wenye fursa ya kumshukuru Bwana kwa ajili ya wingi wa neema na karama walizopokea kwa miaka mingi Shirika la Warmenia Mechitaristi. Hayo maandishi ya Barua ya Papa katika fursa ya maadhimisho ya miaka 300 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Warmeni Mechitaristi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni mwaka wenye fursa ya kumshukuru Bwana kwa ajili ya wingi wa neema na karama walizopokea kwa miaka mingi Shirika la Warmenia Mechitaristi. Hayo maandishi ya Barua Ya Papa katika fursa ya  maadhimisho ya miaka 300 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Warmeni Mechitaristi. Barua hiyo imesomwa tarehe 16 Septemba  wakati wanafanyaLiturujia ya  maadhimisho hayo katika kisiwa cha Mtakatifu Lazaro wa Armeni huko Venezia Italia

Barua ya Papa iliyo andikwa tarehe 5 Septemba 2018 kwa ajili ya maadhimisho ya hayo  ilitumea kwa  Boghos Levon Boghos Zékiyan, mwakilishi wa Papa kwa ajili ya Shirika hilo. Barua hiyo imesomwa tarehe 16 wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo huko Venezia katika Kisiwa ambapo Kardinali Leonardo Sandri ameudhuria maadhimisho hayo, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

Imani iliyo hai hadi kifodini

Katika barua hiyo Papa amekumbusha wajumbe wa Shirika kuwa, wameishi maisha yao kwa uaminifu, na si mara chache, kuwa ushujaa wa kushuhudia na wakati mwingine hata kutoa sadaka ya ufiadini. Anathibitisha hayo kwa kutazama sura ya mtumishi wa Mungu Mechitar , mmoja wa waanzilishi wa Monasteri ya Makanisa ya Mashariki, ambapo Papa amesisitiza juu ya mchango wake, katika ujenzi  wa kuimarisha  imani ya watu wa Armenia, ambapi anasema ni moja ya kieleleza cha kitasaufi na utamaduni wa watu wake. Kwa maana hiyo amewaalika Shirika wahifadhi, watafakari na kusambaza utajiri huo kwa ajili ya wema wa watu wa Armenia, hasa tunu ya kitasaufi na utamaduni ambao unawahusu.

Ufunguzi wa kiekumene

Pamoja na hayo katika barua, Papa amewakumbusha mambo kadhaa kwa namna ya pekee yenye thaman; utamaduni wa ubinadamu katika taalimungu ya kiermeni inayojikita kwa namna ya pekee katika mwongozo wao kikanunu na kwamba, inaelezea wazo la msanii wa mambo matakatifu ya sayansi na sana. Kadhalika ameonesha juu ya asili ya kazi ya Mechitar hasa katika kuendeleza kutoa taalimungu, falsafa, historia, nyaraka na  mashule. Na zaidi kwa mujibu wa Papa ameonsha  ule ufunguzi  wazi wa njia ya uekumene ambao unajikita katika tasaufi ya Mechitaristi , na juu ya utamaduni wa Kanisa la Armenia kuunganika na wengine , kwa mfano wa Mtakatifu Gergorio wa Narek ambao amethibitisha kuwa leo hii unajionesha zaidi katika ishara ya nyakati kwa kutembea pamoja ili  kuelekea umoja kamili.

Ukaribu wa Vatican katika majaribu

Baba Mtakatifu pia amekubumbushia juu ya majaribu na hawa katika ukosewa wa kutoleeleweka na matatizo ambayo Mechitar na Shirika walikutana nayo. Pamoja na hayo anasema waliweza kupata suluhisho na kwamba matatizo hayo  ni sehemu ya karama, hata leo hii kwa kiasi kikibwa. Kutokana na hilo, ameonesha jinsi gani Vatican imekuwa  daima  na utambuzi wa Mechitar, hasa kwa namna ya pekee kutazama hayo kwa umakini. Na pia ukaribu wa Vatican na Shirika hili wakati wa kipindi nyeti kwa kutoa kila iwezekanavyo msaada.

 

 

 

 

 

 

17 September 2018, 15:24