Tafuta

Vatican News
Papa Francis huko  Kaunas nchini Lithuania Papa Francis huko Kaunas nchini Lithuania  (ANSA)

Papa:Gundua mapema fitina ya kudhuru mazingira na utamaduni!

Miaka 75 iliyopita nchini Lithuania, kulitokea katika mjini Vilnus uharibifu wa mtaa wa kibaguzi, kwa maana hiyo, ndiyo ilikuwa hitimisho la maangamizo ya maelfu ya wayahudi. Baba Mtakatifu amekumbuka hayo mara ya Misa Takatifu katika uwanja wa Santakos huko Kanaus Jumapili 23 Septemba 2018 kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika sala ya Malaika wa Bwana kwenye uwanja wa Kaunas nchini Lithuania, Papa Francisko amekumbuka miaka 75 tangu kuvunjwa kwa mtaa mjini wa wayahudi huko Vilnius walimokaa na kuwawa maelfu. Kwa maana hiyo ametoa wito kwa wakristo wagundua kila wakati kichipukizi kipya cha tabia  ya kuweza kudhuru na kufukuzia mbali katika mazingira  na katika utuamauni na ili pasiwepo kamwe uwezekano wa tabia ya ubaguzi wa kila aina .

“Miaka 75 iliyopita nchini Lithuania, kulitokea mjini Vilnus uharibifu wa mtaa wa kibaguzi, kwa maana hiyo, ndiyo ilikuwa hitimisho la maangamizo ya maelfu ya wayahudi. Baba Mtakatifu amekumbuka hayo mara ya Misa Takatifu katika uwanja wa Santakos huko Kanaus Jumapili 23 Septemba 2018 kabla yak usali sala ya Malaika wa Bwana.

Tufanye kumbukumbu ya wakati ule na kumwomba Bwana aweze kutupatia zawadi ya mang’amuzi ya kugundua kila wakati kichipukiza cha tabia ya hatari, kila mvumo wa hewa yenye ubaya wa moyo ambayo inataka kuingia katika moyo wa kizazi kipya ambacho hakikukuwahi kufanya uzoefu huo na ambao unaweza kuleta madhara ya kurudi nyumba katika kukumbuka sauti za ving’ora vya wakati ule. Pamoja na hayo mawazo pia yamwendea hata kwa jumuiya ya wahayahudi, wakati wa sala ya malaika wa Bwana na kuwakumbusha kuwa mchana atakwenda na kuomba sala mbele ya mnara wa Waathirika wa  mtaa wa kiyahudi mjini Vilnius.

Mwovu huongozwa na tabia yake mbaya na hufuatilia mwenye haki

Katika tafakari yake, amejikikita kutazama sura ya mwovu, ambaye anataka kupendekeza itikadi zake ya kufutalia mwenye haki na kwamba tendo la uwepo wa mwenye haki mbele yake, umletea shida, kwa maana hataki wengine wafanye vizuri , na kujiweka kimbelembele kwa maana ya tabia yake inayomtuma afanye hivyo. Ni tabia ambayo inajikita kuwa na sumbuko la roho ya kutaka kuwa mbele daima, kama watu wengine ambao uamini kuwa ndiyo wakuu, wenye kuamini wanastahili haki walizopata na kwa faida zaidi.

Kukaa na walio baguliwa

Jambo ambalo Yesu anapendekeza wakati ukiwa na msukumo huo unaonekana moyoni na katika, “mawazo ya jamii”, ni kujifanya wa mwisho. Kukaa mahali ambapo hakuna anayependa kwenda Baba Mtakatifu anathibitisha; hakuna anayefika na hakuna chochote kinachofika huko katika pembezoni mwa jamii na mbali; ni kuhudumia, na kuunda nafasi ya makutano na walio wa mwisho na kubaguliwa. Iwapo wenye nguvu wangeweza kuamua hilo, iwapo wangeweza kuruhusu Injili ya Kristo ifike kwa kina katika maisha yetu, katika maana hiyo, utandawazi wa mshikamano, ungeweza kweli kuwa hali halisi.

Kutoa umakini kwa wale waliobaguliwa na wachache

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari, amekumbuka pia kilima maarufi cha misalaba kilichopo chini Lithuania, mahali ambapo maelfu ya watu, kwa karne nyigni wamezidi kwedna na kuendelea kusimika ishala ya msalaba: Kutokana na hilo, amesema “ ninawaalika wakati tunasali sala ya Malaika wa Bwana, kumwomba Mama Maria atusaidie kusimika msalaba wetu wa huduma, katika kujitoa kwa dhati , mahali ambapo kuna mahitaji ya walio baguliwa, walio wachache na ili kuweza kuondolea mbali kabisa katika mazingira yetu na katika  utamaduni wetu, ule uwezekano wa kurudi kuangamiza mwingine, kumbagua na kuendelea kubagua yule ambaye unahisi nakuletea usumbufu kwa kuwa anakuharibia kuishi maisha yako ya raha.

 

23 September 2018, 15:10