Cerca

Vatican News
Sala mbele ya Mnara wa waathirika wa ubaguzi dhidi ya wayahudi nchini Lithuania Sala mbele ya Mnara wa waathirika wa ubaguzi dhidi ya wayahudi nchini Lithuania  (AFP or licensors)

Sala ya Papa katika maeneo ya kihistoria nchini Lithuania!

Baba Mtakatifu Francisko ametembele maeneo yenye historia kubwa ya nchi ya Lithuania. Amesali sala kwa kusema maeneo haya:“Mungu wangu, Mungu wangu, kwanini umeniacha? Kilio chako Ee Bwana, hakikosi kusikika katika kuta hizi”…

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndiyo imekuwa hatua mwafaka na cha kiini katika ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi za Kibaltiki, mahali ambapo mjini Vilnius mchana wa tarehe 23 Septemba 2018, ameweza kupitia  katika ngome za kumbukumbu: Mnara kwa ajili ya mtaa wa kibaguzi wa wayahudi, Jumba la makumbusho ya mateso na kupambania uhuru, pamoja na Mnara wa waathirika wa utawala wa kisovietiki.

Sala mbele ya Mnara kwa ajili ya wa mtaa wa kibaguzi

Baba Mtakatifu amejikita katika sala kwenye mnara wa kibaguzi na kwa kukumbuka janga la mauaji ya kibari na kuchukuliwa kwa wayahudi. Ni katika kumbukumbu ya  mwaka wa 75 tangu kuvunjwa kwa mtaa huo wa kibaguzi mjini Vilnius . Baba Mtakatifu ameweka taji la mau katikatika ya uwanja wa Rudininku. Katika chini ya  Lithuania, kabla ya kuingiliwa na utawala wa nguvu wa kizovietiki, walikuwa wakiishi wayahudi 250,000. Watu waliochukuliwa kutoka katika mtaa wa kibaguzi, tarehe 23 Septemba 1943, karibu wote waliuwawa kinyama. Leo hi nchini Lithuania wanaishi karibia wayahudi 4,000.

Ziara ya Jumba la Makubusho ya kuingiliwa na mapambani dhdi ya uhuru

Hatua ya pili ya Baba Mtakatifu na ya kina ilikuwa ni kusimama kimya kwa sala katika jumba la makumbusho na mapambano dhidi ya kuwania uhuru.  Ni sehemu ambayo inakumbusha kuingiliwa  kwa nguvu za  udikteta  na kisovietiki, kwanza na polisi na majeshi ya Gestapo na baadaye wajeshi wa kisovietiki wa Kgb, ambao walitesa kikatili  na kuwaua karibia milioni ya wafungwa. Papa Francisko ametembelea kwa namna ya pekee katika vyumba vya kubaguliwa, namba 9 na 11, vilivyokuwa vidogo sana, na mahali ambao wamewasha mshumaa. Katika chumba namba 11 zimebandikwa picha na historia ya baadhi ya maaskofu katoliki walioteswa kwa ajili ya kutetea imani yao, kati yao ni Askofu Mkuu Teofilo Matulionis, aliyetengazwa mwenyeheri tarehe 25 Juni 2017. Katika jengo hili aliuwawa kunako tarehe 18 Novemba 1946, pia Askofu Vincentas Borisevičius, wa jimbo la  Telšiai.  Kimya pia kimewa ongoza hadi katika chumba cha mauji kinyama. Baba Mtakatifu Francisko baadaye ametia saini katika kitabu cha wageni, kama  kukumbuka ya ziara yake hiyo.

Sala ya tatu ya Papa katika Mnawa wa waathirika wa maingilio ya kisovietiki

Baba Mtakatifu baadaye ameendelea mbele hadi katika Mnara wa waathirika kwa maingilio ya serikali ya Kisovietiki. Katika eneo hilo linaendelea kuhifadhi historia nzima. Papa Francisko amejikita pia katika sala: “Kilio chako ee Bwana hakikomi kusikika, na kujiegemeza kati ya kuta hizi kwa kukumbuka mateso ya wana wako wengi wa watu hawa”. Kilio chako ee Bwana, kituokoe na magonjwa ya kiroho ambayo sisi watu wako daima tunashawishika: tunasahau babu zetu na wale wote ambao waliishi na kuteseka” Ee Bwana , usiruhusu kamwe sisi tuwe viziwi dhidi ya kilio cha wote ambao leo hii wanaendelea kupaza sauti zao mbinguni”.

Utawala wa kidiketa na kisovietiki

Mwaka 1944 majeshi ya udikteta yalivamia nchi za kibaltiki na kuungana na serikali ya Kisovietiki. Zaidi ya wazalendo 200,000 kati ya nchi za Estonia, Latvia na Lithuania walichukuliwa nchini Siberia au walilazimika kukimbilia nchi za nje. Kwa maana hiyo Askofu Katoliki aliyeponea chupuchupu dhidi ya utawala na mateso ya kisovietiki, pia amemsindikiza Papa Francisko kwanza katika Mtaa wa waathiria wa utawala wa kisovietiki. Na mwisho wa ziara hiyo katika eneo lililokuwa linatawaliwa na kumbukumbu kwa sala Baba Mtakatifu amerudi Ubalozini.

24 September 2018, 10:17