Tafuta

Papa  Francis Wakati wa Misa katika huko   Kaunas Papa Francis Wakati wa Misa katika huko Kaunas 

Papa huko Kaunas: Kanisa linalotoka kujikita kwa ajili ya wadogo

Katika Misa Takatifu ya kwanza kwenye ziara nchini Lithuania na katika nchi nyingine za Kibaltiki, kwenye uwanja wa Santakos, Papa ameomba “kupona kwa kumbukumbu ya historia yetu” na ili kuweza kujikita katika ujenzi wa wakati uliopo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tunapaswa kuwa Kanisa “linalotoka nje” na pia  msiwe na hofu ya kutoka na kujitoa hata kama ni kufikiri hakuna suluhisho, kujitoa hasa kwa ajili ya wadogo, waliosahuliwa na wale ambao wanaishi pembezoni mwa maisha yao”. Katika kupona majeraha ya kumbukumbu ya historia, Siberia, mtaa wa wayahudi huko Vilnius na Kaunas, kuingiliwa na uhamisho, kwa ajili ya “kushiriki katika ujenzi wa sasa”. Ndiyo wazo kuu katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko mbele ya waamini zaidi ya 100,000 waliokusanyika katika uwanja wa Kaunas tarehe 23 Septemba 2018, ikiwa ni Misa yake ya kwanza katika ziara yake ya Lithuania; ataendelea katika nchi ya Latvia na Estonia. Mahubiri yake, yamejikita katika mafundisho ya Yesu kwa mitume wake wakiwa katikati ya safari yake kuelekea Yerusalem na Mateso yake kwa mujibu wa Injili ya Mtakatifu Marko.

Uchungu wa kuingiliwa na uhamisho

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake, kwa  kufafanua Injili anasema, ni kama vile Yesu anataka mitume wake, wapyaishe uchaguzi wao kwa kutambua kuwa ufuasi wao utajikita katika kipindi cha “majaribu na uchungu”. “Maisha ya kikristo daima yanapitia katika kipindi cha msalaba na wakati mwingine ni kuona kuwa hakuna mwisho. Kizazi kilichopita walioona kama vile moto wa kipindi cha kuingiliwa na uchungu kwa wale waliokuwa wanachukuliwa”. Wasiwasi kwa wale ambao walikuwa hawarudi, aibu ya mashtaka ya kificho na usaliti”.

Imani ilipatikana huko Siberia na katika mitaa ya wayahudiwa  huko Vilnius na Kaunas

Papa Francisko akitazama maelfu na maelfu ya waamini wa Lithuania mesema: “ni watu wangapi kati yenu wanaweza kutusimulia binafsi au historia kutoka kwa ndugu, hatua hiyo ambayo imesomwa”. Ni wangapi kati yenu wameona hata imani ikiendelea kwa maana Mungu hukutoweka katika kuwalinda; kwa maana tendo la kubaki waamini aikutosha tu kama Yeye hasinge ingilia kati katika historia yenu. Kaunas inatambua hali halis; Lithuania nzima inatoa ushuhuda na msisimko kwa kutaja jina tu la Siberia au mtaa wa wayahudi huko Vilnius na Kaunas, kati ya nyinginezo.

Mitume kuzozana ni nani atakuwa mkubwa zaidi

Katika kuelezea juu ya mitume waliokuwa wanajadiliana juu ya nani atakuwa mkubwa, Papa Francisko anamtaja Mtume Yakobo katika barua yake inayosimulia kuwa “wale wenye kuwa na wivu na ugomvi, ndio walio na machafuko ya vita”. Kwa maana hiyo namesema, “Lakini mitume hawakuwa wanataka Yesu azungunze kwao juu ya uchungu na msalaba; hawakutaka kujua chochcote cha majaribu na uchungu.  Na ndiyo maana walirudi nyumbani wakizungumza ni nani angeweza kuwa mkuu zaidi”. Baba Mtakatifu anafafanua kwa maana hiyo: shauku ya utawala na utukufu ni njia ya pamoja katika mwenendo kwa wale ambao hawawezi kuponya kumbukumbu ya historia yao, na labda kwa njia hiyo hawakubali hata kujibidisha katika kazi ya wakati uliopo. Kwa hiyo ndiyo maana ya kujadili juu ya utukufu huo zaidi, aliyekuwa mwenye sifa wakati uliopita , aliye na haki zaidi na aliye mstari wa mbele kupewa heshima na wengine.

Si kukataa historia bali kujikita katika wakati uliopo

Papa Francisko anaendelea, “tunakana historia yetu”,na hapa ametaja Waraka wa “Evangelii Gaudium”, yaani Furaha ya Injili, isemayo kuwa: “ utukufu unatokana na historia ya sadaka, ya matumaini, ya mapambano ya kila siku, na kuchakarika katika maisha ya huduma na uthabiti wa kazi ngumu. Kukana historia yetu ndiyo tabia tasa na itapaswa kuikataa na kujikita katika ujenzi wa wakati uliopo, kujitoa na kupotelea ndani ya mawasiliano ya hali halisi ya mateso ya watu wetu waamifu. Baba Mtakatifu ametoa mfano kuwa, hatuwezi kuwa kama “wataalam” wa kiroho ambao wanahukumu tu kwa nje na hutumia wakati wote kuzungumza juu ya “nini kinachotakiwa kifanyike”.

Kuweka katikati ya walio wachache, wasio na ajira, wazee na vijana

Yesu kabla ya kuzungumza, aliweka mtoto katikati. Je ni nani leo hii asubuhi ya Jumapili atajiweka katikati? Papa Francisko ameuliza. Je wadogo ni wakina nani, maskini zaidi ya sisi, ambao tunapaswa kuwapokea baada ya miaka 100 ya uhuru? Kwa yule ambaye hana chochote cha kurudisha, kufurahisha nguvu zetu, na kujikatalia? Labda ni wale wa kabila ndogo za miji yetu, au wasio na ajira, ambao wanalazimika kuhama. Labda ni wazee ambao wako peke yao, au vijana ambao hawapati maana ya maisha kwa maana wamepoteza mizizi yao.

Kanisa moja lisilokuwa na hofu ya kutoka nje na kupotelea ndani yake

Kama niko katikati, hakuna anayeweza kujifanya haoni, hakuna anayeweza kudai siyo mwajibikaji wa wengine, Papa Francisko amethibitisha. Bila kutaka ukuu, bila kutaka sifa, au kuwa wa kwanza. Hiyo ni kwasababu uwapo Vilnius imeguswa na mto wa Vilnia, na kumwaga maji yake na kupoteza jina la Neris; hapa ni sawa na kusema kuwa Neris ambayo inapoteza jina lake na kutoa maji yake katika Nemunas”. Katika mfano huo inajihusisha na Kanisa moja la kutoka nje, na lisiogope kutoka na kujitoa hata kama inaonekana kutokuwa na suluhisho, Kanisa linalopotea nyuma ya wadogo , waliosahaliwa  na wale wanaoishi pembezoni mwa jamii. Kwa utambuzi lakini kuwa tendo la kutoka nje kwa kesi nyingine ni kuthibitisha hatua na kujeweka kwa upande wa mahangaiko na dharura, kutambua kutazama kwa macho, kusikiliza na kusindikiza wale waliobaki pembezoni mwa barabara.

Kumbukumbu ya mapatano, upendo kwa ajili ya changamoto ya wakati

Akihitimisha Baba Mtakatifu, amesema, “tupokee Yesu katika Neno lake, katika Ekaristi, na wadogo. Na ili Bwana aweze kupatanisha kumbukumbu yetu na kutusindikiza katika wakati huu, aendelee kutufanya kuwa na upendo kwa ajili ya changamoto, kwa ajili ya ishara zake anazotuachia.  Ili kuweza kuhisi, jinsi gani furaha na matumaini, mateso na uchungu wa waamini wa nyakati zetu, hasa maskini na wanaoteseka. Na ili tuweze kuhisi mshikamano wa jumuiya ya mji, nchi yote ya Lithuania, na hisitoria yake, ni kutaka kujitoa katika maisha ya huduma, kwa furaha na kwa kuwafanya watambue wote kuwa Yesu ni matumaini yetu.

 

 

23 September 2018, 14:17