Cerca

Vatican News
Mkutano wa Papa na Vijana wa Lithuania katika uwanja wa Kanisa Kuu la Vilnius Mkutano wa Papa na Vijana wa Lithuania katika uwanja wa Kanisa Kuu la Vilnius  (Vatican Media)

Papa awashauri vijana wasichezee maisha,Yesu yuko kila kona zao!

Baba Mtakatifu wakati wa kukutana na vijana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Vilnius, amesisitiza kuwa Mungu, “hatashuka kamwe kutoka katika maisha yenu”: Yesu anatuzawadia wakati mpana na mkarimu , mahali ambapo kuna nafasi hata katika kufilizika”.Msiache kamwe kujijenga hata kama wakati mwingine tunajibidisha kubomoa”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuanza mazungumzo  na vijana, ambapo kama desturi sasa, ni vijana wanao anza kuuliza maswali na hivyo mazungumzo ya Papa Francisko na vijana yametiwa joto na maswali mawili ya vijana Monica na Jonas. Na katika kuwajibu amesema maisha siyo shughuli ifanyikayo katika  jumba la maonesho. Kinyume chake ni historia ya kweli na ya dhati, ambapo unaweza kugundua njia za Bwana kwakuwa Mungu anapita daima katika maisha yetu.

Ushuhuda wa Monica

Ushuhuda wa historia ya Monica ulikuwa unahusu juu ya kupokea zawadi ya imani kurithishwa na bibi yakeambaye ana uhusiano mzuri. Maisha yake akiwa mdogo alikuwa na uhusino mbaya na baba yake maana Baba yake alikiwa akimpiga.Pamoja na hayo, hali ya baba yake baada ya kufilizika kampuni yake, aliwaza kujiua  na ndipo akaanza kulewa sana. Kwa upande wa Monika akazidi kuongeza chuki dhidi yake . Lakini katika parokia moja ya Kifransiskani akaweza kukutana na jumuiya na yenye kukaribisha na kumpokea.Kwa maana hiyo, Bwana alianza kumponya majeraha. Na Monika akaomba msamaha baba yake na kubadili chuki kuwa ya huruma na sala. Lakini kwa bahati mbaya Monica baadaye alikuwa akabiliane na uchungu mwingine, kwa maana baba yake alijiua, Monica anasema, “siwezi kufikiria leo hii , kwa maana sijuhi jinsi gani ningeweza kuishi  hadi sasa iwapo ningehifadhi chuki ndani ya moyo wangu hadi kufikia kifo cha baba yake.

Ushuhida wa Jonas

Hata katika maisha ya Jonas, inaonekana hatua ya Mungu, Kwa maana madaktari walipomwambia kuwa anao ugonjwa ambao taratibu, taratibu ungeweza kuharibu mwili wake, alitambua jinsi gani ilivyo kuwa  muhimu kusindikizwa na mwenzake yaani mke wake. Amesisitiza kuwa kilichomsaidia hasa ni imani kwa Mungu. Jonas, mara tatu kwa wiki anapaswa kwenda hospitali na kubadilisha damu na wakati huo huo amethibitisha kuwa anayo matumain ya kupona. Katika kipindi hiki ameongeza kusema ni mwafaka katika maisha yake. Anamwamini Mungu, Bwana ana mpango juu ya maisha yake. Mungu na familia ndiyo mwamba wa kujiegemeza, kwa matumaini na msaada wa furaha na katika uchungu.

Monica na Jonas kama Kanisa Kuu la Vilnius

Mara baada ya kusikiliza ushuhuda wa Monika na Jonas, Papa Francisko amethibitisha kuwa, vijana hawa wawili wamefanya uzoefu, kama vile Kanisa Kuu la Vilnius, katika hali ngumu. Mara nyingi Baba Mtakatifu amekumbuka juu ya  Hekalu hilo ambayo ilichomwa moto mara nyingi , Lakini walikuwapo daima ambao waliamua kuijenga kwa upya. Hata uhuru wa nchi yao ameongeza Baba Mtakatiufu kuwa, imejengwa juu ya wale ambao hawashindwi  na  hofu kubwa na matukio mbalimbali ya kiajabu.

Kwenda kinyume na mambo ya wakati huu

 Neema ya Mungu inakuja kwetu anaongeza Papa, kwa njia ya watu ambao tunakutana nao katika historia na maisha yetu. Akiendelea anasema: Jumuiya ya kifransiskani kwa ajili ya Monica na Mke wa Jonas, imekuwa uwepo  wa msaada madhubuti wa kwenda mbele , kwa ajili ya kutembea katika matumaini. Hakuna yoyote anaweza kusema mimi ninajiokoa. Bwana anatuokoa na kutufanya kuwa sehemu ya watu. Kutokana na hili, Papa Francisko ametoa ushauri daima wa  kukimbilia katika kutafuta  utakatifu kwa kuanzia na makutano na jumuiya ambayo imeundwa na wengine. “ Ni uthibitisho halisi ya kuwa kile kinachotukia kwa mwingine kinaweza kutokea hata kwangu mimi, hivyo ni muhimu kwenda kinyume  na mantiki ya ubinafsi ambao unaunda upweke,na kutufanya tuwe wabinafsi, wabatili, wenye kuhangaikia tu kutengeza sura na ustawi kibinafsi.

Kuwasaidia wengine

Maisha yetu ya kweli yanategemea na uwepo wa watu. Haupo utambulisho wa maabara  na wala utambulisho wa kufuta. Upo utambulisho wa kutembea pamoja, wa kupambana kwa pamoja  na kupenda pamoja, upo utambulisho wa kuwa na familia na watu. Kutazama udhaifu wa wengine, Papa Francisko anabainisha, unatuweka katika hali halisi na kuishi tukilambalamba majeraha yetu. “Wapendwa vijana ni bora kufuata Kristo! Amewashauri. “Ni vijana wangapi wanondoka katika nchi yao, kutokana na ukosefu wa fursa! Ni waathirika wangapi wa sumbuko la roho, ulevi na madawa ya kulevya. Ninyi mnatambua vema. Ni wazee wangapi wako peke yao na hawana mtu wa kushirikishana uwepo na hofu ya kuona kwamba wanarudia  wakati uliopita. Ninyi vijana mnaweza kujibu changamoto hizi kwa uwepo wenu na kukutana kati yenu na wengine. Yesu anatusindikiza, ni safari ya sauku kubwa ambayo inajaza maisha yenu ya maana, ambayo inatufanya tuhisi kushiriki na kuwa sehemu ya jumuiya moja ambayo inatia moyo, katika jumuiya moja ambayo inatusindikiza  na inayo tuwajibisha katika kutoa huduma”

Kuna nafasi ya kila mmoja

Maisha siyo shughuli ya kisanii katika jumba la michezo, au video ya michezo kwenye mtandao. Maisha lazima kuyacheza katika wakati uliopo ukiwa na mahusiano katika moyo na Mungu; wakati mwingine yana heri ya kwenda mbele  na wakati mwingine ni kurudi nyuma, yanatoa majaribu na kujaribu njia, na yanabadilika. Jambo la hatari zaidi Papa Fracisko anabainisha, ni lile ya kuchanganya safari kama vile kupitia njia ya (labirynty) njia isiyo na ukomo, kwa maana ya ile tabia ya kuzungukia utupu kwa njia ya maisha, kujizunguka binafsi bila kupata njia ya kutokea ndani ya barabara ya kukupeleka mbele”!

“Msiwe na hofu ya kutoa uamuzi kwa Yesu, kukumbatia lengo lake, hasa la Injili , ya ubinadamu wa kuwa mtu. Kwa maana yeye hatashuka kamwe kutoka katika mtumbwi wa maisha yenu, yeye atakuwa pale pale  katika kona ya njia zenu na hivyo msikose kamwe kujijenga, hata kama wakati mwingine tunajitahidi kubomoa. Yesu anatuzawadia makati mpana na mkarimu, mahali palipo na nafasi ya kushindwa, mahali ambapo hakuna yoyote anayetaka kuhamia, kwasababu kuna nafsi ya wote. Wengi watakuja kujaza mioyo , kwa kunyunyizia dawa katika shamba la matarajio yenu kwa magugu mabaya, lakini mwishowe, iwapo Bwana ndiye mwenye nafasi, daima mbegu bora itashinda.

Papa Francisko kabla ya kwenda ndani ya Kanisa Kuu la Vilnius katika sala na tafakari fupi katika Kikanisa kidogo cha Mtakatifu Kasimir , amewashauri hatimaye vijana wasisahau mizizi yao, watu wake wenyewe badala yake waipeleke mbele.

 

23 September 2018, 10:09